FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

                                         SOMO: FAIDA KUJAA ROHO MTAKATIFU 



                                                MNENAJI: MWLM C. MWAKASEGE 

                                                                   DAY 01                                                                  29/09/2016


Ni neema ya pekee sana kupata kibali kuwa hapa mkoa wa NJOMBE Mstari mkuu ni kutoka Effeso 5:18;” Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”


Lengo kuu la somo hili ni kujazwa Roho mtakatifu Na hapa tuta angalia mambo makuu matatu;

●Faida za kujazwa Roho mtakatifu

●kiu ya kujazwa Roho mtakatifu

 ●Wajazwe Roho mtakatifu Faida za kujaa Roho mtakatifu Petro analiandia kanisa lililoko effeso kwamba   wasilewe kwa mvinyo ...maana yake ni watu ambao walikuwa wapo kanisani lakini walikuwa wanalewa. Bali anawaasa wajazwe Roho mtakatifu Biblia inatofautisha kati ya Roho mtakatifu na Nguvu ya Roho mtakatifu kama ifuatavyo;

 Matendo 1:8;” Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika yerusalemu, na katika uyahudi wote, na samaria na hata mwisho wa nchi.”

Roho mtakatifu akija mahali kuna vitu vya msingi sana ambavyo anabeba na moja ya hivyo vitu vya msingi ni Nguvu za Mungu. Kwa hiyo Roho mtakatifu huja na nguvu.

 Pia soma Matendo 10:38 1koritho 2:4;” Sisi kama binadamu tunayo mapungufu mengi sana ambayo yana hitaji Roho mtakatifu ili tuwe kamili.”

Kuna nafasi ipo ambayo inahitaji Roho mtakatifu Faida mojawapo unapojazwa Roho mtakatifu ni kwamba utakuwa shahindi wa Mungu.

                                           FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 1


Shahidi wa Mungu ni mtu ambaye anaweza kwenda au kusimama mbele za watu ambao wanasema hakuna Mungu au wanalitukana jina la Mungu na kukidhihirisha kile cha ki Mungu.Naye shahidi lazima awe na mamlaka kimahakama kama shahidi wa Mungu Sio kila mtu aliyeokoka ni shahidi wa Mungu Kuna tofauti kati ya shahidi wa Mungu na mwanafunzi Mkipendana nyinyi kwa ninyi tayari msheshakuwa wanafunzi, tena mbinguni mtaenda lakini shahidi ni kitu kingine ...lazima ujazwe Nguvu za Mungu Ukiwa na Nguvu za Mungu utawasaidia watu walionewa na hata waliofungwa kihalali utawaweka huru. Sio tu kusema umeokoka hapo mbiguni utaenda na haina haja ya kuomba Nguvu za Mungu bali unaomba Nguvu za Roho mtakatifu ili uwasaidie watu waliofungwa Mfano: kuna tofauti kati ya kuwa na imani na Yesu na kuwa na imani ya nguvu za Yesu...ndio maana unakuta mtu anajiita ni mkristo ...ana mchungaji wake na kanisa lake lakini bado analo hirisi... hii ni kwa sababu hana imani na Nguvu za Mungu ...ndio maana anaenda kwa Waganga... Tuwe na imani na Mungu pia tuwe na Imani na Nguvu za Mungu.

Luke 4:18;” Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana ameninipaka mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona.” Unapozunguza mafuta maana yake ni upako Nguvu za Mungu zimezungumziwa katika staili tofauti tofauti Tangu siku ya Pentecost watu wote waliminwa Roho mtakatifu lakini Nguvu za Roho mtakatifu bado...unahitaji uwe na kiu ya kuitaka


JAMBO LA PILI

 kuna tofauti ya viwango vya ujazo ambavyo unatakiwa ujazwe na Roho katika maisha ya mtu Linganisha Yohana 7:37-39 na Yohana 4: 13-14. Yohana 7:37-39;” Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.”

 Na Yohana 4: 13-14;” Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.” hapa tunamuona Roho mtakatifu katiaka namna mbili, kama maji ya mto na maji ya chemchemi Roho ni yule yule lakini vipimo tofauti Zaburi 23:5; Ujazo aliokua nao daudi ni kikombe.”


