KARAMA NA HUDUMA ZA KIROHO KATIKA KANISA

SOMO:(3)-KARAMA NA HUDUMA ZA KIROHO KATIKA KANISA







1. KARAMA SABA ZA MASAIDIANO
Zimewekwa na Mungu Baba ndani ya kila mwanadamu tangu uumbaji, hivyo mtu huzaliwa nazo. (2Tim. 1:4-7)
- Ni vipawa kutoka kwa Mungu kwa kila mwanadamu, iwe ameamini au hajaamini. (Kut.35:35)
- Huonyesha tabia ya misukumo (moyo wa kupenda) ndani ya mtu katika kutambua, kuelewa, na jinsi ya kuyakabili maisha na huduma ambazo Mungu amekusudia mtu huyo azifanye.
- Kila mtu huonyesha mchanganyiko wa karama kadhaa za masaidiano, lakini ipo moja inayodhihirika kwa nguvukuliko nyingine, hivyo twaweza kuiita karama ya msingi ambayo Mungu amemkusudia mtu huyo atumike.
1. Karama Ya Masaidiano Ya Unabii
(Rum. 12:6) Mwonaji/Mtambuzi
- Huona na huelewa kiundani sana maana ya jambo.
- (Bali sio ufunuo;
- Ufunuo ni jambo ambalo halikuwahi kuonekana hapo awali!)
- Kuwa na nuru ya neno la Mungu na nuru ya Roho Mtakatifu katika akili ili kuufunua ukweli wa jambo.
- Mtu aliyejaliwa karama hii
1. Huona au hutambua kiundani zaidi ya sura ya nje.
2. Hupokea na kutangaza ukweli halisi juu ya jambo kama lilivyo.
3. Hupokea na kutangaza undani wa mtu au jambo
4. Mungu Baba humpa mtu huyu uwezo wa kuliona jambo kwa mtizamo wa kiundani sana. Lakini karama hii siyo ile
ya karama ya huduma ya nabii, japokuwa mtu huyu aweza kutumiwa pia)
5. Hupenda na hutamani kukimaliza hadi kiini cha jambo kwa ukweli auonao, bila kubakiza chochote.
6. Haimaanishi kwamba mtu ukiwa na karama hii kwamba ni nabii, bali unaweza kutumika kama;-
Mwenye huduma ya unabii.
Mwalimu mzuri.
Mshauri mzuri.
Kutoa unabii.
JINSI YA Kuitunza:
Usiseme zaidi ya kile Mungu akupacho.
Usipunguze / usinyime kile Mungu akupacho ili kukitoa.
- Kazi Na Faida Ya Karama Hii Katika Kanisa.
Kuutengeneza uhusiano uliovunjika katika mwili wa Kristo.
Kuiendeleza na kuijenga hali ya mtu kutembea pamoja na Mungu maishani mwake.
Yohana Mbatizaji –Ni Mfano Wa Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Unabii.
1. Hakujihusisha na mwonekano wa sura ya nje bali ya ndani pia. (Mt.3:4)
2. Alijiona kama mtumwa asiye na faida (Luk.3:16)
3. Alijitambua kuwa ni sauti tu ya Mungu (Luk.3:3-6)
4. Alikuwa mkweli na mwenye kukabiliana na umati wa watu moja kwa moja kuhusu dhambi zao bila ya kuficha
jambo. (Luk.3:7-9)
5. Hakuangalia upande mmoja tu wa jambo, alionyesha tatizo, suluhisho na matokeo yake (dhambi, haki, na hukumu) Luk.3:10-14)
6. Aliangalia kuwepo kwa toba. (Luk.3:8)
7. Aliweka mkazo mkubwa katika mema na mabaya(Luk.3:10-14)
8. Alitambua nia ndani ya mioyo ya watu, aliuona undani wa jambo. (Luk.3:7)
2. Karama Ya Masaidiano Ya Uhudumu.
Mhudumu / Roho ya uhudumu
Aina za huduma kibiblia katika kanisa ni:-
1. Huduma za kawaida katika kanisa. (Efe.4:12)
2. Huduma za kiutume na neno (Mdo.6:4; 20:24)
3. Huduma au ofisi ya shemasi (Mdo.6:1-3)
Kuhudumu
- Ni kuwa na uwezo wa kukutana na mahitaji yale yasiyofikiwa katika mwili wa Kristo.
