USTAWI (PROSPERITY)

Mch & Mwl Peter Francis Masanja

0744056901

Mwanzo 26:13

13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.

 

Kibiblia maana yake ni Rehobothi

Mwanzo 26:22

Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake REHOBOTHI, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.

 

MAANA YA NENO: REHOBOTHI

Neno hili  limebeba maana mbili

1.Kufanyiwa au kuwekwa katika  nafasi na BWANA.

Zaburi 118:5

Katika shida yangu nalimwita BWANA;

BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.

 

 

Nafasi ni nini?

a). Nafasi ni eneo la umiliki wa kitu.

b). Ni eneo la utenda kazi wa kitu au mtu.

c). Ni eneo la makazi( Mahali pa kukaa).

d). Ni eneo la utawala au mamlaka juu ya jambo Fulani au vitu.

e). Nafasi ni kitu kilichobeba sifa zako( kama vile mke, mume, watoto,mahali pa kuabudia, biashara n.k)

Usitawi wako upo katika uwezo wa kutendea kazi nafasi ambayo Mungu amekuweka uwajibike pamoja naye ili akufanikishe.

Isaka aliwekwa katika nafasi( eneo ) ambayo Mungu alikusudia kumfanikisha.Gerari ilikuwa ni nafasi yake na siyo huko Misri alikotaka kuelekea.

 

 

Mwanzo 26:1-6

1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.

2 BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.

3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.

4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.

5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.

6 Isaka akakaa katika Gerari.

 

Nafasi inaenda sambamba kabisa na Mungu ili akufanikishe. Mungu anazingatia sana kanuni hii ili akubariki anahitaji akuweke kwenye nafasi inayokufaa ambayo kwa hiyo  atapitishia baraka zake.

 

2. Kuzidi ( kuongezeka).

( The Principle of Multiplication and Addition)

Kuzidi  ni matekeo  ya kuitendea kazi nafasi uliyowekwa uimiliki au  uitumie kulingana na vipawa au vipaji ulivyopewa na Mungu.

Isaka alipowekwa Gerari aliitumia fursa hiyo kulima na kufuga kwa ubora zaidi.

 

Mwanzo 26:12- 14

12 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki.

13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.

14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng’ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

Unaposimama katika nafasi ambayo Mungu amekuitia kuitumikia, Mungu atakufanya kuwa mkuu au mtu maarufu katika hiyo nafasi.

Tunamwona Isaka anakuwa mkulima maarufu huko Gerari mwenye nguvu kuliko watu wa pale ugenini.

Hata Raisi wa nchi hiyo ya Gerari( Abimeleki) alimtambua kuwa ana nguvu kupita wao katika eneo la kiuchumi.Huyu mtu  alifikia kiwango cha juu sana maana alikuwa na pesa kuliko Abimeleki. Siri hii ya mafanikio ni kwa sababu aliisikia sauti ya Mungu na kumruhusu Mungu amwongoze.

 

Mwanzo 26:16

Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.

Mtu mwingine ni Ibrahim naye alistawi

Mwanzo 17:1

1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.

3Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,

4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,

5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.

6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*