                                FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 2


Haimaanishi daudi alijazwa sana hapana inategemeana na kipimo cha ujazo wa chombo alichoenda nacho...mfano angekuwa na ndoo au pipa ule upoko ungekuwa tofauti. Kuna tofaut ya upako wa ndoo na upako uliopo katiaka kikombe. Mfano: kama unataka kusafiri umbali mrefu utahitaji full tank ijae ili uweze kufika mahali unapotaka kwenda lasivyo itakua taabu. cheki hata ndege zinajaza mafuta hadi extra ...fikiri ndege inatoka Amerika ya kati kuja Tanzania inakaa hewani masaa 13 plus etra kwa ajili ya tahadhari...ni mafuta kiasi gani


JAMBO LA TATU


 kiu ya mtu ni kipimo cha uhitaji wa Roho katika eneo ambalo ana hitaji ajazwe Yohana 7:37-39 Si kila mtu anayetaka kujazwa Roho ana kiu.... mfano. ukisema ukaita watu waje wajazwe Roho watakuja wengi wana lakini sio kweli wote wana kiu Kama huna kiu ya kuwa shahidi wa Mungu hauna haja ya kujazwa Nguvu...kwa sababu ..mbiguni utaenda haina haja ya kuhitaji ambacho hauta kitumia...kuna watu wana Nguvu za Mungu lakini si mashahidi Hakuna mtu anayeweza kusome udactari miaka saba halafu hana kiu ya kutibu watu.... itakua haina maana.


 Linganisha Effeso 3:20 na Yohana 3:34 Effeso 3:20;” Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu” Yohana 3:34;” Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.” Hatutoi Roho kwa kipimo lakini tunampokea huyo Roho kwa kipimo Mfano....kama Roho mtakatifu amekuja ndani yako 100% na wewe ukachukua 50% na ukawa unatumia 10% maana yake kuonekana kwa Mungu katika maisha yako ni 10% na sio 50% tena ....na hizo 40% maana yake zinapotea Bure Upako uliopo ndani yako ambao ni extra hauna faida kwako, hauna faida kwa Mungu pia. Tunapewa vipawa na Mungu hii inatokana na Kiu ya uhitaji wa vipawa ndani yetu. Tulimalizia kwa shuhuda za Dar es salaam, Tanga na Shinyanga... Tukafanya maombi ya kupokea Nguvu za Roho mtakatifu...watu wengi sana walipokea.
                                                         


 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 3
                                            SOMO: FAIDA KUJAA ROHO MTAKATIFU



                                                                           DAY 02                                                                       30/09/2016



 Tulianza na umuhimu wa kuwaambia watu wote wanaotuzunguka kusikiza habari ya Neno la Mungu.Ukisoma habari za lazaro na yule tajiri.... hii ilikua ni picha halisi na wala si mfano ....ni picha halisi juu ya mambo yanayotokea kule kuzimu.... yule tajiri anaomba angalau tone la maji ili kuondoa kiu .... haya hayakua maji ya kawaida bali ni maji ya uzima....maana yake anamwambia ibrahim amwambie lazaro amletee wokovu ...lakini anambiwa umesha chelewa matengezo ni duniani.... Ni hatari sana kwenda kuzimu.... duniani, mbinguni, na kuzimu kote wanasema tusiende kuzimu maana ni hatari sana Tajiri analalamika pia jambo lingine......kwamba atumwe mtu kutoka kuzimu ili aende awape habari ndugu zake watano waliopo duniani ili waokoke lakini nafasi hiyo haipo ....anaona labda akie.da mtu ambaye ameonja ya huko kuzimu wakawahubiri labda wangesikia (maana nyingine ya tajiri juu ya ombi lake).....lakini anaambiwa wasipowasikiliza hao waliopo duniani basi. Hakikisha unamjulisha rafiki yako, ndugu, jamaa....wa dini , dhehebu lolote asikilize na kulisoma Neno la Mungu....ipo siku atakushika mkono .....na ukimuuliza nini atakwambia ni lile Neno ulilo niambia.... Yesu hakuja duniani kwa ajili ya wakristo bali kwa kila aamniye....yaani Dunia nzima.....kwa maani hii Mungu aliupenda ulimwengu.....sio wakristo bali ulimwengu wote. Jana tuliangalia faida za kujazwa Roho...


