AINA ZA MAOMBI
AINA ZA MAOMBI
NA
Mr
ZAWADI NGAILO
Sikonge
TABORA
⇒Inawezekana si Mara nyingi
umesikia habari zinazohusiana na Maombi
Umesoma Maandiko mbalimbali yanayohusu Maombi
Na umefundishwa masomo mbali mbali kuhusu Maombi
Lakini na Leo pia napenda tukumbushane pia kuhusu kipengele
hiki
Tunapozungumzia habari za Maombi
Tunaweza kumanisha vitu vingi na maana tofauti tofauti
kulingana na Mazingira tofauti tofauti
*Maombi* inaweza kuwa ni njia ya ...
Msaada wa kusaidiwa ..
Muunganiko wa kitu Fulani katika Eneo Fulani .
Ninaposema ni njia ya
⇒Maana yake Maombi yanaweza kutumika kama njia ya
kukuunganisha wewe ,Kuinganisha nafsi yako ,Roho yako na Eneo Fulani /Na kitu
au MTU Fulani ..
Maombi ni njia ya kuunganisha /kutengeneza daraja kati yako
wewe na Mungu pia
1 Timotheo 2:1 1 Basi, kabla ya mambo
yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya
watu wote;
Mtume Paulo anasema Basi (Yatosha ) kabla ya Mambo
yote nataka dua ,na sala na maombezi na Shukrani zifanyike kwa ajili ya watu
wote ...
Katika Maombi au tunapoomba siku zote tutambue kuna
vitu hivyo hapo vinne vya Muhimu
⇒Dua/Supplication s
⇒Sala /Prayers
⇒Maombezi /intercessions
Na
⇒Shukrani /Thanksgiving
Dua
Kwenye Dua tunamuuliza Mungu kuhusu mahitaji yetu /Asking
God na hii inapaswa kuambatana na Unyenyekevu ndani yake..
Unapokuwa unamuuliza Mungu maana yake unatafuta
Msaada wake kwa ajili ya Hitaji ulilonalo
Baada ya kutafuta msaada unaingia kwenye mawasiliano
/kuwasiliana naye kwa Njia ya Sala
Unapoingia kwenye kuwasiliana utaunganishwa moja kwa
moja na Mungu ukiwa unawasiliana naye
Maombezi
Maombezi ni kitendo cha kupeleka mahitaji kwa Mungu
/kuwasiliana na Mungu kwa niamba ya MTU mwingine ..
Unapowasiliana na Mungu moja kwa moja mwenyewe au kwa
niaba ya MTU mwingine tambua kuna mambo ambayo Mungu atafanya ambayo
yatakulazimu
Shukrani
Shukrani ni Maombi kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa
kukutendea ulichokiomba
AINA ZA MAOMBI
⇛Maombi yenye IMANI ..
Maombi yote au Dua ,Sala unayompelekea Mungu au kumfanyia
Mungu ni lazima yaambatane na IMANI ndani yake ..
IMANI ndio itakayomuokoa MTU atoke au utoke kati hali
/mazingira ya aina yoyote ..
*Yakobo 5:15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa
mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa....
Kinachomuokoa MTU sio kuomba tu ili mradi isipokuwa *Kuomba
kwa IMANI*
Nikupe mfano huu wa kutoka kitabu cha Marko
9:23 23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.
Ukisoma kabla huu mstari hapo huu Huyu ni Yesu
mwenyewe anamwambia MTU mmoja aliyeletwa na Pepo Bubu
Kwa mazingira ya kawaida watu wa mahali hapo hawakuamini
kuwa Pepo litatoka
Lakini Yesu anasema *"Ukiweza! yote yanawezekana kwake
aaminiye*
Kumbe IMANI Na kuamini ni kitu cha msingi na
Yakobo anasema na kule kuomba kwa IMANI kutamwokoa mgonjwa yule .
Hapa Maombi yametokelewa kwa IMANI kwa mgonjwa ..
Akiulizwa Mungu kumponya
Tunapoomba tunapaswa kuamini nguvu na Uzuri uliopo ndani ya
Mungu ( Mk 9:23)
⇛Maombi ya Mapatano / Kuwa wa moja
*Matendo 1:14 Hawa
wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na
Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
*Matendo 2:42 Wakawa wakidumu katika
fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika
kusali.Maisha ya Waumini*
Maombi haya ni kuungana pamoja na kuomba kwa
pamoja
Mnajitoa kwa Pamoja kwa ajili ya kuombea jambo Fulani
Haya *maombi yanatuhamasisha na sisi kuomba Na wengine kwa
Pamoja*
⇛Maombi ya kumwomba Mungu
kuhusu mahitaji yetu
*Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo
lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja
zenu na zijulikane na Mungu.*
Njia mojawapo ya Ushindi wetu ni kupigana vita
ya Kiroho "Kuomba kila wakati katika Roho na Kweli
Waefeso 6:18 kwa
sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na
kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Maombi ya Shukrani
Rejea pia wafilipi 4:6..
