MAJIBU YA MAOMBI YAKO YANATEGEMEA IMANI ULIYONAYO*

*MAJIBU YA MAOMBI YAKO YANATEGEMEA IMANI ULIYONAYO*







πŸ‘‰ Ukiamini kupokea vidogo utapokea vidogo


πŸ‘‰Mungu atakujibu kulingana na unachoamini


πŸ‘‰Yule mwanamke aliyetokwa damu mda wa miaka 12 aliamini akigusa vazi la Yesu atapona .Ndyivyo ilivyokuwa akapona



25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,
Marko 5 :25

26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya
Marko 5 :26

27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
Marko 5 :27

28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
Marko 5 :28



πŸ‘‰Wengine waliamini katika kuwekewa mikono na Yesu wakapona na ndivyo ilivyokuwa


22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,
Marko 5 :22

23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Marko 5 :23



πŸ‘‰ Wengine waliweka imani yao kuwa Yesu akitamka tu watu wao watapona hata kama asifike nyumbani . Hii ndivyo ilivyokuwa kwa yule akida



Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

Mathayo 8:5
Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Mathayo 8:8
Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.

Mathayo 8:13



 *
 *MASWALI YANGU KWAKO NI HAYA**




Unaamini kuwa Yesu anaweza kutenda jambo ndani yako❓

Tambua kwamba usipo amini hvo utafunga na kuomba na majibu ya maombi yako hupati



Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Waebrania 11:6




Unamchukulia Yesu kwa viwango gani ❓





 *HITIMISHO*


Imani yako ndyo majibu ya Maombi yako

Ukiomba kwa Mungu uishi maisha ya katikati yaani maisha ambayo huonekani tajiri wala huonekani kuwa maskini Mungu atafungua milango ya baraka kwa kadri ulivyoomba


Ukiomba mbele za Mungu akubariki umiliki uchumi mkubwa Mungu atakufungulia milango ya baraka na utamiliki kwelikweli




Peter Francis

0679392829





Mungu akubariki

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*