MUNGU HUMBARIKI MTU KUPITIA UTOAJI
📖👨🏻💻 *MUNGU HUMBARIKI MTU KUPITIA UTOAJI* 📖👨🏻💻
_Mwlm .Peter Francis_
*0679392829*
👉Ninamuomba Mungu akubariki na akufundishe zaidi kupitia ujumbe huu leo .
👉Je unapomtolea Mungu utapata faida gani ❓Jiulize hilo Swali kisha kwenye jibu hapa chini kuona faida za utoaji ambayo mojawapo ni kupata baraka
💒 7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Malaki 3 :7
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
Malaki 3 :8
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
Malaki 3 :9
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malaki 3 :10
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 3 :11
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 3 :12
👉Tunaona jinsi gani Mungu anambariki amtoleaye kwa uaminifu
Anamjaza kiuchumi anakuwa na maendeleo ya viwango vya juu sana.
👉Moja ya jambo analoliangalia sana Mungu katika utoaji ni fungu la kumi
📖FUNGU LA KUMI NI MOJA YA KUMI YA KAZI YA MIKONO YAKO
MFANO UMEFANYA KAZI UKALIPWA 10000 KWA SIKU
Moja ya kumi ya 10000 ni 1000 hyo utamtolea Mungu usipunguze maana utakuwa umemwibia Mungu
📖👨🏻💻 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malaki 3 :10
👉Mungu anakuahidi atakufungulia madirisha ya mbinguni
*MALAKI 3:10*
*HASARA ZA KUTOMTOLEA MUNGU*
📖👨🏻💻
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
Hagai 1 :9
10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.
Hagai 1 :10
11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.
Hagai 1 :11
UNAWEZA UKAMTOLEA MUNGU NA ASIKUBARIKI KWA SABABU HII ✍✍✍✍✍✍✍✍✍
📖👨🏻💻
8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
Mithali 15 :8
💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒
Maoni
Chapisha Maoni