JE , WEWE NI MTAKATIFU

JEJE WEWE NI MTAKATIFU* ❓

Mwlm.Peter Francis Masanja

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Wengi uliwaonya waache dhambi wakakuuliza hili swali

Jibu la hilo swali ni ndyo

👉wewe ni mtakatifu

: Wewe ni mtakatifu kwa sababu hushiriki matendo ya giza

: Nini basi maana ya kuitwa mtakatifu ?

: Katika mtakatifu ni mtu yeyote aliyetengwa na uchafu wa dunia hii ili atumike kwa kazi ya BWANA

Chombo au kitu kitakatifu kimetengwa kwa ajili ya kazi ya Mungu

Huwezi kupeleka kinanda cha kanisani kikapigiwe mziki kwenye bar au virabu vya pombe

Unafikiri kwanini ❓

Ni kwa sababu kimewekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu

Aliyeokoka hawezi kwenda night club au kujiuza au kununua makahaba

Kwa sababu Mungu kamchagua awe mtakatifu wake kwa ajili ya kazi yake Mungu: Ni nani achukuaye vyombo vya kanisani vya mziki kwenda kupiga mziki kwenye bar ❓

Jibu ni hakuna awezaye

Vivyo hivyo na aliyeokoka hawezi kwenda kufanya vikao bar

Maana hata Mungu atamshangaa

Utakatifu unasisitizwa sana kwenye biblia

Biblia yenyewe ni takatifu kwahyo aisomaye pia yampasa awe mtakatifu

Asemaye kuwa yeye si mtakatifu na huku anasema ameokoka huyo anamkataa Mungu

Yaani anasema yeye si wa Mungu .

Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.

Mambo ya Walawi 11 :44

45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.

Mambo ya Walawi 11 :45

Rafiki yangu unaye nisikiza hapa inawezekana ulimkemea mtu dhambi akakuuliza

Inamaana wewe ni mtakatifu

Na wewe kwa sababu hukujua aliyeokoka na kuijua kweli ya Mungu ni mtakatifu ulijikana .

Akikuuliza mwambie wewe ni Mtakatifu

JE NI NANI ATAKAYEINGIA MBINGUNI BILA KUWA MTAKATIFU

Jibu ni hapana hata mmoja

👉 kwahyo wewe uliyeokoka ni mtakatifu

📖 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

Waebrania 12 :14

Wewe ni mtakatifu ndyo maana Mungu amekupa yafuatayo :

👉 Baraka

👉 Anajibu maombi yako

👉 Ulinzi ( ndyo maana hakuna wa kukuroga .)

ISAYA 62:6

MUNGU AMEKUCHAGUA UWE MTAKATIFU

📖👨🏻‍💻 Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.

Mambo ya Walawi 20:26

Maombi yetu yanajibiwa kwa sababu sisi tumchao BWANA ni watakatifu

Kwahiyo Mungu atakujibu Maombi yako ukiishi maisha matakatufu

👉Mungu aliwakemea Israeli kwa ibada*, *sifa*,na *matoleo*,waliyofanya huku wakiwa katika dhambi

📖👨🏻‍💻11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.
Isaya 1 :11

12 Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?

Isaya 1 :12

13 Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.

Isaya 1 :13

14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua.

Isaya 1 :14

15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu
.
Isaya 1 :15

16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;

Isaya 1 :16

17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.

Isaya 1 :17

UTAKATIFU UNAMFANYA MUNGU AKUOKOE

*Utakatifu ni kujitenga na uchafu wa dunia hii yaani dhambi .*

📖👨🏻‍💻 1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

Isaya 59 :1

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Isaya 59 :2

Mungu anahidi tuwe watakatifu ili atujibu Maombi Yetu

📖👨🏻‍💻14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

2 Mambo ya Nyakati 7 :14

15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.

2 Mambo ya Nyakati 7 :15

16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.

2 Mambo ya Nyakati 7 :16

Alimtoa Yesu afe pale msalabani ili sisi tufanyike watakatifu akatutenga mbali na dhambi

📖👨🏻‍💻 46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Mathayo 27 :46

YESU ALIMAKIZA KILA KITU MSALABANI AKASEMA IMEKWISHA

👉 Kwahyo aliposema imekwisha alikutenga mbali na dhambi

📖👨🏻‍💻 30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.

Yohana 19 :30

PETRO PIA ALISISITIZA SUALA LA UTAKATIFU

📖👨🏻‍💻 16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

1 Petro 1 :16

KWA KUWA MUNGU NI MTAKATIFU YATUPASA KUFANYA KILA JAMBO KWA MAPENZI YA MUNGU

👉HATA NDOA YAKO INATAKIWA IFUNGWE KANISANI ILI IWEVTAKATIFU KUWA MUNGU NI MTAKATIFU💍👫

👉Usifunge ndoa za kimila

👉Usifunge ndoa za kiserikali

👉 Usiishi na mwanaume kama mume kabla ya ndoa

📖👨🏻‍💻 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

1 Wakorintho 10 :31

.NDYO MAANA YESU ALIZALIWA MTAKATIFU NA AKAISHI MAISHA MATAKATIFU AKATUACHIA KIELELEZO CHA KUFUATA

📖👨🏻‍💻 21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

1 Petro 2 :21

22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

1 Petro 2 :22

NEEMA YA YESU INATUFUNDISHA UTAKATIFU NA KUCHUKIA DHAMBI

📖👨🏻‍💻 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
Tito 2 :11

12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

Tito 2 :12

Utauwa maana yake ni utakatifu

SISI NI NURU NA TUMEBEBA NURU NA NURU HII NI UTAKATIFU

KWAHIYO INAPASWA IANGAZE

📖👨🏻‍💻 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

Mathayo 5 :14

15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

Mathayo 5 :15

16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Mathayo 5 :16

. HITIMISHO

UTAKATIFU WETU TUUTUNZE ILI TULIFANYE JINA LA BWANA LISITUKANWE

👉Litatukanwaje❓

Tukiwa sisi tuliookoka ndyo wa kwanza kutenda maovu tutamfanya Yesu atukanwe na wasioamini

📖👨🏻‍💻 17 Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu,

Warumi 2 :17

18 na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati,

Warumi 2 :18

19 na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani,

Warumi 2 :19

20 mkufunzi wa wajinga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati;

Warumi 2 :20

21 basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe?

Warumi 2 :21

22 Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?

Warumi 2 :22

23 Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?

Warumi 2 :23

24 Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.

Warumi 2 :24

💒💒💒💒👑💒👑

Mungu akubariki

Mwlm. Peter Francis

📖📖📖📖📖👨🏻‍💻👨🏻‍💻👨🏻‍💻👨🏻‍💻👨🏻‍💻

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*