FAIDA YA KUFUNGA NA KUOMBA

*📖👨🏻‍💻HAKIKA UKIFUNGA UTAPATA AFYA KIROHO*

💒  💒💒💒💒💒💒💒💒

Kufunga ni hali ya kuutiisha mwili kwa kuunyima chakula, vinywaji, malazi mazuri, mavazi yakupendeza na vitu  vya kuvutia

Maombi ya kufunga yanaanza masaa 6 kwa watoto ,masaa 12,24, 72 yaani siku tatu, siku 5 , siku 7 ,21 na 40

Maombi ya kufunga ni mbinu au style ya juu ya kuomba ambayo ni ishara ya kumaanisha unachoomba

👉 Bwana Yesu anasema hali hii haitoki bali kwa kufunga na kuomba

👉 Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.

2 Mambo ya Nyakati 20:3
Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.

Esta 4:3
Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.

Zaburi 109:24
Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

Isaya 58:3
Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya Bwana yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya Bwana, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda, watokao katika miji yao.

Yeremia 36:6
[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

Mathayo 17:21

👉Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

Esta 4:16
Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.

Yona 1:17

👉 Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani.

Mathayo 15:32

📖 Mara ya kwanza nafunga maombi haya nilijisikia nguvu ya ajabu na mwepesi kimwili

Kuna mtu aliniangalia machoni akasema siku niliposimama madhabahuni macho yalikuwa kama ya simba ni hapo ambapo hakuna pepo linahimili kukuangalia machoni

🚶🏻‍♂ Kama unataka kuhama kutoka level moja ya huduma kwenda nyingine fanya mambo 3

1. Tunza utakatifu

2. Soma neno kwa tafakari na msaada wa Roho mtakatifu. Roho mt akusaidie kupata tafsiri ya mstari ujumbe wako ndani ya Biblia kwanza kisha nje kwenye maisha ya kawaida

3. Ongeza Muda wa maombi na masaa ya ukimya nje ya uyapendayo

Mungu awabariki sana

Pastor peter Sponga
Bahi Dodoma Tz

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*