 Nguvu za Mungu hukusaidia kuwa shahidi wa Mungu Matendo 1:8 Utawasaidia watu walio onewa. Matendo 10:38 Itakusaidi kupata Nguvu za kuhubiri 1 koritho 2:4 Tuendelee na somo Letu Effeso 5:18 FAIDA YA NNE ILI UWEZE KUMALIZIA VIZURI KAZI ULIYOANZA KUIFANYA KWA MSAADA WA MUNGU Msomaji wa Biblia anafahamu umuhimu wa kumaliza vizuri Yesu anasema yeye ni Alfa na Omega maana yake anajua mwisho....
                                                         

  FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 4



Paulo anasema nimevipiga vizur vita ....imani nimeilinda na pia anauona mwisho...kazi ameimaliza... Haijalishi ulianza na mbio kiasi gani lakini inategemea umemalizaje mbio....haijalishi ulianzaje bali unamalizaje... Kocha wa timu haijalishi alishinda mechi ngapi....bali atamalizaje legue...akimaliza vibaya anafukuzwa...Hakikisha katika maisha yako .....safari ulio ianza lazima uimalize vizuri Upo upako katika Nguvu za Mungu utakao kusaidia umalize vizuri Luke 22 :41-44;”Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.” Kwa mara ya Kwanza tunamwona Yesu akiomba asifuate mapenzi ya Baba. Wakati ananza kazi lengo lake lilikua kuyafanya mapenzi Mungu...sasa hapa nini kinampata Yesu anaomba asiyafanye Mapenzi ya Baba yake. Yesu anasema sifanyi lolote isipokuwa lile alilonituma lakini hapa mwisho tunaona Yesu anakata tamaa...shida ni nini hapa? Yesu anapita mahali Pangumu sana ....anawambia wanafunzi wake angalau wamsaidie kuomba angalauhata lisaa limoja lakini ....wanafunzi wake wanalala.... Katika mistari hii Yesu anajaribu kusema kwaa maana nyingine....hakuna njia nyingine kuwasaidia hawa watu..isipokuwa njia ya Msalaba? Si kila anayepokea Nguvu za Mungu hubadilisha msimamo wake....kama usipopata upako wa kukusaidia mwishoni... si kila Nguvu inaweza kubadilisha sehemu katika maisha yako.....ndio maana unahitaji upako wa kumaliza vizuri Mzingo wa Yesu ilikua ni kuwa Adamu wa pili.....lakini anafika mwisha anakata tamaa.... Yesu aliomba mpaka Jasho liliisha hadi Damu inatoka kichwani mwake .....ili tu apate Nguvu...... Pamoja na kuwa Yesu ni Yesu na kuwa na Nguvu za Mungu na alikuwa na Roho mtakatifu lakini inafika mahali anakata tamaa Luke 8:43-48; Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara. Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.”
                                                         

 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 5


Ukitiza hii mistari tuna mwona huyu binti amabaye alitumia gharama nyingi sana ili kupona ugonjwa wake lakini hakupona.... ndipo alipogusa pindo la Yesu hapo hapo damu ikakauka ....na hapo Yesu anagundua Nguvu zimepungua ......maana yake Yesu anahitaji kuongezewa Nguvu maana. Yesu alimwambia yule dada mameno mawili ya msingi sana ....



●imani tako imekuponya

●Enenenda na amani kwa amani... Maana yake asingejieleza angeweza kupona lakini asingekuwa na amani....ndio maana ni lazima kumaliza vizur...watu wengi sana wanaishia hewani wanashindwa kumaliza..... Galatia 5:16-17;”Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili., Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.” Tunapaswa kuomba angalau hata lisaa limoja ili kuweza kuushinda mwili....ukiomba lisaa utaona kitu cha tofauti sana ndani yako....ndio maana Yesu ana waasa wanafunzi waombe angalau lisaa limoja ....sio kila baada ya dakika tano.. tena kumi ukijumlisha upate lisaa apana ni lisaa limoja hadi litimie utapata changes katika maisha yako ...unaweza kuushinda mwili. Ukiomba angalau lisaa itakusaidia kujazwa Nguvu za Mungu ambazo zitakusaidia kufika Mwisho... Ndio maana Mungu hakuambii inatosha kuomba bali Anakuongezea Nguvu ili uendelee kuomba zaidi Marko 8:22-26;” Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie.” Kwanini Yesu anamgusa huyu kipofu mara ya pili? maana dozi ya kwanza ilikua haitoshi ndio maana mara ya kwanza kipofu anaona watu kama miti... Yesu kama Mwanadamu anatufundisha kutembea na nguvu za Mungu...ili kumaliza salama Faida mojawapo kubwa ya kujazwa Nguvu za Mungu ni kukusaidia kumaliza vizuri kazi ulioianza. Tuangalie mfano wa pili kwa Elisha 2wafalme 2:9;”Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.” Kwa nini elisha anaomba upako mara mbili...? Elia hakumaliza kazi yake....Elia alipewa kazi ya kuzirudisha zile kabila kumi zilizoasi ili wamrudie Mungu na pia ammalize Yezebeli
                                                         


