SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YAKOSE MAJIBU
_Mwlm.Peter Francis_
0679392829
*SEHEMU YA TATU*
_BWANA YESU ASIFIWE_
karibu katika mwendelezo wa darasa letu la maombi .
πLeo tutaangalia sababu nyingine zinazoweza kumfanya Mungu asikujibu maombi yako kama ifuatavyo:
π¨π»π» _UHUSIANO MBAYA NA WATU WENGINE_
πMoja ya vitu ambavyo Mungu vinaweza kumfanya asikujibu maombi yako ni hili suala la kuishi vizuri na watu yaani kuwa na amani na watu wote .
πIli Mungu akubariki anaangalia unaishije na watu wanaokuzunguka .
Ukiishi nao vibaya utakosa baraka kutoka kwa Mungu
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
πHuwezi kumwona Mungu akitenda jambo jipya katika maisha yako bila kuwa na amani na watu wote.
Maana utaomba lakini Mungu atakufungia milango yako ya baraka mpaka utakapo amua kutubu na kuishika kweli .
π« _UHUSIANO MBAYA WA MUME NA MKE_
uhusiano wa mke na mume unamfanya Mungu asisikie maombi ya wanandoa
πmwanaume akikosa uhusiano mzuri na mke wake maombi yake yanakosa majibu mbele za Mungu .
7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
1 Petro 3 :7
πHata mwanamke akikosa utii kwa mumewe ndoa haiwezi kubarikiwa na itakosa amani .
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
Wakolosai 3:18
Mungu anajibu maombi ya mwanamke amtiiye Mumewe na kudumu katika kumwombea .
π¨π©π§π§ _UHUSIANO MBAYA KATI YA WAZAZI NA WATOTO_
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
Waefeso 6 :1
2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
Waefeso 6 :2
3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
Waefeso 6 :3
πMungu anajibu maombi ya mtu mwenye uhusiano mzuri na wazazi wake kwanza
Mtoto mtiifu siku zote hupata baraka toka kwa wazazi kwanza na Mungu humjibu Maombi yake hujibiwa na Mungu .
πWapo watu waliwasahau wazazi wao na hawarudi nyumbani kuwasalimia , wamewadharau sana .Watu hawa wamejikuta hawana makao wanahangaika na matokeo yake wanaingia kwenye matatizo na vifungo vya kiroho .
Ndipo utagundua kuwa watu hawa wengi wao wanajaribu kila jambo wanapata hasara kwa sababu Mungu anakaa mbali nao.
πKama humpendi baba yako au mama yako unayemwona utampendaje Mungu usiyemwona❓
πWazazi pia wanapaswa kuishi vizuri na watoto wao
Huwezi kubarikiwa na Mungu kama huwapendi watoto wako
Mungu anataka uishi vizuri na watoto ili ajibu Maombi yako
Kila mtoto lazima umpe haki yake ya msingi ili ubarikiwe
Usioneshe upendeleo kwa kutaka kupenda baadhi ya watoto na wengine kutowajali
Utakosea sana na utapanda mbegu ya chuki
4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Waefeso 6 :4
π¨π»π» *UHUSIANO NA JIRANI YAKO*
πJirani yako ni mtu yeyote unayemfahamu .Kama mtakuwa na uhusiano mbaya na yeye Maombi yako yatakataliwa mbele za Mungu .
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
Mathayo 5 :23
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo 5 :24
πMungu anataka uwapende watu ili akujibu Maombi yako
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
2 Timotheo 3 :2
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
2 Timotheo 3 :3
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
2 Timotheo 3 :4
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
2 Timotheo 3 :5
π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»π¨π»π»
*HITIMISHO*
ISHI VIZURI NA WATU
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Wakolosai 4:6
Ni mimi
MWL.Peter Francis
0679392829
_USIKOSE SEHEMU YA NNE_
wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
1 Wakorintho 10:4
Maoni
Chapisha Maoni