MACHO YA MWANADAMU

*πŸ–Š MACHO YA MWANADAMU πŸ–Š*

SEHEMU YA KWANZA



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


Bwana Yesu Kristo apewe sifa .


πŸ–Š Nakukaribisha sana katika somo hili litakalokufanya ubadili mtazamo wa kibinadamu utazame kama Mungu atazamavyo na kuenenda kama Mungu atakavyo .

πŸ–Š Somo hili nimelipa kichwa kisemacho macho ya mwanadamu kwa sababu macho ni taa ya mwili wa mwanadamu .


πŸ“– 22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.

Mathayo 6 :22

23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!

Mathayo 6 :23

πŸ–Š Macho yako yanaweza kukupa kufanukiwa au kushindwa kwako .

πŸ–Š Macho yako yanaweza yakakufanya udharau kitu kwa kukiangalia .

πŸ–Š Macho yako yanaweza kukufanya uhofu kitu fulani pale unapikiona katika safari yako na ukafanya uamzi wa kuahirisha safari au ukakimbia kabisa .


πŸ–Š Tunashidwa vita kwa kuangalia wingi au ukubwa wa mtu .


πŸ–Š Sikiliza nikwambie mwana wa Mungu jambo lililofichika katika macho yako .

πŸ–Š Unajua kwamba kuna watu huona jambo na kujiandikia kufa kwao ❓

πŸ–Š Naam unaweza ukaona jinsi gani Israeli pale jangwani walijiandikia kufa kabisa .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua *macho yao* , na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana.

Kutoka 14 :10

11 Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko *ili tufe jangwani* ? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?

Kutoka 14 :11



πŸ–Š Israeli walipoona wingi wa jeshi la farao walijiandikia kufa jangwani .

πŸ–Š Macho yao yaliona kisha hofu ikawaingia na kupoteza matumaini ya kuishi kabisa .

πŸ–Š Macho ya mwanadamu yanaweza kumfanya mtu awe na hofu na kujihesabia kufa pale aonapo kitu cha kutisha .

πŸ–Š Musa alipowatuma watu kuipeleza nchi ya Kanaani wapelelezi waliona watu wakubwa sana wao wakajawa na
πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

1⃣ Hofu

2⃣ Kujidharau

πŸ–Š Walipo waona wana wa Anaki ( wanefili ) waliogopa sana wakajiona ni dhaifu sana hata hawawezi kupigana nao .

πŸ–ŠWalijiona kama panzi kwa Wanefili ( wana wa Anaki ).

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, *Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.*

Hesabu-Numbers 13 :31

32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala *watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.*


Hesabu-Numbers 13 :32

33 Kisha, *huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki* , waliotoka kwa hao Wanefili; *tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.*


Hesabu-Numbers 13 :33

πŸ–Š Kuna mambo ukiyaangalia kwa macho yako yatakushinda kwasababu yapo juu ya uwezo wako .

πŸ–Š Israeli walipoona Wanefili wakajiona si kitu na kujihesabia hawawezi kabisa .

πŸ–Š Walijiona dhaifu sana wala hawawezi kupigana na Wanefili .


πŸ–Š Lakini Mungu hakuangalia kama wao wanavyoangalia .


πŸ–Š Wanefili nao vivyo hivyo kwa macho yao waliwahesabu Israeli si kitu yaani ni kama panzi tu 🀣🀣🀣lakini Mungu hakuangalia kama wao waangaliavyo .


πŸ–Š Macho ya mwanadamu yanaweza yakamfanya afuate maamuzi yasiyo ya KiMungu na kuacha kumtegemea Mungu.


πŸ–Š Lakini tunaona kuna mtu katika hao wapelelezi hakuangalia kibinadamu bali aliangalia kama Mungu aangaliavyo .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 30 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Hesabu-Numbers 13 :30


πŸ–Š Kalebu pamoja na kwamba aliwaona Wanefili hakuogopa urefu wao na nguvu zao maana aliangalia kama Mungu aangaliavyo ambaye ndiye adui wa adui za kila mtu amwaminiye na kutembea katika njia zake kama ilivyoandikwa

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.


Kutoka 23:22

πŸ–Š Naam , macho ya mwanadamu yanamatokeo makubwa sana katika maisha yake .

πŸ–Š Matokeo haya yanaweza kuwa mazuri au mabaya sana .

πŸ–Š Macho ya mwanadamu yanaweza kumfanya asimsikilize Mungu kabisa asikilize sauti za wanadamu.

πŸ–Š Wanadamu wanamitazamo yao kulingana na kile wakionacho

πŸ–Š Wanaweza wakakitazama na kukidharau na kukiona .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

1⃣ Kidogo

2⃣ Kifupi

3⃣ Dhaifu


πŸ–Š Lakini Mungu anakiangalia hicho kidogo , kifupi au dhaifu kama chombo cha kuwakomboa watu wengi sana ambapo bila hicho watu wangeangamia .

πŸ–Š Daudi alidharauliwa sana na kufanyiwa dhihaka wakati mwingine pale aliposema ataweza kupigana na Goliati


πŸ–Š Watu wote ndugu zake na wale wengine walimsema mtoto mdogo sana na ni dhaifu sana wala hawezi kumpiga Goliati.


πŸ–Š Lakini Mungu alimwona ni shujaa sana .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 33 *Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye* ; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.
1 Samweli 17 :33

41 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
1 Samweli 17 :41

42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, *akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri* .

1 Samweli 17 :42

45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.

1 Samweli 17 :45

46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

1 Samweli 17 :46

47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.

1 Samweli 17 :47

48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.

1 Samweli 17 :48

49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.

1 Samweli 17 :49

50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.

1 Samweli 17 :50

πŸ–ŠKumdharau mtu kwa mwonekano au kwa hali aliyonayo ni vibaya sana .

πŸ–Š Maana kila mtu Mungu humtumia katika eneo fulani ambapo wewe hupawezi kabisa kufanikisha kusudi lake .

πŸ–Š Mungu haangalii hali ya mtu ya kudharauliwa kwa sababu ni mdogo, mfupi, maskini ,na dhaifu huyo ambaye wanadamu wanamwona hawezi ndye anakuwa mkombozi wao .


πŸ–ŠDaudi alionekana mdogo sana kwa macho ya wanadamu lakini Mungu alimtumia kushinda vita .

πŸ–Š Hii ndyo kusema kwamba macho ya mwanadamu yanaweza kuangalia kitu /mtu na kumdharau lakini Mungu ameweka kitu kikubwa sana ndani ya hicho kitu au mtu ambacho wanadamu hawawezi kukiona mpaka waone utendaji wake .Ndivyo ilivyokuwa kwa Daudi .

πŸ–Š Nakutakia siku njema

πŸ–Š Usikose mwendelezo wa somo hili

πŸ–Š Tutakuja tuangalie

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

Macho ya mwanadamu dhidi ya maamuzi katika

1⃣ Uongozi

2⃣ Ndoa

3⃣ Uchumi



Karibu sana

Ni Mimi

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

francispeter424@gmail.com


Unakaribishwa kwa maswali na maoni.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*