 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 6



 Inafika mahali Elia anaomba Mungu amuue kwa maana alikata tamaa....na kabla ya hapo tunamwona Elia anawaua wale manabii wa baali , pia alishusha moto unalamba zile sadaka ....lakini hapa mwisho anakosa Nguvu kabisa anakata tamaa.... Methali 24:10 Ukizimia siku ya taabu Nguvu zako ni chache ukikata tamaa katikati ya taabu ujue kumaliza kwako ni vigumu sana, Elia anapungukiwa na nguvu katikati ya taabu.....na Mungu anamwondoa duniani kwa gari la moto .... Ijapokuwa mbiguni anaenda lakini hakumaliza kazi aliyoipewa..... Alitakiwa asife kabla kabla ya kuzimaliza Nguvu za Yezebeli na kuzirudisha zile kabila 10 zilizoasi Elisha alipata double ili amalize kazi ya Elia pamoja na kazi yake mwenyewe alioijia hapa duniani... Saa ingine kwenye office yako au kazi yako au kwa wachungaji inabidi uombe Nguvu ya ziada ili kufanya kazi pamoja na Yule alieondoka lasivyo itakua vigumu sana na unaweza usimalize vizuri..... Saa nyingine katika huduma tunapozunguka nchi nzima ili kuifanya kazi ya Mungu tunapata shida sana (unachoka mwili)....lakini bado unahitaji kusonga mbele zaidi na watu wana kiu ya kukusikiliza na wewe hauna nguvu , hapo ni lazima uende kwa Yesu ili akutie nguvu mwambie nimechoka ,mwambie nisaidie hapa .....Alitoa ushuhuda wa Mwanza kwamba , semina imefika siku ya tatu.....imebaki kama nusu saa huduma ianze lakini hana nguvu na hana hata neno la kuzungumza na hata notes hajaandaa....ilikua si rahisi.....lakini akamwambia Rafiki yake Yesu nipe Nguvu.......alipata Nguvu ya ajabu akaenda kulihuburi Neno la Mungu kwa Nguvu kama mtu aliyejiandaa kwa miaka mitano.......Usijifanye uko ok wakati hauko ok.....Mweleze Yesu....Huwezi kushinda vita kama unaeshindana na ana Nguvu zaidi yako... Baada ya hapo tulifanya maombi ya kupokea Nguvu ya Roho mtakatifu ili...tuweze kumaliza vizuri kazi tulio ianza kwa msaada wa Mungu....na watu wengi walipokea... Hallelujah.....Hallelujah.               
                                             FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 7


                                                SOMO: FAIDA KUJAA ROHO MTAKATIFU 

                                                                          DAY 03                                                                       01/09/2016




[Mstari mkuu ni Effeso 5:18;” Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi bali ; mjazwe Roho”. Tulianza kwa wimbo wa maombi juu ya mkoa wa Njombe...ulio imbwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Mh. Rehema Nchimbi...uliosema Tufanye nini Njombe tutembee kwenye maji kama petro... Tufanye nini Njombe tupite kwenye Bahari kama Musu.... Tufanye nini Njombe Mungu ashuke kwenye moto kama ilivyotokea kwa Elia Tukafanya maombi juu ya mkoa wa Njombe ambao ni Lango la mikoa ya kusini....na hakika tulimwona Mungu akifanya katika mkoa wa Njombe..... Tunaendelea na somo letu juu ya faida za kujazwa Roho mtakatifu. Lengo kuu ni kuongeza ufahamu juu faida za kujazwa Roho mtakatifu ili ukizifahamu hizo faida uwe na kiu ya kujazwa. Tuliangalia faida nne za kujazwa Roho mtakatifu ambazo ni

�kuwa shahidi...matendo 1:8

�kuponya walionewa na ibilisi ....matendo 10:38

 �Imani yetu iwe katika nguvu za Mungu.......1koritho 2:4

�Ili uweze kumaliza vizuri kazi uliyoianza kwa msaada Mungu.......luke 22:41-44 Msisitizo ukiwa ni mstari 43.....malaika akamtia nguvu ili amalize kazi aliyoianza.

