SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU

*SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU*
Sehemu ya kwanza:

 _SEHEMU YA PILI_


Mwlm.Peter Francis

0679392829


 *Bwana Yesu apewe sifa .



Nakukaribisha kwenya mwendelezo wa somo letu la Maombi katika jina la Baba , Mwana na Roho Mtakatifu.Amen.
.

πŸ‘‰Zifuatazo ni sababu zinazofanya maombi yako yakose majibu  :




πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» *KUTOKUTUMIA NENO LA MUNGU KATIKA MAOMBI*


πŸ‘‰ Inawezekana unaomba bila kuachilia neno la Mungu katika kile ukiombacho mbele za Mungu ndyo maana umekosa majibu .


πŸ‘‰ Kwanini umekosa majibu uliyoyatarajia Mungu atende jambo ndani yako ❓


Hii ni kwa sababu Mungu anaangalia moyoni mwako haoni neno kuhusu uombacho .


7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Yohana 15 :7

πŸ‘‰Jifunze kuachilia neno katika kile ukiombacho mbele za Mungu.

Utaniuliza utaliachiliaje neno ?

Basi nakupa mfano hapa chini kama ifuatavyo :


 *MFANO*

πŸ”₯ _Katika jina lenye uweza na nguvu kupita majina yote la Bwana Yesu Kristo wa Nazareth. Ninaangusha kila nguvu za giza zijiinuazo kinyume na elimu ya Mungu ,kama neno lako Mungu linavyosema :.

5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

2 Wakorintho 10 :5

Ninasimamia huu mstari ninaamuru kila kitu kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na fikira ijiinuazo kinyume na elimu ya Mungu naziteka zilitii jina la Yesu. Amen_


πŸ‘‰ Tambua kuwa Mungu analiangalia neno lake ndani yako ili atende jambo.


12 Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.

Yeremia 1 :12


πŸ‘‰ Mungu anatimiza jambo kwa kuangalia neno .


πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» *KUTOKUSAMEHE*


πŸ‘‰Msamaha ni kitu cha muhimu sana na ni njia pekee ambayo inaweza kukufanya ujibiwe Maombi yako mbele za Mungu .


25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11 :25


πŸ‘‰Kutokusamehe ni dhambi .


25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11 :25


πŸ‘‰ 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Mathayo 6 :14

15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6 :15



πŸ‘‰Mungu hawezi kukusamehe dhambi zako kama hujasamehe maana kutokusamehe ni dhambi


35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Mathayo 18 :35


πŸ‘‰Usiposamehe huwezi kupata baraka za Mungu

12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Mathayo 6 :12

πŸ‘‰Jiulize , je,unapomwambia Mungu akusamehe dhambi zako wewe umesamehe❓

Kama hujasamehe nawewe hatakusamehe kabsa .


Kwahiyo Mungu anataka usamehe wangine ili ajibu Maombi yako .



πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» *KUTOKUOMBA KATIKA MAPENZI YA MUNGU*


14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.


1 Yohana 5 :14

15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

1 Yohana 5 :15


πŸ‘‰ hakikisha kila uombacho na ufanuacho kifanye ukifuata mapenzi ya Mungu .

πŸ‘‰ Usiombe kitu kwa Mungu mfano : unaomba Mungu akupe utajiri lakini ndani yako unataka uutumie huo utajiri kunyanyasa wengine .Huwezi kujibiwa Maombi yako .


Unamwambia Mungu akupe utajiri ili watu  wakukome  huwezi kutendewa .


10 mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
Waefeso 5 :10

πŸ‘‰Hakikisha uombacho kipo sawasawa na mapenzi ya Mungu ili Maombi yako yajibiwe.



πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Mungu akubariki sana usikose sehemu ya tatu


21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Ayubu 22 :21

22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.

Ayubu 22 :22

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*