MATENDO MEMA BILA KUOKOKA
*MATENDO MEMA BILA KUOKOKA(WOKOVU) YANA MAANA?*
*MATENDO MEMA YANAWEZA KUWA MBADALA WA WOKOVU BILA KUPITIA WOKOVU WA YESU MSALABANI?*
Mwl Raphael Mtui(0762 731869)
_Naomba sana usiache kusoma makala hii, na naomba uisome kwa unyenyekevu kabisa_.
Tuanze kwanza kwa kusema ukweli huu:
HAKUNA MWANADAMU AMBAYE HAKUWAHI KUINGIA KWENYE KITABU CHA DHAMBI NA HUKUMU!
HAKUNA MTU HATA MMOJA AMBAYE ETI HAJAWAHI KUHITAJI MSAMAHA WA MUNGU KISA ANA MATENDO MEMA SANA!!
HAKUNA MTU AMBAYE ETI HAHITAJI KUTUBU NA KUOKOKA, KISA AMEKUWA MTENDA MEMA SANA.
NI YESU PEKE YAKE HAJAWAHI KUHITAJI TOBA NA MSAMAHA WA MUNGU, MAANA YEYE HAKUWAHI KAMWE KUWA MDHAMBI.
SIFA HII YA KUTOHITAJI MSAMAHA WA MUNGU KUTOKANA NA UTAKATIFU WAKE, NDIO KIGEZO KILICHOPELEKEA YEYE KUFAA KUWA MWOKOZI WETU, NA DAMU YAKE KUPATA UHALALI WA KUTUFANYIA UPATANISHO KWENYE MADHABAHU YA MUNGU, MAANA HAIKUWA NA HATIA KABISA!
WATU WENGINE WOTE KABISA WAMEWAHI KUWA WADHAMBI, *HATA KABLA WAO HAWAJATENDA DHAMBI ZAO WENYEWE!*
(Isipokuwa kwa kesi ya watoto wadogo, wao huwa wanahesabiwa haki tu, hata kama wakikosea, tena wana ile hali ya dhambi/utu wa dhambi waliozaliwa nao, ila Mungu hawaweki hatiani maana bado hawajafikia uwezo wa kupambanua mema na mabaya ili waushughulikie huo utu wa kale).
KWA HIYO UJUE, HATA KAMA HUKUWAHI KUFANYA DHAMBI YOYOTE, WEWE UNA MATENDO MEMA SANA, *LAKINI DHAMBI YA WAZAZI WETU ADAMU ILITUWEKA WATU WOTE KATIKA HALI YA HUKUMU, HIVYO TUKAJIKUTA TUNAHITAJI MSAMAHA NA WOKOVU/MWOKOZI.*
Kumbuka sana, sikusema ili tuokoke na hiyo hali ya dhambi tuliyoirithi kutoka kwa kina Adamu, eti tungehitaji matendo mema!
Tunahitaji kwanza MSAMAHA, YAANI WOKOVU, ndio kuanzia hapo tuanze kutenda mema, na matendo hayo mema baada ya kupata TOBA/KUOKOKA yatakuwa na maana.
Naomba sana kwa unyenyekevu, usome Maandiko yafuatayo, ILI UONE JINSI KOSA LA ADAMU LILIVYOTUWEKA KATIKA *HALI YA DHAMBI, ADHABU, NA HUKUMU,* LAKINI PIA YANAONESHA JINSI YESU ALITUOKOA(SI MATENDO YETU MEMA YALIVYOTUOKOA).
Warumi 5:12-19
*Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti IKAWAFIKIA WATU WOTE KWA SABABU WOTE WAMEFANYA DHAMBI;*
*................*
*walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala HATA WAO WASIOFANYA DHAMBI IFANANAYO NA KOSA LA ADAMU aliye mfano wake yeye atakayekuja.*
*Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa KWA KUKOSA KWAKE YULE MMOJA WENGI WALIKUFA, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.*
*Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana HUKUMU ILIKUJA KWA NJIA YA MTU MMOJA IKALETA ADHABU; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.*
*Kwa maana ikiwa KWA KUKOSA MTU MMOJA MAUTI ILITAWALA KWA SABABU YA YULE MMOJA, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.*
*Basi tena, kama KWA KOSA MOJA WATU WOTE WALIHUKUMIWA ADHABU, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.*
*Kwa sababu kama kwa KUASI KWAKE MTU MMOJA WATU WENGI WALIINGIZWA KATIKA HALI YA WENYE DHAMBI, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.*
Maandiko hayo yanatuambia wazi kuwa, kosa la wazazi wetu Adamu na Eva lilitosha kutia watu wote hukumuni.