- Huduma ya kuwasaidia masikini na wanyonge
- Huduma hii mara nyingi hudharauliwa lakini ni ya muhimu sana katika kanisa,
- Kwani hata BWANA Yesu mwenyewe aliifanya pia. (Yoh.13:3-17)
- Watu wenye karama hii huwa pia ni wenye nguvu za kimwili (stamina).
Martha –Ni Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Uhudumu. (Luk.10:38-42)
1. Ni wa muhimu sana watu hawa katika kanisa.
2. Hupenda kuzifanya kazi wenyewe, si kuagiza watu.
3. Hupenda kutimiza huduma kwa vitendo siyo maneno matupu.
4. Siyo wapangiliaji wa mipango ya kikazi au wafundishaji wa wengine katika kuifanya kazi hiyo.
5. Hujihusisha na mambo mengi, na kujisumbua na mengi, huona vigumu kusema basi au hapana kwa kazi
wanazo pewa au wanazosifanya.
6. Huweza hata kujisahau wenyewe kiroho.
3. Karama Ya Masaidiano Ya Ualimu (Rum.12:7)
Wenye karama hii wanahitajika sana katika kanisa na katika ulimwengu, katika elimu ya kawaida.
Karama hii huelekea;-
Ufahamu au akili.
Kuitafuta kweli na mafundisho kwa nadharia na kwa vitendo.
Kutamani kuwapa wengine ujuzi na kuwaongoza katika kuifahamu kweli.
( 1Tim.5:17)
Apolo – Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Ualimu Katika Kanisa. (Mdo.18:24-28; 1kor.3:6)
KAMA Mwalimu unatakiwa
1. Kumwagilia maji (1Kor.3:6), yaani kulisaidia kanisa likue kiroho.
2. Kuwa mzungumzaji mzuri (–kama Apolo.)
3. Mafundisho yako yasimamie katika maandiko. ( Kama Apolo muweza wa maandiko)
4. Kusema na kufundisha kwa usahihi.
5. Kukubali kufundishwa / kuelekezwa pia (Apolo alifundishwa na Prisila na Akila)
6. Kuwasaidia waamini katika neema.
4. Karama Ya Masaidiano Ya Uhamasishaji. (Rum.12:8)
Kufariji, kutia moyo, kuhamasisha au kuonya.
Mwana wa faraja. (Nuhu, Barnaba)
Kufundisha huelekea ufahamu / akili, lakini kuhamasisha, kuonya, kufariji nakutia moyo, huelekea, nia,
dhamiri, na makusudi-vilivyomo moyoni mwa mtu.
Tabia
Mwenye karama hii husukumwa kuwasisitiza wengine wafikie au wanie kupevuka kiroho.
Hasa huelekea kwa wale walio katika nyakati ngumu na mateso au majaribu ya kukatisha tamaa.
Hutenda kazi vizuri katika ushirika na karama nyingine kama ualimu, unabii, na uchungaji.
(1Tim.4:13; Tito 1:9; 1Kor.14:3, Mdo:36)
Mhamasishaji huamsha wote, mwamini mmoja mmoja, na kanisa zima katika kuvumilia, upendano wa
ndugu, na matendo mema (Ebr.3:13, 10:23-25)
Wahamasishaji wanao uwezo mkubwa wa kuichochea imani na ukuaji wa wengine kiroho.
Barnaba:Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Kuhamasisha Katika Kanisa.
