MAOMBI YA KIBALI
π *MAOMBI YA KIBALI* π SOMO LA KWANZA Mwl Peter Francis Masanja 0679392829 http://peterfrancismasanja.blogspot.com π° 1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Isaya 43 :1 2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Isaya 43 :2 3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. Isaya 43 :3 4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. Isaya 43 :4 π Mungu hajakuumba kwa bahati mbaya bali anampango mzuri kabisa juu yako . π Lakini ili yale aliyoyapanga kwako yatimie unahitaji ujitambue . π Umehangaika miaka ...