Kosa hilo lilitufanya tuwe KATIKA HALI YA DHAMBI/UTU WA DHAMBI, au UTU WA KALE, HATA KAMA HATUJATENDA DHAMBI ZETU WENYEWE.
Usichanganye, HATUKURITHI DHAMBI YA KULA TUNDA, BALI TULIRITHI HALI YA DHAMBI, AU BIBLIA HUUITA UTU WA DHAMBI, AU UTU WA KALE, AU UTUMWA WA DHAMBI, NA *HALI HII ILITOSHA KUTUHUKUMU BILA HATA KUHITAJIKA DHAMBI ZETU.*
Mwembe ni mwembe tu, hata kama hauna maembe.
Ili tutoke katika hali hiyo ya udhambi tuliyoirithi, tunahitajika kuzaliwa mara ya pili, yaani utu wetu wa kale usulibiwe na kuzikwa, ndio tufufuke na utu mpya, tuwe viumbe vipya.
Unatenda matendo mema wakati hujazaliwa mara ya pili/hujaokoka?
Yesu alisisitiza;
Yohana 3:3
*Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI, HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU.*
Kwa hiyo tunazaliwaje mara ya pili?
Kwa maneno mengine, *Tunausulibishaje utu wa kale ili tuzaliwe na utu mpya?*
KWA KUTUBU UKIMAANISHA KUACHA/KUTOTENDA DHAMBI.
Unapotubu, utu wako wa kale unapelekwa pale msalabani Yesu alikosulibiwa, na unauawa namna ile ile Yesu aliyouawa.
*Tunazikaje utu wa kale?*
Kwa KUBATIZWA, yaani KUZIKWA kwenye maji mwili mzima.
Unapozamishwa kwenye maji wakati wa tendo la ubatizo, maiti ya utu wa kale/mwili wa dhambi uliosulibiwa sekunde zile ulipotubu, unapelekwa moja kwa moja katika lile kaburi Yesu alimozikwa na kuachwa huko.
Soma haya Maandiko tafadhali:
Warumi 6:3-6
*Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?*
*Basi TULIZIKWA NAYE KWA NJIA YA UBATIZO katika mauti yake, kusudi KAMA KRISTO ALIVYOFUFUKA katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, VIVYO HIVYO NA SISI TUENENDE KATIKA UPYA WA UZIMA.*
*Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;*
*mkijua neno hili, ya kuwa UTU WETU WA KALE ULISULIBISHWA PAMOJA NAYE, ILI MWILI WA DHAMBI UBATILIKE, tusitumikie dhambi tena;*
Tena, utu wa kale/mwili wa dhambi unapozikwa, hata magonjwa, mapepo, vifungo vya dhambi na mauchafu mengine huweza kumwachia mtu anayebatizwa, maana utu wa kale hubeba furushi la utumwa wa dhambi, pamoja takataka zote zitokanazo na dhambi.
Unapotolewa kwenye maji, unatoka ukiwa na utu mpya, au upya wa uzima, yaani unakuwa kiumbe kipya kabisa kama vile hukuwahi kuwa mwanadamu aliyezaliwa kutoka kwa kina Adamu na Eva.
Unakuwa na sura ya Mungu kabisa ndani yako, unapewa hadhi ya kuitwa mtoto wa Mungu, mtakatifu, mwenyeji kabisa wa Mbinguni ambaye bado yupo duniani kwa kazi maalumu ya kuwahubiria wengine wokovu huu.
Huu ndio wokovu, ndio kuingia ndani ya Kristo na kuwa kiumbe kipya (2Kor 5:17).
MATENDO MEMA BILA WOKOVU HUU HAYANA MAANA KABISA!
MATENDO MEMA WAKATI NDANI KUNA UTU WA KALE, NI SAWA NA CHAKULA KIZURI KILICHOPIKWA VIZURI, LAKINI KIKAWEKWA KWENYE SAHANI YENYE MAVI! NACHO KITAITWA UCHAFU!
Haijalishi unajitahidi kukwepa dhambi namna gani, lakini kama hujamwamini Yesu KAMA MWOKOZI ukaokoka, basi ujue matendo yako hayatakusaidia wala hutahesabiwa haki.
Utahesabiwa haki kwa kumwamini Yesu na kumpokea awe Mwokozi wako.
