SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU
📖 *SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU* 📖
_SEHEMU YA TANO_
Mwlm. Peter Francis
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Karubu tena katika mwendelezo wa somo tuendelee kujifunza
Nakuombea kwa Mungu uweze kujifunza kitu hapa na roho wa Mungu akupe ujuzi kupitia somo hili .Amen
👉ZIFUATAZO NI SABABU ZINAZOWEZA KUFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU
📖👨🏻💻 _KUSHINDWA KUTUMIA MAMLAKA_
👉Mamlaka tunayo izungumzia hapa ni ya kiroho ambayo tumepewa na Mungu .
Watu wengi walijikuta hawaoni matokeo chanya ya Maombi yao kwa sababu walishindwa kuitumia mamlaka waliyopewa na Mungu
📖 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Luka 10 :19
👉Wengi walijikuta shetani anawanasa kwa kushindwa kutumia mamlaka vizuri .
👉Ukiitumia mamlaka uliyopewa na Mungu utayaona matendo makuu ya Mungu yanajidhihirisha kwako .
📖 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Marko 11 :23
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11 :24
👉 ukiitumia mamlaka ya kiroho uliyopewa na Mungu hata mapepo utayatoa na wagonjwa pia watapona kabsa .
📖 1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 10 :1
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Mathayo 10 :8
👉Ukiitumia vizuri mamlaka utaona mambo makuu maishani mwako yanatendeka
Hata wanaokuzunguka utawashangaza sana kwa jinsi Mungu anavyozidi kukutendea mema .
📖 wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka hii?
Luka 20:2
👉Ukiitumia mamlaka hata watu wataona jinsi Mungu anavyojidhihirisha kwako kupitia imani uliyonayo .
📖👨🏻💻 _KUACHA KUTUBU DHAMBI_
📖 8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
1 Yohana 1 :8
👉Mungu anataka tutubu dhambi zetu ili atusikie kuomba kwetu.
📖 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Isaya 1:18
👉 Mungu mwenyewe tunamkosea sana na tunamkasirisha sana kwahyo tunapomwendea lazima tutubu dhambi zetu bila toba tutakuwa mbali na Mungu
📖 1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
Isaya 59 :1
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Isaya 59 :2
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.
Isaya 59 :3
👉Tunaona jinsi gani Mungu anahitaji tutubu ili atujibu maombo yetu .
📖 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
2 Petro 3:9
👉Ahadi za Mungu ndani ya maisha yako zinahitaji toba ili zitimie maishani mwako .
✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍
Katibu tena katika sehemu ya sita .
MUNGU AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni