USTAWI (PROSPERITY) Mch & Mwl Peter Francis Masanja 0744056901 Mwanzo 26:13 13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Kibiblia maana yake ni Rehobothi Mwanzo 26:22 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake REHOBOTHI, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. MAANA YA NENO: REHOBOTHI Neno hili limebeba maana mbili 1. Kufanyiwa au kuwekwa katika nafasi na BWANA. Zaburi 118:5 Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. Nafasi ni nini? a). Nafasi ni eneo la umiliki wa kitu. b). Ni eneo la utenda kazi wa kitu au mtu. c). Ni eneo la makazi( Mahali pa kukaa). d). Ni eneo la utawala au mamlaka juu ya jambo Fulani au vitu. e). Nafasi ni kitu kilichobeba sifa zako( kama vile mke, mume, watoto,mahali pa kuabudia, biashara n.k) Usitawi wako upo katika uwezo wa k...