Wagalatia 2:16
*hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.*
Matendo yetu mema hayataweza kutupa wokovu, na kama yangeweza, basi Yesu asingekuwa na haja ya kuja duniani kutuokoa, wala mpango wa Mungu wa wokovu usingekuwepo.
Tungepewa tu sheria na kuambiwa tuziishi, atakayezitii ataenda Mbinguni, asiyeweza kuzitii ni jehanum.
*Kila mwanadamu aliyezaliwa huku duniani, anahitaji wokovu, na lazima amwamini huyo anayeokoa, yaani huyo Mwokozi.*
Yesu ndiye Mwokozi mwenye uwezo wa kutuokoa kutoka kwenye utumwa wa dhambi, tuliourithi kutoka kwa baba zetu.
Wito wa kwanza kabisa, mara mtu anapopata akili na ufahamu wa kutosha kupambanua mema na mabaya, huwa anatakiwa amwamini Yesu kama Mwokozi ili aokoke.
Kila mwanadamu anapozaliwa, huwa anakuwa moja kwa moja katika hali ya dhambi, isipokuwa tulipokuwa bado watoto wadogo, Mungu alituhesabu kama watakatifu tu (1Kor 7:14b) kwa maana tulikuwa bado hatujui kupambanua mema na mabaya.
Mara tu unapokuwa na uwezo wa kujua mema na mabaya, UNAANZA KUDAIWA JAMBO MOJA KUU: *KUMWAMINI YESU NA KUTUBU.*
Katika Injili yote ya Bwana Yesu, pamoja na wale Mitume wa Kanisa la Kwanza, ujumbe wao wote ulikuwa ni kuiambia dunia imwamini Yesu, na impokee kama Mwokozi wa ulimwengu.
KUMPOKEA YESU MOYONI NI KUFANYAJE?
Kutubu toba ya ki-Biblia, na kubatizwa ki-Biblia.
Baada ya hapo, ndio matendo mema yaanze.
Kila walikoenda, ujumbe wao wa kwanza ulikuwa TUBUNI, NA MBATIZWE, NDIPO MUANZE KUISHI MAISHA YAPASAYO TOBA(YAANI MAISHA MATAKATIFU).
Mathayo 3:8
*Basi zaeni matunda yapasayo toba;*
Kama mtu asipomwamini Yesu, akatubu na kubatizwa, huyo amekwisha kuhukumiwa.
Yohana 3:8
*Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.*
Dhambi kuu ambayo Roho Mtakatifu ataihukumu dunia ni KUTOKUMWAMINI YESU.
Yohana 16:8-9
*Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.*
*Kwa habari ya dhambi, kwa sababu HAWANIAMINI MIMI;*
*_Tunajuaje umemwamini Yesu?_*
Pale unapokubali kutubu na kumkiri Yesu kuwa Bwana wako na Mwokozi wako, kisha ukabatizwa kwa kuzikwa kwenye maji ishara ya kuzika utu wako wa kale, na kisha kubatizwa kwa kuombewa ujazo wa Roho Mtakatifu.
MATENDO MEMA YANATAKIWA YAJENGWE JUU YA MSINGI HUO.
Lakini kama ukiamka tu siku moja asubuhi, ukaanza kutenda mema, ukaacha tabia zote mbaya, lakini hukutubu wala hukubatizwa, haijalishi unasema unamwamini Yesu, lakini kama imani hiyo haikuambatana na tendo la toba na kumkiri Yesu pamoja na kubatizwa, hiyo ni imani iliyokufa.
Si unajua imani bila matendo ya kuonesha unachoamini ni bure?
Matendo mema bila wokovu, hayawezi kumwokoa mtu, tena wala hayawezi kumhesabia mtu haki, ili afae kuingia Mbinguni.

Matendo mema ni ushuhuda kuwa tumeokoka.
*Matendo mema si kigezo cha kupata wokovu, bali matendo mema yanatakiwa yawe matokeo ya kupata wokovu.*
Wokovu haufuati matendo mema, bali matendo mema hufuata wokovu.
Ni kiburi cha hali ya juu sana kufikiri unaweza kutenda mema yakakuokoa bila kukubali kupitia mpango wa Mungu wa wokovu alioufanya katika Kristo kwa ajili yetu.
Ingekua hivyo kweli tungeringa!!
Lakini sasa hatuwezi kuringa, maana hatuwezi kujiokoa wenyewe kwa matendo yetu mema.
Tumeokolewa kwa neema tu wala si kwa matendo yetu mema, hivyo hatuwezi kujisifu.
Waefeso 2:8-9
*Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;*
*wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.*

Maoni
Chapisha Maoni