(Mdo.4:36) Mwana Wa Faraja- Kutia Moyo.
1. Wana ujumbe wa kutia moyo. (Mdo.11:22-24)
2. Ujumbe wa kuziimarisha roho za waamini.Mdo.14:20-22)
3. Wako upande wa waamini, hawakati tamaa.(Mdo.9:26-27)
4. Wana uwezo wa kupambanua mtu yupo katika kiwango gani cha kukua kiroho na kuzungumza naye katika
kiwango hicho alichopo mtu huyo.
5. Barnaba aliwahamasisha mitume kumpokea Sauli alipoamini. (Mdo.15:37-39; 2Tim.4:11)
5. Karama Ya Masaidiano Ya Utoaji. (Ukarimu) Rum. 12:8.
Hujisikia hamu sana ya kutoa mali ya binafsi na sio hazina ya kikanisa ili kukutana na mahitaji ya
watu wa Mungu.
Mwenye ukarimu hana ubinafsi.
Huhitajika kuwa na nia safi, kutoa kwa kupenda, na siyo kwa lazima au kujitafutia umaarufu.
Wote huhitajika kutoa zaka na dhabihu, lakini mwenye ukarimu hutoa zaidi.
Ibrahimu –Ni Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Ukarimu.
(Mwenye Kukirimu)
1. Huwekewa dhamana vitu vingi na Mungu (Mwa. 13:1-2)
2. Huwa na ukarimu na moyo huru, moyo wa kupenda au roho huru.(Mwa.13:9-10)
3. Ni watunzaji wazuri sana wa mali zao.( Mwa.14:14-16)
4. Wana maarifa thabiti kwamba Mungu ndiye chanzo cha utajiri, hivyo, humpa Mungu utukufu kwa mali zao
pia. (Mwa.14:22-24)
5. Wanaitambua kazi ya Mungu na kuonyesha mwitikio kwa mali zao. (Mwa.14:18-20)
6. Mungu huwawekea watoaji sehemu yenyewe hasa na kwa wakati halisi.
6. Karama Ya Masaidiano Ya Uongozi / Utumishi
Karama hii hutenda kazi katika ushirika na karama nyingine, kama mitume, manabii, wachungaji na walimu.
Mwenye karama hii huongoza kwa kutenda kazi na kupitia wengine.
Hufanya kazi kwa kupanga na kugawa wajibu na mamlaka kwa wengine.
Hutoa maana ya kazi na msaada wa maelekezo; wakati huo huo, huwaachilia wengine kushiriki katika
kutimiza lengo au kazi hiyo.
Nehemia –Ni Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Uongozi / Utumishi.
1. Kama kiongozi unakuwa na mguso maalumu kwa ajili ya watu wa Mungu. (Neh.1:1-4)
2. Unakuwa na uwezo wa kupitia (kusavei) na kutoa maana ya kinachohitajika kufanywa. (Neh. 2:12-17)
3. Unakuwa na uwezo wa kuligawa lengo kubwa katika njia au kazi ndogo za kuweza kutendeka kwa neno la
hekima. (Neh.3:1-32)
4. Unakuwa na na uwezo wa kustahimili kusongwa na upinzani na bado unasonga mbele. (Neh.4:1-23)
5. Unafanya mambo magumu kuwa mepesi kwa ajili ya wengine wala mwenyewe huwi mzigo kwa wale
unaowaongoza, kutumika badala ya kutumikiwa. (Neh.5:14-19)
6. Unakuwa na ufahamu wa jinsi ya kuyagawa mamlaka yanayohitajika katika kutimiza wajibu unaohitajika.
(Neh.7:1-2)
7. Karama Ya Masaidiano Ya Kurehemu/ Kuhurumia.
Mwenye kurehemu / mwenye huruma.
Karama hii maeneo mengine inafanana na karama ya masaidiano katika utoaji.
Ni huduma ya moja kwa moja kwa wahitaji tu.
