🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



🔰 BWANA YESU ASIFIWE


🖊 Nakukaribisha tena katika somo hili wewe ndugu au rafiki yangu wa imani tujifunze kwa pamoja .


🖊 Kufunga na kuomba kuna faida kubwa sana kwa kila aliyempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake


🛐 *NAMNA GANI UTAFUNGA NA KUOMBA* ?


🖊 Utakapoanza kufunga na kuomba utaona mafanikio makubwa sana kiroho .Sasa unatakiwa upitie hatua fulani ili upate muda mzuri wa kuzungumza na Mungu .


🛐 *HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUFUNGA NA KUOMBA* 🔰


1⃣ _WEKA MALENGO YAKO📖🖊


🔰 Kwanini unafunga ? Je unafunga kwa sababu ipi ama kwa 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

🖊 Kurudisha uhusiano wako na Mungu

🖊 Kutafta uongozi wa Mungu

🖊 Kutafta uponyaji .


🖊 Kwa ajili ya suluhu ya tatizo

🖊 Kutafta namna ya kutatua tatizo .


Mwambie Roho Mtakatifu akuongoze na kukupa maelekezo katika malengo ya kufunga kwako .

Hii itakusaidia uombe kwa kulenga kwenye eneo maalumu na kwa ustadi zaidi .


Kupitia kufunga na kuomba tunajinyenyekeza kwa Mungu ili Roho Mtakatifu awe na nafasi kubwa ndani yetu na nguvu ya uponyaji ionekane .


📖 *_14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao_*


2 Mambo ya Nyakati 7 :14



2⃣ JITOE KATIKA MFUNGO


✍🏻 Ombea aina ya mfungo ambao unaenda kuufanya .


📖 16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.


Mathayo 6 :16

17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;


Mathayo 6 :17

18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.


Mathayo 6 :18


📖 14 Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?


Mathayo 9 :14

15 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; *ndipo watakapofunga* .


Mathayo 9 :15


✍🏻 Kila amfuataye Yesu Kristo lazima afunge .

🔰KABLA YA KUFUNGA AMUA YAFUAYAYO :

⏹ Unafunga kwa mda gani ?
Ni mlo mmoja kwa siku ,Siku moja, wiki ,mwezi,siku arobaini .Kama wewe unaanza kufunga anza kidogo kisha utakuja kuvuka viwango vya juu .


⏹ Aina ya mfungo ambao Mungu anataka ufanye kwa mfano unaweza kunywa maji tu au juisi na maji na ni aina gani ya juisi utakunywa na ni mara ngapi ?


⏹  Ni shughuli gani za nguvu hutafanya .

⏹  Utatumia muda gani katika kuomba na kusoma neno .

Usifunge bila kuwa na mda wa kuomba na kusoma neno .



3⃣ JITAYARISHE MWENYEWE KIROHO

✍🏻Msingi mzuri wa kufunga na kuomba ni toba .

✍🏻 Dhambi isiyotubiwa huzuia maombi kujibiwa .


🔰 MAMBO YA KUFANYA ILI KUUANDAA MOYO WAKO


⏹ Mwambie Mungu akusaidie kuzijua dhambi zako zote.

⏹ Tubu dhambi zako zote ambazo Roho Mtakatifu amekukumbusha


📖 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.


1 Yohana 1 :9


⏹ Wasamehe wote waliokukosea na waliokuumiza


📖 4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].

Luka 11 :4


📖 3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.


Luka 17 :3

4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.


Luka 17 :4



📖 25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.


Marko 11 :25


⏹Rejesha upya moyo wako kama akuongozavyo Roho Mtakatifu


⏹ Mwambie Mungu akujaze Roho Mtakatifu na amri na ahadi zake .


📖 18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Waefeso 5 :18


📖 14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.


1 Yohana 5 :14

15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.


1 Yohana 5 :15


⏹  Yatoe maisha yako kwa Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako .Usitii mambo ya dunia .

📖 1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.


Warumi 12 :1

2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Warumi 12 :2


⏹  Tafakari sifa za Mungu ,

🖊 Upendo wake

🖊 Ukuu wake

🖊 Uweza wake

🖊  Hekima yake

🖊  Uaminifu wake

🖊 Neema yake


🖊 Huruma yake


📖 9 Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako.


Zaburi 48 :9

10 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki;


Zaburi 48 :10


📖 1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.