FAIDA YA TANO ILI UWE NA MOTO WA MUNGU NDANI YAKO KAMA MUNGU ANAVYOTAKA UWE NAO


Hii ni faida muhimu sana ambayo inaweza kuwa mpya kwa watu wengi. Matendo 2:1-4; “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.” Mathayo 3:11:” Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichua viatu vyake yeye atawabatiza kwa Roho mtakatifu na kwa moto.”
                                                           

FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 8
Ufunuo 4:5;”Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo.Na taa saba za moto zikiwaka mbele ya kiti cha enzi , ndizo Roho saba za Mungu.” Tuangalie kwa mtirieiko ufuatao. 1. Kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila moja wao na kujazwa Roho kila moja wao......msistizo ni kwamba kila moja na Moto wake....Mungu anataka kila Mtu na wake.... 2. Kuna uhusiano wa moto huo na kujaa Roho mtakatifu....maana yake  palipo na Roho mtakatifu panatakiwa pawe na moto 3. Moto ni ishara toka kwa Mungu juu ya kile ambacho Mungu amemtuma Roho mtakatifu kufanya ndani ya mtu na katika maisha yake. 4. Kuna umuhimu wa kutambua moto unao waka ndani yako ni kwa ajili ya nini?... Pamoja na kuwa Roho mtakatifu ni moja lakini majukumu yamegawanyika..

�Zile taa saba katika kiti cha enzi maana yake ni Roho saba ....na Roho saba maana yake ni majukumu saba..mambo saba au macho saba ya Mungu

 � Namba saba kibiblia maana yake ni ukamilifu wa Mungu..

�Roho wa taa moja akija ni tofauti na yule mwingine ....anasema unajuaje? Isaya 11:1-2;” Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;” Zile Roho saba zinaoneshwa hapa Kuna Roho ya uchaji

 ●Roho ya maarifa

 ●Roho ya ushauri

 ●Roho ya uweza

 ●Roho ya Bwana

●Roho ya ufahamu

 ●Roho ya hekima Sasa ni Muhimu sna kuitambua moto au Roho inayowaka ndani yako.... Hizi habari za moto zimezungumzwa vibaya kwenye bibilia sijui ni kwanni hawa watu wanaofundisha wamesema hivyo juu Roho wa moto....
                                                         

 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 9

�Ile kwamba magari yanaanguka haiondoi sisi kupanda magari.....ile kwamba wengine wanachanganyikiwa wanaposoma bibilia haiondoi sisi kusoma biblia.....ile kwamba wachugaji, wakristo wengi wanatenda dhambi haiondoi sisi kuutafuta utukufu wa Mungu

�Tambua kwamba Mungu anataka uwe na moto ndani yako kwa sababu moto ni ishara... Kabla ya kuangalia hizo ishara za moto ...tutizame namna ya kusoma Angano la kale kwa sababu watu wengi sana wanashidwa kulisoma kwa sababu kuna masharti... "......Siku moja nilimuuliza marehem mzee Moses kolola juu ya maneno aliyokuwa anayazungumza juu ya jiwe la haki, nyota kuanguka yameandikwa kwenye biblia .... akaniambia nakupa assignment...na mimi nakupa assignment...tafuta kwenye biblia ...yapo"

�Agano jipya ndilo angano bora kuliko maagano yote ....Soma  Agano la kale kwa Sura ya agano jipya.... Paulo anaandika watakapo mgeukia ndipo naye atawafunulia ....kama haujaokoka ni vigumu sana kuelewa mambo ambayo yapo kwenye maandiko kwa sababu ni kazi ya Roho mtakatifu kukujulisha na kukufundisha..... yale yaliyo fanyika agano la kale ni kivuli cha Agano jipya....kwa wale ambao walipiga picha zamani kidogo....agano la kale ni Zile Negative na Agano jipya ni picha halisi Moto wa Mungu hausikiki sana katika agano jipya na unasikaka sana katiaka agano la kale kwa sababu Yesu yupo kwa sura nyingine ndani ya Mwandamu Angalia sasa hizo ishara za moto.... 1.Ni ishara ya utambulisha juu ya umiliki wa Mungu juu ya eneo husika ambapo moto unawaka Mambo ya walawi 10:1-3;” Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya BWANA, ambao yeye hakuwaagiza.Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, nao ukawala, nao wakafa mbele za BWANA. Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo BWANA alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya.” mahali amabapo Mungu ameamua kujitambulisha ishara mojawapo ni moto....waulize wachawi...ndio maana katika ulimwengu wa Roho hakuna  moto wa kigeni...shetani alinyamaza kimya kipindi cha elia wakati anawachinja wale manabii wa baali kwa sababu anajua nini kingamkuta angeshusha moto wa kigeni....moto Moto wa Mungu ulilamba kila kitu....maana yake Mungu anajitambulisha kuwa eneo lile ni lake na elia ni mtumishi wake.... Hata ule moto kwa wanafunzi  Mungu alikua anajitambulisha kwao..... usipokee moto wa kigeni...maana yake usikubali dhambi hata siku moja kwa sababu...utakufa ...maana yake utakufa Kiroho(utapoa).
JAMBO LA PILI 2. Ni ishara  ya Mungu kuwapokea watu wake katika utumishi kama sadaka kwenye madhabahu yake.
                                                         


 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 10


Waebrania 1:7 Walawi 6: 8-9, 12-13 Waebrania 1:7;”Na kwa habari za malaika asema,Afanyaye malaika wake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa miali ya moto. BWANA akanena na Musa na kumwambia, Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hata asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike”.

