MAFANIKIO YA KIUCHUMI
*π°MAFANIKIO YA KIUCHUMI π°*
SOMO LA PILI
Mwl Peter Francis Masanja
0679392829
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
π° 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Mwanzo 28 :20
21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.
Mwanzo 28 :21
22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Mwanzo 28 :22
π Katika somo la kwanza nilifundisha somo la malango yako ya kiuchumi na mambo ya kushughulikia kwenye malango yako .
πLeo nakukaribisha katika somo hili la pili tujifunze jambo moja kwa ufupi.
ππππππππππ
✍π» *MAFANIKIO YA KIUCHUMI NI AGANO*
π Kila aliyefanikiwa kiuchumi alifanya agano kati ya uchumi wake na kile anachokiabudu .
π Inawezekana ikawa kafanya agano na mashetani akapokea masharti fulani ayafuate ili apate kujitanua kiuchumi kama vile kutoa kafara za damu ya ndugu zake ,mke wake , watoto wake, wazazi wake ,au wafanya kazi wake .Pia anaweza kupatana watu waugue magonjwa tu ya ajabu kama vile magonjwa ya akili n.k.Aidha , anaweza pia akaweka agano na kuzimu la kuoa na kuacha wake au kutokusaidia ndugu zake .
π Vivyo hivyo na mafanikio ya watu wa Mungu aliyehai mafanikio yao yapo kwenye agano na Mungu wao .
π Mungu akitaka kumfanikisha mtu anazingatia sana agano kati ya huyo mtu na uchumi wake ambalo kamwekea Mungu .
π Tunamwona Yakobo aliagana na Mungu kabla ya kwenda kutafta na alimfanikisha sana .
*π° 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;*
Mwanzo 28 :20
*21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.*
Mwanzo 28 :21
π Yakobo aliweka nadhiri kwa Mungu kuhusu mafanikio yake ya uchumi .
πNadhiri ni ahadi ya kutimiza jambo fulani kwa kile ulichofanyiwa au unachotarajia kukifanya au kufanyiwa .
π Nadhiri kwa maana nyingine ni makubaliano au mapatano .
πHakuna nadhiri bila kuwa na makubaliano
π Na hakuna agano bila kuwa na makubaliano au mapatano .
π Jambo la muhimu sana Mungu analitumia kumfanikisha mtu ni kuagana naye kwamba huyo mtu atafanya nini kwa ajili ya Mungu endapo atamfanikisha .
π Mungu ni mwaminifu sana katika agano au patano .Agano ni mkataba kwahiyo mtu wa Mungu anatakiwa aheshimu asitoke nje ya huo mkataba .
π unapofanya agano la kiuchumi ujue mpaka wana wa wanao watanufaika na huo uchumi .
π Katika Somo linalofuata tutaona matokeo ya kufanya agano na Mungu kiuchumi
Karibu sana .
Maoni
Chapisha Maoni