MAOMBI YA KIBALI
*π° MAOMBI YA KIBALI π*
πSOMO LA PILIπ
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
http://peterfrancismasanja.blogspot.com
π° Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Mwanzo 39:21
πKati ya vitu vya muhimu katika maisha ya wokovu ni pamoja na kuomba Mungu akupe kibali .
πUnaweza ukasota miaka mingi sana huendelei kama kaini na kubaki unajaa wivu na kinyongo kwa watu wanaofanikiwa kumbe hujamwomba Mungu akupe kibali .
π Maisha ya mtu ya kuweza kufanya vitu vikubwa yamebebwa na kibali .
π Ukitaka kuanzisha biashara lazima uwe na leseni ya biashara .
π Ukitaka kuwa dereva anayetambulika na anayeweza kuomba kazi ya udereva lazima uwe na leseni .Hiyo leseni ndiyo kibali cha kupata hiyo kazi .
π Katika mambo yako yote tambua kuwa chochote utakacho kukifanya kina uhusiano na maisha yako ya kiroho.
π Wafalme hawakuweza kwenda vitani bila kuomba kibali toka kwa Mungu.
π° Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye Bwana akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.
1 Mambo ya Nyakati 14:10
πPia unatakiwa ujifunze kwamba ni kibali cha Mungu pekee kitakachofanya uinuliwe viwango vya juu.
πKama hujaomba Mungu akupe kibali machoni pa watu utahangaika kufanikiwa kwako .
π Nakuombea leo hiyo roho ya kukataliwa ikuachie katka jina la Yesu Kristoπ₯π₯
Itaendelea.....
Maoni
Chapisha Maoni