 Walawi 6: 8-9, 12-13;” Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake.Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike.” Mungu alipokuwa anashusha Roho na Moto ishara mojawapo ni kuwapokea  watu wake kama watumishi....Yesu alizungumza habari ya kutumwa na kututuma sisi kama sadaka .... kama unampenda Mungu utatoa uhai wake kwa Mungu...maana yake wewe ni sadaka  madhabahuni mwa Mungu... chochote ambacho Mungu anataka kukitumia hukiweka madhabahuni kama sadaka ... angalia sadaka ya ibrahim ( isaka ) kwa Mungu.... Angalia pia lile ombi la Elia ...kwamaba na ijulikane  wewe ni Mungu nami ni mtumishi wako...ndio maana Mungu alishuka kwa moto na hii ni kwa sababu ya ebrania 1:7


�kipindi cha angano la kale ni tofauti na kipindi kingine kwz sababu hatuoni Mungu akipita mtaani na moto wake akiwauwa watoto.. watu wasio na hatia ...hii ni kwa sababu Mungu anajifunua kwa moto wake kwa mtu binafsi aliyetayar kupokea...... moto wa Mungu uko ndani yako

 � Na katika ulimwengu wa Roho wewe umetiwa muhuri wa arabuni na moto wa Mungu upo ndani yako.... wale watumishi wakati wa huduma kule tabora mchawi moja alikuwa akishuhudia saivi ni mchugaji anasema ...walikuwa wanaonekana kama ...miali ya moto...wale wachawi wakashindwa kumsaidia mwenzao. JAMBO LA TATU 3. Ni ishara ya ulinzi na silaha ya Mungu dhidi ya Adui za watu wake. Zakaria 2:5:” Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake”. Changamoto kubwa ni kuhakikisha moto wa Mungu hauzimiki..duniani , hauzimiki kanisani , haijalishi mchungaji wako yupo au hayupo moto usizimike. Utajuaje ya kwamba moto umezimika 1: kutokuona kama kumtumikia Mungu  ni kujitoa sadaka...yaani unaona kuna faida gani ya kumtumikia Mungu.....

� unapomtumika Mungu usitafute faida yako , tafuta faida yake na kati ya faida yake faida yako ipo pia......unakuwa shareholder.
                                                            FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 11
Mfano ni kwenye kampuni....unapoifanyia kampuni kazi na unapozalisha ikipata faida  automatically na wewe na wewe unapata faida ...faida ikipungua wanapunguza na  wafanya kazi pia

�Mungu anaoutaratibu  wa kuwatunza watu wake wanaomtumikia ....yeye anajua namna ya kukutunza , si dhalimu. 2: Ni kutaka kuacha kazi ya Mungu na husikii moto ukiwaka kukuzuia  usiache.... Angalia ile Jeremiah 20.. Analamika kuacha kazi ya Mungu lakini mwisho moto ukawaka ndani kumzuia

 �Ukiona unataka  kuacha kumtumikia Mungu  na hakuna moto unaokuzuia maana yake umepoa ...ndio maana moto upo ili ukupe starter..unapotaka kupoa. 3: Moto wa kigeni unaweza ukaja kwako na uziweze kupata upinzani....Neno la Mungu  ni moto ulao kwa hiyo lolote liliso la ki Mungu likija kwako lazima liondoke...Moto wa kigeni ukija ndani utakutana na moto wa Mungu ...
Baada ya hapo tulifanya maombi ya kupokea moto wa Mungu na hakika nilipoke...
                                               


 SOMO: FAIDA KUJAA ROHO MTAKATIFU                                                                            DAY 04
                                                            FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 12


                                                                       02/09/2016


 Mstari unatuongoza ni Effeso 5:18 Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi bali mjazwe Roho Mungu ametupa huduma hii ya kufundisha kwa saa au wakati halisi.....unapokutana mwalimu na akakufundisha ujue kuna mtihani upo mbele yako utaufanya tena utaufanya ukiwa peke yako...."


