SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU

SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU

SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU



SEHEMU YA NNE










Mwlm. PETER FRANCIS

0679392829

0744056901
francispeter424@gmail.com




BWANA YESU APEWE SIFA 


Karibu katika sehemu ya nne katika mwendelezo wa somo hili naamini Mungu atakufanikisha na kufungua macho yako ya kiroho ili akufanikishe kufikia viwango vya juu sana katika imani yako popote ulipo .Mungu kakusudia jambo jema sana katika maisha yako nami nakuombea mbele za Mungu ili akubariki zaidi katika maisha yako.


Basi karibu sana katika somo hili , na zifuatazo ni sababu zinazoweza kumfanya Mungu asikujibu maombi yako|:


  • KUOMBA KWA TAMAA ZA MOYO WAKO
" Hata mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya ,ili mvitumie kwa tamaa zenu"


YAKOBO 4:3,15





Katika maombi yatupasa kuomba mahitaji yetu kwa kuangalia tunataka tumfanyie nini MUNGU baada ya kutupatia tuyaombayo?

Je, tunaomba ili badae tukipata tutumie kwa tamaa zetu ili kutimiza matakwa ya miili yetu ?

Mungu pia anaangalia moyo wa mtu aombaye anaweza akaona ndani yako unamwomba kitu ili ukitumie kurahisisha dhambi katika maisha yako.
wengine huomba wapewe vitu ili wavitumie kunyanyasa, kukomesha, na kuwadhulumu na kuwadharau wengine.
Mungu anaweza akaona moyoni mwako kuna kitu unakiomba kumbe unawaza kukitumia kufanya uasi.
Kwahyo hawezi kukujibu haja ya moyo wako maana akikuangalia anasema huyu simpi hiki maana ataniasi .

  • KUWA NA UNAFIKI NDANI YAKO
Tena msalipo msiwe kama wanafiki ,kwa maana wao wanapenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi( makanisa) na njiani ili waonekane na watu .Amini nawaambia wamekwisha kupata dhawabu yao ,Bali wewe usalipo ingia katika chumba chako cha ndani,na ukiissha kufunga mlango wako ,usali mbele za baba yako aliye sirini,na baba yako aonaye sirini atakujaza

MATHAYO 6:5_6


Nenda mbele za Mungu umwombe haja za moyo wako naye atakujibu ,usijioneshe kwa watu ili uonekane kwamba nawewe unafanya maombi na unajua sana .Siyo kila sehemu unapaswa kusimama uombe huwezi kufanya maombi barabarani ili uonekane na watu kwanza ni dhambi na pia ni kelele ndyo maana Mungu anataka utafute eneo kwa ajili ya kusema naye juu ya shida zako. Mungu anachukizwa na wale waombao kwa kujionyesha na hatendi jambo ndani ya maisha yao.
Yesu mwenyewe alikuwa anaenda mlimani  ili kumwomba Mungu ,hili la kujionyesha limetoka wapi?


Naye alipokwisha kuwaga makutano,alipanda mlimani faraghani,kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni,alikuwako huko peke yake.

Kwahyo unapomwemba Mungu tafta mahali pa siri ili uongee na Mungu wako.Angalia mahali patulivu kabsa ni vizuri ufanyie chumbani kwako au kanisani .Kufikia hapo Mungu atakujibu maombi yako .


MUNGU AKUBARIKI SANA 


KARIBU SEHEMU YA TANO


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*