FAIDA YA KUOMBEA TAIFA








AYUBU 22:21



πŸ‘‰ *_Taifa ni nini_* ❓

Taifa ni watu wanaoishi katika eneo fulani waliounganishwa na lugha moja kama njia ya mawasiliano yao ya kila siku .

πŸ’’ Katika taifa lolote kuna mfumo wa utawala unaoongoza watu waweze kufikia malengo yao ya kimaisha ili wapate kuifurahia nchi yao waikaayo .

πŸ‘‰ Taifa lolote linahitaji kuendesha kwa misingi na kanuni za Mungu ili kila kitakachofanyika kipate kibali kwa Mungu ili watu wakaao katika nchi hiyo wabarikiwe .

 πŸ‡ΉπŸ‡Ώ_Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.

Mwanzo 11:6πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

_ πŸ‡ΉπŸ‡Ώ *Nchi ni nini* ❓

Nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya umiliki .

πŸ‘‰ Tanzania ni nchi yenye mipaka halali ya umiliki , ndyo maana kaskazini imepakana na Kenya na Uganda , Mashariki imepakana na bahari ya Hindi , Kusini imepakana na Msumbiji na Zambia , na Magharibi imepakana na Congo .

 _Nchi hii inamilikiwa na watu wa kabila mbalimbali kabila zaidi ya 120_

πŸ‘‰Nchi hii inategemea watu hawa waitunze na kuiombea pia

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kabla ya kuombea taifa ombea nchi ( ardhi ) ya Tanzania ili kila pando ambalo shetani alilisimamisha litoweke , anza na toba ili Mungu ayasamehe kila maovu yaliyotendeka katika nchi yakoπŸ‡ΉπŸ‡Ώ naye Mungu ametupa ahadi atatusikiliza na kuitakasa nchi yetu .

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
2 Mambo ya Nyakati 7 :14


15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.
2 Mambo ya Nyakati 7 :15

16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
2 Mambo ya Nyakati 7 :16

17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;
2 Mambo ya Nyakati 7 :17

18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 7 :18

πŸ‡ΉπŸ‡ΏSasa , baada ya toba ondosha kila roho chafu na maagano yaliyokuwa yamelikamata taifa lisifanikiwe , vunja zile madhabahu

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ 2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;
Kumbukumbu la Torati 12 :2

3 nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.
Kumbukumbu la Torati 12 :3
πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

πŸ‡ΉπŸ‡ΏTAKASA ARDHI YA TANZANIA PAMOJA NA MALANGO YAKE KWA DAMU YA YESU

πŸ‘‰ 30 Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na malango, na ukuta.
Nehemia 12 :30

πŸ‡ΉπŸ‡ΏUnapotakasa nchi yako takasa na watu na viongozi wa nchi wanaoongoza ili waongoze na kutenda haki

πŸ’’ 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9 :22

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ NCHI IKITAKASWA ,TAIFA LINABARIKIWA NA WATU WAKAAO HUMO HUFANIKIWA

πŸ’’ 1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Kumbukumbu la Torati 28 :1

2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 28 :2

3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Kumbukumbu la Torati 28 :3

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Kumbukumbu la Torati 28 :4

5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
Kumbukumbu la Torati 28 :5

6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
Kumbukumbu la Torati 28 :6

7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Kumbukumbu la Torati 28 :7

8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 28 :8

9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
Kumbukumbu la Torati 28 :9

10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako.
Kumbukumbu la Torati 28 :10

πŸ‘‰Naiona Tanzania inazidi kuogopwa na mataifa mengine kwasababu Mungu amesikia Maombi ya watu wake na kuibariki .

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ. Rafiki yangu usichoke kupaza sauti juu ya nchi yako Tanzania , ili Mungu azidi kuibariki na kuilinda .

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ 6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
Isaya 62 :6

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.
Isaya 62 :7

πŸ‘‰Usinyaze kuiombea nchi yako Tanzania , Mungu anasubiri utamke jambo jema naye afanye.

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ KWA NINI TUOMBEE TAIFA ❓

Tunaombea Taifa ili

1. Amani itawale

2. Watu wakaao katika nchi hiyo wafanikiwe

3. Shetani asipate nafasi ya kupitisha mipango yake.

Mungu akubabiri sana katika kuliombea Taifa

Perter Francis

0679392829

francispeter424@gmail.com

Maoni

  1. Amen mtumishi nimebarikiwa sana na neno lako ubarikiwe pia

    JibuFuta
  2. Mtu wa Mungu ujumbe huu ni mnzito sana Mungu akubariki sana.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*