MACHO YA MWANADAMU 2

*πŸ–Š MACHO YA MWANADAMU πŸ–Š*


SOMO LA PILI

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829




BWANA YESU ASIFIWE



πŸ–Š Napenda nikukumbushe kuwa mwanadamu anamacho ambayo yanaweza kumletea matokeo mazuri au mabaya katika maisha yake

πŸ–Š Kupitia macho mwanadamu huona ,kisha hutafakari na kufanya maamuzi mazuri au mabaya .


πŸ–Š Maamuzi hayo ya mwanadamu yanaweza kumponza siku zote za maisha yake .


πŸ–Š Tambua kuwa mtu hawezi kupenda bila kuona au kusikia lakini katika kupenda kwake hutangulia kuona , kisha kutamani na kupenda .


πŸ–Š Kwasababu macho ya mwanadamu ni taa ya mwili wake yanaweza yakamkosesha na Mungu .

πŸ–Š Macho kwa sababu ya kuona mwanadamu huingia katika majaribu na kutenda dhambi


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.

Mathayo 6 :22

23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!

Mathayo 6 :23


πŸ–Š Ayubu mtumishi wa Mungu aliliona hili jambo .

πŸ–Š Aliona kwamba macho ya mwanadamu yametawaliwa na zinaa kwa asilimia kubwa sana mwanadamu huanguka kwa kuona .


πŸ–Š Ndipo Ayubu alisema hivi


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?

Ayubu 31 :1

2 Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini, Na urithi wa Mwenyezi utokao juu?

Ayubu 31 :2

3 Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu?

Ayubu 31 :3

4 Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote?

Ayubu 31 :4

5 Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;

Ayubu 31 :5

6 (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

Ayubu 31 :6

7 Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;

Ayubu 31 :7

8 Basi na nipande, mwingine ale; Naam, mazao ya shamba langu na yang'olewe.

Ayubu 31 :8

9 Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;

Ayubu 31 :9

10 Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake.


Ayubu 31 :10

11 Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;

Ayubu 31 :11

12 Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang'oa maongeo yangu yote.


Ayubu 31 :12


πŸ–ŠMacho ya mwanadamu yanaweza kumkoseha akawa adui wa Mungu .

πŸ–Š Mfalme Daudi alipokuwa ghorofani juu alimwona Bathsheba mke wa Uria akioga akamtamani .

πŸ–Š Kwasababu ni mfalme aliwatuma watu wake wamfuate yule mwanamke akafanya naye uzinzi

πŸ–Š Bathsheba alipata mimba siku hiyo , na Daudi mfalme,alifanya njama ya kumuua Uria ili amuoe Bathsheba .Jambo hili lilimkasirisha sana Mungu .

πŸ–Š Nataka nikwambie kwamba macho ya mwanadamu yanaweza kumfanya aangukie kwenye zinaa .


MACHO YA MWANADAMU JUU YA MAAMUZI YA KUOA NA KUOLEWA


πŸ–Š Siku zote mtu anapohiji kuoa kitu cha kwanza ni kuona ni nani anataka kumwoa anaumbo gani ,ana vitu gani , ana uchumi kiasi gani .


πŸ–Š Ndyo ni vizuri saana kuangalia hivyo kwa macho ya kibinadamu

πŸ–Š Lakini ni hasara kwa mwanadamu kufanya maamuzi kwa kuona uzuri na vitu vingine amilikivyo mtu bila kutumia macho ya Mungu ( macho ya rohoni ) .


πŸ–Š Kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa kwa macho ya mwanadamu bila macho ya rohoni ni kujitaftia uangamivu mkuu na kujitakia uadui na Mungu .


πŸ–Š Mfalme Suleiman alitumia macho ya kibinadamu akajitosa kuwaoa wanawake ambao Mungu kamkataza .