Zaburi 103 :1

2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.


Zaburi 103 :2

3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,


Zaburi 103 :3

4 Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,


Zaburi 103 :4

5 Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;


Zaburi 103 :5

6 Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.


Zaburi 103 :6

7 Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake.


Zaburi 103 :7

8 Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

Zaburi 103 :8

11 Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.


Zaburi 103 :11

12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.


Zaburi 103 :12

13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.


Zaburi 103 :13


⏹ Anza mfungo wako wa maombi na moyo wenye matarajio ya kupokea kitu .Imani ni kitu cha msingi sana .

📖 6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


Waebrania 11 :6


⏹ Usiupe nafasi  upinzani wa kiroho .Shetani kunawakati huleta upinzani kati ya mwili na roho .


📖 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.


Wagalatia 5 :16

17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

Wagalatia 5 :17


4⃣ JIANDAE KIMWILI

🖊 Kufunga kunahitaji maandalizi ya mwili

🖊 Usikatize mfungo wa maombi

🖊 Andaa mwili wako .

🖊 Pata mda mzuri wa kupumzika


5⃣ PANGILIA RATIBA YAKO YA MAOMBI VIZURI

🖊 Kwa manufaa makubwa ya kiroho tafta muda wa kutosha wa kuzungumza na Mungu .Sikiliza uongozi wake .


🔰 ASUBUHI

⏹ Anza siku yako kwa kumsifu na kumwabudu Mungu

⏹ Soma na kutafakari neno la Mungu

⏹ Mkaribishe Roho Mtakatifu atende kazi na wewe

📖 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

Wafilipi 2 :13


⏹ Mkaribishe au mwambie Mungu akutumie katika nyanja mbalimbali kama vile namna ya kuleta matokeo mazuri kwenye familia , kanisa , n.k

⏹ Omba akupe maono ya maisha yako na akutie nguvu uweze kutembea katika mapenzi yake.


🔰 MCHANA

⏹Rudia kuomba na kusoma neno la Mungu

⏹ Fanya maombi ya kutembea kwa mwendo mfupi .


🔰 JIONI


⏹ Tafta mda wa kuutafta uso wa Mungu.

⏹ Kama kuna watu wamefunga pamoja kutana nao muombe pamoja .

⏹ Epuka vitu vitakavyokufanya uwe mbali na Mungu .


⏹ Kama umeoa au umeolewa anza na kumaliza mfungo wa maombi na mwenzi wako mkimsifu na kumshukuru Mungu kwa mda mfupi  .
Maombi ya mda mrefu na kusoma neno ni yanafanya kazi vizuri kwa mtu binafsi kusema na Mungu .Maombi haya hufanyika sana usiku au mchana mahali penye utulivu zaidi .


6⃣ USIANZE KULA CHAKULA KIGUMU MARA UNAPOHITIMISHA MFUNGO WA MAOMBI

🖊  Tumia vyakula vyepesi kama vile uji ,au chai .



7⃣ TEGEMEA KUONA MUNGU AKIJIBU ULICHOOMBA

🖊 Kama ukijinyenyekeza kwa Mungu ukatubu ,ukaomba na kuutafta uso wake .Pia ukiutafakari ukuu wake kupitia neno lake utapata ufahamu mkubwa wa mambo ya rohoni .


📖 21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

Yohana 14 :21


Mungu atakupa nguvu mpya zaidi na utaona matokeo mazuri kwako .




Mungu akubariki sana

KARIBU TENA


https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

  1. Mungu awabariki sana kwa mim nimebatikiwa sana natamani kujua Huduma zenu zinapatikana wapi mtu Wa mungu.

    JibuFuta
  2. Nimebarikiwa na mafundisho haya
    Mungu awabariki nitafanya hivi kama roho mtakatifu alivowaonyesha mtufundishe
    Ahsanteni

    JibuFuta
  3. Hongera na barikiwa kwa SoMo zuri ,,nimejifunza Sana kupitia SoMo lako Mungu akukumbuke popote ulipo,,Yeremia 1:8

    JibuFuta
  4. Nimebarikiwa na kufurahishwa na nalala hii...!!
    Mbarikiwe SANA!!

    JibuFuta
  5. Asanteni sana kwa muongozo mzuri . Mungu awabariki

    JibuFuta
  6. Aminaaaa,, ubarikiwe saanaa nmebalikiwa na Maneno hayaaa,,

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA