KIJANA JITAMBUE

KUJITAMBUA


Somo la Kwanza


Mwl Peter Francis Masanja

0679392829


πŸ–ŠNi muhimu sana kuongea na vijana wenzangu katika kizazi hiki .


πŸ–ŠNeno la Mungu linasema sana mambo mazuri kuhusu vijana .


*πŸ”° Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.*

1 Timotheo 4:12



πŸ–ŠMungu hajamuumba kijana ili ujana wake udharaulike


πŸ–ŠKijana yeyote hajazaliwa ili aaibike katika ujana wake .


πŸ–Š Ni jambo la aibu kijana kushindwa kujitambua .Pale anaposhindwa kujitambua ndipo huja kudharauliwa katika ujana wake .

πŸ–ŠKijana anayejitambua kwanza anatambulishwa na mambo haya mawili ya kwanza


1⃣ USEMI


πŸ–ŠKatika usemi , kijana ambaye anampenda Mungu lazima kinywa chake pia kibadilike ,yaani usemi wake .


πŸ–ŠSiyo kila misemo kijana utaisema kama vile kumwita mkristo mwenzako

πŸ‘‰Oyaaaa

πŸ‘‰Msela vipi

πŸ‘‰ Mchizi wangu vipi


πŸ–ŠHata katika salamu siyo kila salamu zinafaa uziongee mfano

πŸ‘‰ mzuka

πŸ‘‰balida

πŸ‘‰ cool

πŸ–Š Vijana usemi wao unapaswa wajipambanue , wengi ni wamevutwa na usemi wa kimatataifa na kuacha kuwa na usemi mzuri kwao kutamka Bwana Yesu Kristo asifiwe wakikutana mtaani hakuna .Pia hii salamu wameifanya ya ubaguzi wanawasalimu wale waliokaa sana uweponi mwa Mungu .


πŸ–ŠKijana anayempenda Mungu maneno yake yamtukuze Mungu


2⃣ MWENENDO


πŸ–ŠMwenendo ni kitu cha muhimu sana kwa Kijana .

*πŸ”° 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.*

2 Timotheo 3 :17


πŸ–ŠIli kijana akamilike atambue ameitwa na Mungu kutenda mema .


πŸ–ŠKatika hayo matendo ajue kwamba kuenenda kwake kunapimwa na neno la Mungu .


πŸ–ŠKila akifanyacho na akipime kama kinautukufu wa Mungu au la !

πŸ–ŠKama hicho kitu hakina utukufu wa Mungu basi Kijana anapaswa akiache ili ujana wake usidharauliwe .


*πŸ”° 17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.*

Wakolosai 3 :17


πŸ–ŠKama ukifanyacho huwezi kumwambia Mungu ahsante kwa hiki basi kiache .


*πŸ”° 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.*


1 Wakorintho 10 :31


πŸ–ŠHauwezi kufanya uasherati ukamshukuru Mungu .Kwahiyo kama jambo lolote halina nafasi ya kumshukuru Mungu ni la kuaibisha ujana wako.


πŸ–ŠMungu akubariki sana


Karibu somo la pili

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*