FAIDA YA TATU ILI UJUE NAMNA YA KUJIANDAA KUMLAKI YESU ATAKAPOKUJA KULINYAKUA KANISA

 Mathayo 25 :1-13 Ni ile habari ya wana wali 10 walio kuwa wakimsubiri bwana harusi. JAMBO LA KWANZA

�wanawali watano wapumbavu walizuiwa kuingia harusini kwa sababu hawakujua namna ya kujiandaa kumlaki bwana harusi... maana yake nini...walikuwa na maandalizi ya kula karamu hawakuwa na maandalizi ya kumlaki bwana harusi Hawa kujua tukio la kumlaki bwana harusi ni muhimu sana kuliko tukio la karamu .....walijiandaa zaidi kula karamu kuliko kujiandaa kumlaki.


JAMBO LA PILI


�Tukio la kumlaki bwana harusi ndio tukio la kunyakuliwa kwa kanisa linalokuja kabla ya harusi ya Mwana kondoo. Ufunuo 19:7-9 1thethalonike 4:15-18 Mathayo 24:40-41. Ufunuo 19:7-9;”Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.” 1thethalonike 4:15-18;”Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika
                                                         

  FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 13


Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” Mathayo 24:40-41.;”Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.” Kama unasoma vizuri biblia juu ya ujio wa Yesu ...kuna vitu vya msingi wana unatakiwa ujue... ujio wa Yesu ni kipindi muhimu sana kuliko vipindi vyote...kristo ni sura ya Mungu na vyote viliumbwa katika yeye na pasipo yeye hakikuumbwa kitu ...Mwanadamu alipomkorofisha Mungu katika dhambi ndipo Yesu alipoondoka kwa mwanadamu ...maana yake ni nini... Yesu akaondoka na ufalme wake kwa Mwanadamu Yesu akaondoka katika maisha ya watu. Hii ni kwa sababu dhambi ni uasi. Ukisoma agano la kale Yesu alivyokuwa akijifunua si kama tunavyomfaham sasa katika agano jipya lakini alikuwepo...kwa hiyo tangu dhambi ilipotendeka  Mungu amekuwa akijifunua kwa wanadamu katika majina tofautitofauti au maagano tofauti.. Mfano wakati wa kipindi cha sodoma na gomora Yesu alijifunua kwa ibrahi..... Kulikuwa na malaika wawili na Bwana  na Bwana alibaki kuongea na ibrahim...na yule Bwana alikuwa ni Yesu......maandiko yanasema alipomaliza kuongea na ibrahim Bwana akaondoka ! Hata  habari za kina daniel yule alikuwa kwenye tanuru la moto...alikuwa ni Yesu mwenyewe.... Wakati wa agano la kale Yesu kuna majina Mungu alijifunua kwa ibrahim, Musa , elia.. lakini wakati wa  jipyajipyaianajifunuajina la Yesu..... lakini jina la Yesu ndilo jina kuu kuliko majina yote Yesu anasema naenda kuandaa makao kuja kuwa chukua... Kuna namna mbili ambazo Yesu atakuja Moja.....kila jicho litamwona.. Ya pili.....atakuja kama mwivi... Maana yake nini. 1..tukio la kuja kuhukumu....malaika nawaambia 2...tukio la kuja kulichukua kanisa.....hapa Yesu anawaambia wanafunzi wake



 �jambo lililo karibu sana ni la Yesu kuja kulichukua kanisa ( watu ambao wamemkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao )
Hili ni tukio ambalo lipo mbele yetu kwa karibu sana ....
                                                            FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 14
Kumbuka jambo hili..... hatuwezi kufika kwenye karamu kabla hatuja nyakuliwa kwanza Usianze kusherehekea sherehe ya mwanakondoo kabla ya kunyakuliwa.. Kabla ya sherehe kuna maandalizi. Ile 1thethalonike 4:13-18 Tunaona mambo saba yatatokea kwa dakika moja tu....

 �Yesu atakapokuja kulichukua kanisa haji duniani tutamlaki mawinguni....lakini atakapokuja kuhukumu atakuja duniani....ni muhimu sana kujua hizi tofauti..