πŸ–Š Kwa sababu hakuzingatia macho ya rohoni aone mbele yake kuna nini alijiingiza kuwaoa wanawake waabudu miungu wakamkosesha kwa Mungu .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

1 Wafalme 11 :1

2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

1 Wafalme 11 :2

3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

1 Wafalme 11 :3

4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
1 Wafalme 11 :4

5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

1 Wafalme 11 :5

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

1 Wafalme 11 :6

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

1 Wafalme 11 :7

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.

1 Wafalme 11 :8

9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,

1 Wafalme 11 :9

10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

1 Wafalme 11 :10

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.

1 Wafalme 11 :11

12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.

1 Wafalme 11 :12

13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.

1 Wafalme 11 :13


πŸ–Š Watu wengi wamekuja kukosea wenzi wa ndoa zao kwasababu ya macho yao .

πŸ–Š Watu hawa wamekaribisha vita kali ndani ya ndoa zao kwasababu walitazama kwa macho ya kibinadamu

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

1⃣ Anavutia

2⃣ Anamiliki utajiri


πŸ–Š Vigezo hivi vimewafanya wanadamu wakosee kuoa au kuolewa .

πŸ–Š Jambo la muhimu sana hapo ni

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

1⃣ Ni wangu kweli kutoka kwa Mungu ?

2⃣ Anaupendo ?

3⃣ Anatabia njema ?

4⃣ Ni mcha Mungu ( ana hofu ya Mungu )

5⃣ Atatunza familia ?


πŸ–Š Lakini kwasababu ya macho ya kibinadamu watu wengi wamenaswa na mitego ya ibilisi .


πŸ–Š Usipangiwe kuoa au kuolewa kwako na wanadamu tafta kupangiwa na Mungu

πŸ–Š Usijipangie kuoa au kuolewa kwa macho yako tafta macho ya Mungu yakuonyeshe mwenzi sahihi wa ndoa .


πŸ–Š Ukifta mashauri ya wanadamu  wataka kukosea sana , wewe mtafte Mungu ndiye mshauri mkuu .


πŸ–Š Shida ya vijana wengi ni wepesi kutafta mashauri ya wanadamu kuliko Mungu


πŸ–Š Mashauri ya wanadamu siku zote huja kwa kile wakionacho katika macho yao wenyewe na siyo macho ya Mungu .


πŸ–Š Ndyo maana unatakiwa kuwa makini sana na wanadamu macho yao yamejaa tamaa

πŸ–Š Watakushauri kulingana vipaumbele vya macho yao kama vile mwonekano na umiliki wa vitu huku wakishindana na aliyejuu yaani Mungu Mtakatifu ambaye mawazo yake hayafanani na mawazo ya mwanadamu .


πŸ–Š Napenda nikwambie kwamba kile ukionacho kwa macho yako kisikupe uamuzi wa kwamba kinakufaa


πŸ–Š Ili kionekane kinakufaa unahitaji kutumia macho ya Mungu ( macho ya rohoni  ) siyo macho ya mwanadamu .


πŸ–Š Wanadamu wanaweza kukiona kwamba hakikufai kwasababu ya macho yao lakini kwa sababu ya macho ya Mungu kinakufaa .

πŸ–ŠWaache wakiseme vibaya maana ni chako kwa kuwa Mungu kakupa wewe hicho hawajakupa wao

πŸ–Š Ukitafta wakupe kile wakionacho kwa macho yao utakosea kuoa au kuolewa.


πŸ–Š Angalia habari hii

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

Hesabu-Numbers 12 :1

2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

Hesabu-Numbers 12 :2

3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

Hesabu-Numbers 12 :3

4 Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.

Hesabu-Numbers 12 :4

5 Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.

Hesabu-Numbers 12 :5

6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.

Hesabu-Numbers 12 :6

7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
Hesabu-Numbers 12 :7

8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

Hesabu-Numbers 12 :8


πŸ–Š Macho kama ya Miriam na Haruni yapo mpaka makanisani haijalishi wengine wanajiita watumishi wa Mungu msikilize Mungu katika maamuzi yako usisikilize matakwa ya wanadamu .


Mungu akubariki sana

Ni mimi

Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829

francispeter424@gmail.com


Usikose somo la tatu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*