*KUMKOMBOA ALIYEFUNGWA NA MIUNGU YA UKOO*

πŸ”₯ *KUMKOMBOA ALIYEFUNGWA NA MIUNGU YA UKOO* πŸ”₯





Sehemu ya Kwanza







πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’






10 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma,
Zaburi 107 :10



πŸ‘‰ Mtu alinayetumikishwa na miungu ya ukoo yupo kwenye taabu sana

Amefungwa hafurukuti na ana asilimia chache sana za kumjua Mungu


Hivyo basi anahitaji kufunguliwa huko alikoshikwa kupitia matambiko na matamko ya ukoo



2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Mithali 6 :2



πŸ‘‰Maneno yanakamata maisha ya mtu

Hivyo jina lako likiingizwa kwenye orodha ya majina ya ukoo kupitia matambiko utahangaika sana



πŸ‘‰ Unaweza ukashangaa tena baadhi ya familia wanafunga mbuzi wenye mabaka meusi na meupe na wale mbuzi weusi kengele shingoni ili kupitia hao mbuzi wakiomba jambo lolote watalipata



Cha ajabu zaidi hao mbuzi wanapewa majina ya mababu waliokwisha kufariki tayari na kuwafanya miungu yao


πŸ‘‰ sasa utakuta unapewa jina hilo na kunambuzi au ng'ombe nyumbani kwenu amefungwa kengele anaitwa jina hilohilo ulilonalo



πŸ‘‰ Basi ukiona umepewa jina hilo ujue umeunganishwa kwenye mizimu ya ukoo na sasa unahitaji kufunguliwa kutoka kwenye kifungo hicho


Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili.

Zaburi 18:5
Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;

Zaburi 116:3



πŸ‘‰ Ile kengele aliyofungiwa huyo mbuzi aliyepewa jina sawa na lako inauhusiano na mauti na kuzimu

Nawewe umefungwa hiyo kamba katika ulimwengu Wa roho japo katika ulimwengu wa macho huioni

Hiyo imekuwa nira kwako lazima uitoe



Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.

Isaya 10:27


Naomba niishie hapa huu ni utangulizi wa somo hili


Peter Francis

0679392829

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*