 JAMBO LA TATU

 �Kuna uhusiano wa jambo la kukosa mafuta ya taa na kule kutokuwa na namna ya kujiandaa kumlaki bwana harusi. Mathayo 25:5-13;”Wale wana wali wote walikuwa na taa wote wanenda kumlaki bwana harusi ...watano...wapumbavu...maana yake...wanaelewa lakini hawataki kufanya hii ndio maana ya mpumbavu....ila mjinga ....haelewi au hajui kitu” Mpumbavu hupata adhabu lakini ...mjinga hapati adhabu... Ukisoma ule mstari wa nane...waliziwashataa lakini zikazika...tatizo ni nini  ...mafuta! Tatizo sio kwenda kumlaki tatizo ni kujiandaa Namna neno mafuta lilivyo simama ni Nguvu na upako wa Roho mtakatifu ambao kazi yake kubwa ni  kukuandaa namna ya kumlaki Bwana ...kazi ya Roho mtakatifu si kuhubiri na kuwa shahidi bali namna  kukuandaa kwenda kwenye harusi.. Haitoshi kwenda kwenye harusi bila kuingia kwenye harusi.....unaweza kwenda kwenye harusi ukaishia njiani ....maana nyingine unaweza kuingia kwenye harusi na usikae kwenye harusi.. Wale wanawali walikuwa na wrong timing.... Tatizo la yule mtu moja kwenye harusi ambaye hakuwa na vazi la harusi......

 �Nguo nyeupe ni vazi la wokovu haulipata baada ya kufa unalipata unalinunua kwa damu ya Yesu baada ya kuokoka..... Sio suala la kusema unakadi ya harusi....no una vazi? Swala la kwenda mbinguni ni swawa na swala la kusafiri...sio kila mwenye tiketi anasafiri......atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka....kuokoka kwa mwanzo ni kununua tiketi....na si kila anayenunua tiketi anaenda wengine hutoa udhuru.....wengine wanaachwa na basi kwa kuchelewa....si kila anayesema nimeokoka ataenda mbinguni...unapookoka hakikisha kwamba hauachwi...ile kwamba umepanda ndege haimaanishi kwamba utaenda.....biblia inasema mkuu wa ulimwengu anakuja lakini hana kitu kwako....Hakikisha hakutoi kwenye ndege.


 JAMBO LA NNE
                                                         



 FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU 15



� walioingia na kula karamu ya bwana harusi ni wale walio kuwa tayari.... je wewe una utayari kiasi gani kumlaki  Bwana ajapo.... Wale wanawali watano walikuwa kwenye kundi la wakristo hawakujiandaa....waliporudi wakakuta mlango umefungwa.....Muda wako wa kukaa kanisani hauna faida kama utakosa kukaa na Bwana milele.... Kesheni mkiomba.......Muombe na mkae mkao wa utayari... Ukisoma ile mathayo 24 yote....... Utaona watishi wengine hawatenda mbiguni si kwa sababu wametenda dhambi lakini ni kwa sababu hawakujali muda wa kumtumikia Mungu( their out of time )...si w atmishi tu hata wewe unayetoa sadaka unachelewesha  N eno la Mungu kufika mahali husika kwa wakati......watahubirije wasipopelekwa? Mtu anaandaliwa kumpokea Yesu kabla ya kufa .....haukuitwa tu kuwaombea wagojwa bali kuwafungulia geti waende mbinguni....usiogope kuwaombea..ni changamoto nzito lakini unahitaji kuwaandaa watu ili wairidhi nchi......

�hata kama unatoa pepo.....hakukupi tiketi ya kwenda mbinguni...bali ni kuwa na mafuta ya Roho mtakatifu....yatakayo kupa saa mwafaka,kujua mafuta yako ya taa yako kiasi gani. Pia mafuta yatakusaidia kukuonesha dalili za kuja kwa Yesu....

 �Endelelea kucheki je? Parapanda ikilia saiv nitaenda mbinguni

 �Lazima watu wakae mkao unaonesha kwamba mbinguni wataenda....unatakiwa ukae mkao wa kusafiri Jitahidi kila wakati kujihoji kama ukosawa kwenda mbinguni....ikiwa na tumaini jipya.... �Huwezi fika mbinguni kama haujajianda au haujaandaliwa.......hivyo kama kuna ndugu zako wa karibu kaa nao uwaandae juu ya kurudi kwa Yesu....

�Mungu hana upendeleleo wala si dhalimu ukikaa mkao wa kusikia hakika utasikia..

�Mungu hawezi kukushtukiza asikwambie yeye si dhalimu lazima akuambie juu ya kuondoka kwako.... Baada ya hapo tulifanya maombi ya kuwa tayari ........ Mbarikiwe na Bwana Yesu.......Wokovu sio dini ni tumaini jipya kwa Yesu kristo..



                                                            FAIDA ZA KUJAZWA ROHO

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*