RAFIKI MWEMA

πŸ’’ *RAFIKI MWEMA* πŸ’’



Mwlm. Peter Francis Masanja


0679392829.
.
https://peterfrancismasanja.blogspot.com



 _BWANA YESU ASIFIWE_


Karibu katika somo hili popote ulipo , neema ya Mungu itawale ndani yako ili Mungu akupandishe viwango vya juu sana .




πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» _UNAJIJUA JINSI ULIVYO_ ❓


3 Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?

Amosi 3 :3


πŸ‘‰Rafiki yangu leo nataka ujifunze kuwa asilimia kubwa ya marafiki hufanana tabia .


πŸ‘‰ Kama unatafta rafiki lazima ujiulize jinsi ulivyo wewe na kisha tafta rafiki kulingana na ulivyo wewe .


Siku zote msomi atataka marafiki wasomi


Mwasherati atataka marafiki washerati kwasababu anafanana nao tabia .


Aliyeokoka hutafuta marafiki waliookoka ili wafanane na kuelewana zaidi



Kijana aliyeokoka hawezi kwenda kwenye vijiwe vya vijana wanaojadili upotovu kila wakati




πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 63 Mimi ni mwenzao watu wote wakuchao, Na wale wayatiio mausia yako.

Zaburi 119 :63

64 Bwana, dunia imejaa fadhili zako, Unifundishe amri zako.

Zaburi 119 :64



πŸ‘‰ Ili Kijana uweze kufikia malengo yako usikubali kila mtu awe rafiki yako


πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.

Mithali 1 :10


πŸ‘‰ Kama kijana umeokoka na bado unamarafiki wabaya wazinzi ,waasherati walevi huwezi ukamwona Mungu


Amua kuwaacha kabisa leo.


πŸ‘‰ Dhambi inanguvu kuliko haki
Kwahiyo ukiambatana na waovu hata wewe utaitwa mwovu pia .


Achana na marafiki wabaya , wenye dharau , wenye mizaha , wanaofurahia matendo ya giza . Hata kama wameokoka ikiwa hawatembei nuruni jitenge nao.


πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Zaburi 1 :1

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Zaburi 1 :2

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Zaburi 1 :3

4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

Zaburi 1 :4

5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

Zaburi 1 :5

6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.

Zaburi 1 :6


πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» _HUKUZALIWA KWA BAHATI MBAYA_


Mungu alikuleta duniani umsikilize yeye na awe mshauri wako Wa kwanza


8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Zaburi 32 :8


πŸ‘‰ Mungu kabla ya kukuleta duniani alikuandalia marafiki wazuri na waanifu .


πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi 139 :14

15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi 139 :15

16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Zaburi 139 :16

17 Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
Zaburi 139 :17

18 Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe.

Zaburi 139 :18


πŸ‘‰ usijidharau wewe ni wa thamani sana usikubali marafiki wabaya wakuharie maono yako .


πŸ‘‰ Usitamani kufanana na mtu Fulani tamani tabia zako zimpendeze Mungu



πŸ“–πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» *AINA HIZI ZA MARAFIKI ZITAMANI SANA*


πŸ‘‰ Marafiki Wa rika ( peer friends)

Wawe wanaendana na jinsi ulivyo wewe kitabia


πŸ‘‰Marafiki wanaokuzidi umri , maarifa, ujuzi au fani yako ( Mentor friends)

πŸ“– 24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Mithali 18 :24

πŸ‘‰Angalia mfano wa hawa marafiki .


πŸ‘¬YAKOBO  NA LABANI


14 Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.
Mwanzo 29 :14

15 Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini?

Mwanzo 29 :15


πŸ‘¬YOSHUA  NA MUSA


Bwana akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania.

Kumbukumbu la Torati 31:14



πŸ‘¬TIMOTHEO NA PAULO



1 Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi.

Wafilipi 1 :1


πŸ‘¬PETRO NA YESU

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe.
Mathayo 26 :36

37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.
Mathayo 26 :37

38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.

Mathayo 26 :38


πŸ‘¬JE , WEWE UNAAMBATANA NA NANI NA ANAKUFUNDISHA NINI ?



TAFAKARI



KAMA UNATAKA UWE MTUMISHI WA MUNGU KUBALI KUWA KARUBU ZAIDI NA MTUMISHI WA MUNGU



πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Mungu akubariki sana

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*