Unakuwa na uwezo wa kulitambua jambo lile linalohitajika na linalowatesa waamini au wale unaokutana nao
kiuhitaji.
Unaweza kuwa mshauri mzuri sana kama ukitumia hekima na nidhamu.
Karama hii huhitajika kuitenda kwa furaha kwani, yawezekana kuwa ngumu na isikubalike kwa aliye nayo,
yaweza kukusababisha usiipende, kuichukia, au usiitende kabisa; hali hizi huizima kabisa.
Ili kushinda – unapaswa kumwendea Yeye ambaye rehema zake ni mpya (kila) siku kwa siku na kujazwa
Roho Mtakatifu. (Omb.3:22-23)
Mwenye karama hii utafaulu sana kama utajijenga kwa Neno na Maombi kila siku.
Msamaria Mwema –Ni Mfano Wa Mtu Mwenye Karama Ya Masaidiano Ya Kurehemu. (Luk. 10:29-37)
Isipokuwa; Mungu ndiye mfano mzuri sana wa karama hii, hakuna mfano zaidi yake.
1. Ana huruma sana. (Mstari 33)
2. Huvutiwa sana na waliovunjika moyo. (Mstari 34; Zab.51:17)
3. Huwa na utayari kutenda kitakiwacho; hata kuchafuka mikono ikihitajika. (Mstari 34)- alivifunga vidonda.
BWANA Yesu alikubali kuchafuka kwa ajili ya dhambi zetu, hata hakuwa na uzuri wa kutamanika. (Isa 63:1-3)
4. Huwa makini kwa mahitaji ya watu. (mstari 35) –alilipa deni.
Mfano Wa Kuonyesha Utendaji Wa Karama Zote Saba Za Masaidiano.
Watu saba wameketi mezani hotelini wakila chakula cha mchana, kila mmoja ana karama ya masaidiano
tofauti na mwingine. Na mtu wa nane akiwa katika kundi hilo. Mara, mtu wa nane anaigonga bilauri ya maji
kwa kiweko chake na kuisababisha idondoke sakafuni kwenye sementi na kuvunjika vipande vipande.
Mwitikio Kutokana Na Mguso Wa Karama Za Masaidiano.
Kila mmoja huonyesha mwitikio kulingana na karama ya masaidiano iliyomo ndani yake kama ifuatavyo;-
1. Mwenye karama ya masaidiano ya unabii. Atasema, “Nilijua kile kitakachotokea”
2. Mwenye karama ya masaidiano ya uhudumu/utumishi, atasema, “Tulia mimi nitakusaidia kusafisha”.
3. Mwenye karama ya masaidiano ya Ualimu atasema, “Kuna kitu cha kujifunza hapa, Kama ungeliiweka bilauri
hii sehemu nzuri,….
4. Mwenye karama ya masaidiano ya Kufariji/Kuhamasisha atamgeukia na kusema, “Usijisikie vibaya, hilo
halitatokea tena Mungu atafanikisha nyingine itapatikana tu.”
5. Mwenye Karama ya Utoaji atasema, “Usijali mimi nitalipa”.
6. Mwenye karama ya masaidiano ya Uongozi haraka atachukua nafasi katika jambo hilo akimwambia
mngojezi (weita) “ Lete ufagio na kizoleo cha takataka, kisha tuletee na bilauri nyingine ya maji.”
7. Mwenye karama ya masaidiano ya Kurehemu/Kuhurumia atasema, “Oh, hii ni mbaya sana, natumaini sasa unajisikia vizuri.
Kwa ufupi:
1. Kila mmoja analiona jambo kwa mtizamo tofauti kulingana na karama aliyojaliwa.
2. Anaonyesha mwitikio wa tofauti na mwingine kulingana na karama aliyojaliwa.
3. Hali hizi zote zimewekwa ili kutenda kazi moja kwa pamoja na kwa namna tofauti, zikitegemeana


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*