MAFANIKIO YA KIUCHUMI

MAFANIKIO YA KIUCHUMI
SOMO LA KWANZA

Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829

https://peterfrancismasanja.blogspot.com


Ni muhimu sana kujua kuwa juhudi za kutafuta kufanikiwa bila kupatana na Mungu mwanadamu hawezi kufanikiwa.

Waangalie hao waabudu mizimu kabla hawajaenda kufanya chochote huenda kutambika kwa mizimu yao au kuangalia milango yao ya mafanikio kwamba waendako watafanikiwa au hawatafanikiwa.

Wapo watu wananguvu sana hapa duniani wanachimba mitaro ili wapate hela ya kuwasaidia kupata chakula chao cha kila siku na siyo kuwafanya waanzishe kitu chao.

Lakini pia wapo walioanzisha kitu chao na bado kile kinawapa chakula tu na siyo kuwapa kitu cha ziada kitakachowasaidia kujitanua zaidi kiuchumi.

Hali hii ikionekana kwa watu kama hawa huwa ni vigumu sana kutoka kwenye umaskini.Maana mtu yeyote ambaye anapata cha kula tu na hana ziada kufanikiwa kwake huwa ni ngumu bali hubaki mtumwa.

Mungu ameweka utaratibu katika maalumu ili aweze kukufanikisha ufikie kiwango cha kuitwa mbarikiwa.



MAMBO YA KUZINGATIA ILI MUNGU AKUFANIKISHE

Mungu anayazingatia mambo yafuatayo ili akufanikishe kiuchumi.
1. Malango

2. Madhabahu

3. Agano

1. MALANGO

Mafanikio ya kiuchumi yamebebwa na malango ya kiroho ambayo Mungu huyatumia kuzungumza na mtu kama vile kwa ndoto au maono.

Yakobo alikuwa makini sana kusikia sauti ya Mungu alipozungumza naye kwa njia ya ndoto.

Yeye mwenyewe kwa kinywa chake alisema kama ifuatavyo:
Mwanzo 28 :16-17
                 16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
    17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.

Ili Mungu amfanikishe mtu hutafta namna ya kuzungumza na huyo mtu ili atekeleze alichoambiwa akifanye .Aliona achague mahali pa utulivu ambapo atazungumza na Yakobo kwa habari ya kumfanikisha na kumlinda.

Mtu anamilango ya mafanikio ,na milango hiyo imeunganishwa na mbingu kwaajili ya Mungu kumfanikisha .

Katika kila kitu mtu atakacho kukifanya anatakiwa kusema na Mungu ili afungue malango yake.Na hapo lazima ajue kwamba mafanikio yake akiyahusisha na Mungu awe mtakatifu mbele zake ,maana hatuwezi kutenganisha utakatifu na mafanikio ya kiuchumi.

Hatuwezi kutenganisha utakatifu na mafanikio ya kiMungu kwasababu Mungu anazungumza na mtu mtakatifu anamwonyesha nini akifanye ili afanikiwe kiuchumi.

Baraka za Mungu hazimfikii mtu bila kuwa mtakatifu mbele zake.
Malango ya mtu hayawezi kufunguliwa akafanikiwa kama mtu huyo hataki kumsikiliza Mungu.Vinginevyo ataambulia kuzungumza na mashetani ili yamfanikishe.

Katika eneo unalofanyia kazi kuna lango la kiroho kati yako na Mungu wako .Kama hilo lango likiwa limevamiwa na nguvu za giza utayaona matokeo yafuatayo:

I. Kazi kuwa ngumu kama vile kuwa na uchovu usio wa kawaida.
II. Kama ni mfanya biashara utaona mauzo hafifu sana kwako wakati jirani yako anauza kwa wingi.
III. Kupotelewa na mizigo uliyoagiza .
IV. Kupotelewa na fedha.
V. Kukosa akiba mda mwingine unakula mpaka mtaji.
VI. Wateja kuulizia vitu na kuacha na kwenda kuchukua bidhaa ileile kwa jirani unajionea kwa macho.
VII. Kukata tama

Ni vizuri sana kabla ya kuanza jambo ufanye maombi ya kufungua malango katika eneo hilo ili Mungu atawale mahali hapo.
Hakikisha unabatilisha roho ya mauti mahali hapo iachie malango ya eneo hilo.

Ombea malango yako ya kiroho na kiuchumi pia.

Angusha ufalme wa giza ulioshikilia anga la mahali hapo.

Alika malaika wa Mungu watawale anga la mahali hapo walinde vitu vyako pamoja na wewe pia.

Kumbuka kwamba pande zote za dunia ni malango yako ya mafanikio ambazo Mungu hutumia kuwaleta watu kwaajili yako ili wewe ufanikiwe kiuchumi.Kwahiyo batilisha roho ya mauti iliyofunga hayo malango ili yawe wazi.
Malango ni mahali pa Mungu kusema na mtu .Pia ni mahali pa kupitishia baraka za mtu kwahiyo mruhusu Mungu ayatawale.
Isaya 60:11
Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.
                                 

           
 MUNGU AKUBARIKI SANA KARIBU SOMO LA PILI

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*