MAOMBI YA KIBALI

🖊 *MAOMBI YA KIBALI* 🖊


SOMO LA KWANZA


Mwl Peter Francis Masanja

0679392829

http://peterfrancismasanja.blogspot.com

🔰 1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

Isaya 43 :1

2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

Isaya 43 :2

3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.

Isaya 43 :3

4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.

Isaya 43 :4


🖊 Mungu hajakuumba kwa bahati mbaya bali anampango mzuri kabisa juu yako .

🖊  Lakini ili yale aliyoyapanga kwako yatimie unahitaji ujitambue .

🖊 Umehangaika miaka na miaka hupati au hufanikiwi kabisaa

🖊 Unajuhudi katika kazi za mikono yako lakini hujamtambua Mungu amekuandalia kitu gani kwaajili ya maisha yako .


🖊 Somo la mafanikio wengi hulihubiri vibaya saaana .

🖊 Ili ufanikiwe unahitaji kupatana na Mungu kwanza .


🖊 Ili ufanikiwe unahitaji uwe mnyenyekevu kwa Mungu .


🖊 Huwezi kumwomba Mungu akupe kitu kama huna uhusiano naye mzuri .


🖊 Mungu akiwa na uhusiano na wewe vizuri atasema na wewe moja kwa moja kuhusu uchumi wako na siyo kuitwa na mtumishi ukaombewe upate gari .


🖊 Jambo la kuzingatia sana ni kwamba Mungu ukiwa na uhusiano naye vizuri anakufanya rafiki yake .


🖊 Katika maombi ya leo unachotakiwa kuomba ni kibali na siyo kazi wala mali .


🖊 Mali ni matokeo ya kibali unachopewa na Mungu .


🖊 Kama Mungu hajakupa kibali cha kumiliki mali utahangaika sana .

🖊 Mungu akikupa kibali anakufanya ukubalike mbele za watu wamchao na wasiomcha yeye .


🖊 Unapokuwa na kibali atakupa uimara mzuri sana .


🖊 Ninapokwambia omba kibali cha kumiliki na kutawala ninamaana kubwa saana .


🖊 Ili Mungu atoe watu kwaajili yako ujue ametoa kibali kwako .


🖊 Kama hajatoa kibali utapatana na watu wa kukufilisi kila siku .

🖊 Omba kibali kwenye biashara yako na ndoa yako .

🖊 Unapokuwa umeomba kibali ujue mpaka amekupa kibali ameona uhusiano wako na yeye umekuwa mzuri .


🖊 Amesema atatoa watu kwaajili yako .


🔰 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.


Isaya 60:11



🖊 Anapotaka kukufanikisha huanza kuangalia uhusiano wako na yeye .


🖊 Kibali ni cha muhimu sana kuliko kazi uombayo .


🖊 Unapokuwa na kibali Mungu atakukutanisha na watu sahihi na kazi sahihi

🖊 Unapokuwa na kibali vitu vingine utaletewa na vingine utaitiwa .


🖊 Unapokuwa na kibali utaanzisha kitu kitafanikiwa.

🖊 Mruhusu Mungu atawale maisha yako.



Mungu akubariki saana

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*