MACHO YA MWANADAMU 2
*🖊 MACHO YA MWANADAMU 🖊* SOMO LA PILI Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 BWANA YESU ASIFIWE 🖊 Napenda nikukumbushe kuwa mwanadamu anamacho ambayo yanaweza kumletea matokeo mazuri au mabaya katika maisha yake 🖊 Kupitia macho mwanadamu huona ,kisha hutafakari na kufanya maamuzi mazuri au mabaya . 🖊 Maamuzi hayo ya mwanadamu yanaweza kumponza siku zote za maisha yake . 🖊 Tambua kuwa mtu hawezi kupenda bila kuona au kusikia lakini katika kupenda kwake hutangulia kuona , kisha kutamani na kupenda . 🖊 Kwasababu macho ya mwanadamu ni taa ya mwili wake yanaweza yakamkosesha na Mungu . 🖊 Macho kwa sababu ya kuona mwanadamu huingia katika majaribu na kutenda dhambi 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻 📖 22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Mathayo 6 :22 23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! Mathayo 6 :2...