Maombi haya pia yanapatikana pia Zaburi mbali mbali
⇛Maombi ya kuabudu/Kumfanyia Mungu ibada
Haya ni sawa na ya Shukrani isipokuwa tofauti ya Maombi
haya yanalenga kuonyesha Mungu ni nani?,Shukrani na Yaliyofanywa na Mungu
*Matendo 13:2 Basi hawa walipokuwa
wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba
na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.*
*3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao
juu yao, wakawaacha waende zao.*
⇛Maombi ya kujiweka tayari
kutimiza mapenzi ya Mungu ..
Haya yalifanyika na Yesu mwenyewe kabla ya kusulubiwa
*Mathayo 26:39 Akaendelea mbele kidogo,
akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki
kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.*
⇛Maombi ya maombezi /Sala ya maombezi
Haya yanahusu kuwaombea wengine
Ukisoma YOHANA 17 mlango wote utaona jinsi
Yesu alivyoomba kwa ajili ya wanafunzi /mitume wake na Waumini wote.
⇛ Maombi ya kuombea maadui zetu (
Kuwaombea mema)
Sisi kama Kanisa tunazingungukwa na Maadui wengi sana
pamoja na hayo inatupasa kuomba kwa ajili yao pia na hatupaswi kuwaombea mabaya
bali tunapaswa kuwaombea mema ..
Msaada zaidi soma
Zaburi 7 ,55 na 69
Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha /anatufundisha tuwaombee
na kuwabariki maadui zetu
Mathayo 5:44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui
zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana
yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio
haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu
gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la
ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa
mbinguni alivyo mkamilifu.
⇛Maombi ya kutufungua
kwenye Vifungo mbali mbali
Haya ni maombi ya kututoa katika vifungo
tulivyonavyo au mambo yasiyowezekana mbele ya macho yetu ..
Zaburi 69:1
Ee Mungu, uniokoe,Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
2 Ninazama katika matope mengi,Pasipowezekana
kusimama.Nimefika penye maji ya vilindi,Mkondo wa maji unanigharikisha.
3 Nimechoka kwa kulia kwangu,Koo yangu imekauka.Macho yangu
yamedhoofuKwa kumngoja Mungu wangu.
⇛Maombi ya kuleta Ulinzi katika MAISHA yetu.
Haya ni kwa ajili ya kutulinda sisi Na vyote
tulivyo navyo
Yeremia 1:18
Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na
nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na
juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.
*19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi
nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.*
ZIPO AINA NYINGI KWA LEO NITAISHIA HIZI CHACHE ...
MWISHO NIKUPE BAADHI YA VIZUIZI VYA MAOMBI
1⃣
Dhambi
Dhambi inafanya maombi yetu yasisikilizwe na Mungu
wetu.
Isaya 59:1
Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze
kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
*2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu,
na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.*
2⃣
Kuomba vibaya
Yakobo 4:3
Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya,
ili mvitumie kwa tamaa zenu.
3⃣ Kutokuwa na IMANI
*1Timotheo 1:19 uwe mwenye imani na dhamiri
njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.*
4⃣
Kutokushukuru
LUKA 17:11 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu,
alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu
kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa,
uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa
makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku
akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye
alikuwa Msamaria.
17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale
kenda wa wapi?
Kutokumshukuru Mungu baada ya kukutendea ya mwanzo
inaweza kusabisha usijibiwe yajayo ..
Hitimisho
Maombi ni agizo la Mungu ndio maana anasema *Mathayo
26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia Majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni
dhaifu.*
Hivyo tukeshe katika maombi siku zote
Na Biblia inasema tuombe katika Roho na kweli
Maombi ni mawasiliano au majibizano na Mungu ambayo
hayapaswi Kuwa na kikomo
1Thesalonike 5:16-18 ,Tukue katika UPENDO wa Yesu Kristo na tutakuwa hamu ya
kuzungumza naye Daima .
*Bwana ninakushukuru kwa kunipa kibali kusema na Kanisa
lako mahali hapa
Ahsante kwa kusema na Roho zetu ,nafsi zetu ns mioyo yetu
na MAISHA yetu pia .
Endelea Bwana kutuhudumia mchana na usiku ,Tuhudumie kwa
NENO lako daima ,tufundishe na kutuonya na k
NENO lako zaidi ya ya yote tujalie kuitumia NEEMA hii
uliyotupa kwa ajili ya kukutumikia na kuutafuta USO wako
Ongoza MAISHA yetu ,njia zetu na mipango yetu
Tawala fikra zetu ,fahamu zetu na mawazo yetu ili Bwana
tuyatende mapenzi yako daima .
Tunajikabidhi mikononi mwako tembea nasi siku zote na
kuishi pamoja nasi .
MUNGU AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni