FAIDA YA KUOMBA KWA KUTUMIA NENO

FAIDA YA KULITUMIA NENO KWENYE MAOMBI







[1/24, 22:15] Mr Zawad Ngailo:

Maombi mazuri pia kwetu ni kutumia NENO la Mungu pia ili kumuonyesha Mungu kitu kilichopo ndani yetu ..

Mfano

Zaburi  107:20 Hulituma neno lake, huwaponya,Huwatoa katika maangamizo yao.

    Ukimwambia nalituma NENO la ko likawaokeo kumbuka atakwenda kufanya kile unenacho .....

Nguvu ya Maombi inatoka kwa Mungu mwenyewe

Kwenye kusima cha haki

Lakini tunapotuma maombi ahadi zake zinajieleza Kutoka moyoni.

: Tunajua tunakubaliana na Mungu kwa kutumia NENO lake katika (Sala na Maombi).

Kadri tunavyo kumbuka maneno ya kwenye Biblia ..
Yatakuwa sehemu yetu


: Ukweli tunaojifunza utaingia kwenye   fahamu zetu /fikra zetu ( Mind) tunapokuwa tunaomba
[

: Na majibu tunayoyatafuta tunayapokea

Tunaposhindwa kuomba tukijua kutumia maandiko ( NENO la Mungu ) tutaongeza maneno ya kuomba

Kama hujatambua IPO siri kubwa mno katika kulifahamu kwa wingi NENO la Mungu na kuomba sana

Msomaji mzuri wa NENO ni mwombaji mzuri pia

Mvivu wa NENO ni mvivu wa kuomba pia

Kiwango chako cha kuomba kinatokana na kiwango cha nguvu ya NENO la Mungu iliyojaa ndani yako .

: Ukisoma kitabu cha Zaburi Mara nyingi utajifunza vitu vingi vinavyohusu maombi

Kuna wakati nilipokuwa naanza kuzisoma

Kuna muda nilipokuwa naanza kuzisoma sikuwa na hamu ya kuomba

Nikianza kusoma tu automatic najikuta naingia kuomba ghafla

Kuna wakati nikiwa na Furaha unajikuta umeanza kutoa machozi ghafla .n.k

Zaburi nyingi zimebeba mawazo yetu kwenye mfumo wa Maneno




: YOHANA 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;
2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
6 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.
8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;
10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
24 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.
26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

✍Yesu Kristo ametupa mfano mzuri kupitia mlango  huo 👆👆👆Juu..

Ametuandikia sala /maombi marefu ila nasi yakiwa ni ya kujitukuza na Kumtukuza Mungu pia kwa kazi aliyoifanya duniani

Pia na kuuombea Ulimwengu wote.

✍Jambo LA kwanza kuonekana ni

Umoja wa Roho uliopo katika Ya Yesu Kristo na Mungu ( Baba yake)

Alianza kwa kusema Baba Mtukuze Mwanao ,SAA imekwisha kufika .

Yesu hakumwambia Baba yake kila kitu ,Asichokijus  Bali alimshukuru na kumheshimu kwa kuwa walikuwa pamoja siku zote.

Alitumia muda mwingi kuomba kwa bidii kwa maana alitambua Moyo wa Baba yake.

Hii ndio sala ya mwenye haki niliyokwambia Jana

Unatakiwa kuufahamu moyo wa Mungu kisha omba sawa sawa na mapenzi yake

Ikiwa na kwa kutumia maneno yako /yetu au yaliyoandikwa  ndani ya Biblia .
Sala ya Mwenye haki /maombi ya mwenye haki ni .

*Yale yanayotoka kwenye Moyo na kuyatafuta mapenzi ya Mungu*

: Kuomba kwa kutumia NENO LA MUNGU ni kitendo cha kumweleza Mungu kwamba tunahitaji kutembea katika njia sahihi kwa kujua tunaomba itupasavyo

*Waefeso 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.*

Mfano Kwa NENO hili Unaweza ukamwomba Mungu kwa maneno yafuatayo

*Baba Leo nimesulubiwa na Kristo,Si Mimi niliyekuwa tangu mwanzo ,Yesu Kristo anaishi ndani yangu ,MAISHA ninayoishi Leo ,nitaishi kwa IMANI ndani ya Mwanao Yesu Kristo ,Aliyenipenda Mimi na kujitoa kwa ajili yangu .*

Kwa njia hii tunakuwa tUmeugusa moyo wa Mungu na kuyafikia malengo yetu

WATHESALONIKE 5;10          23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
[1/25, 07:04] Mr Zawad Ngailo: Hakuna kitu cha kustaajibisha katika neno ama cha ajabu katika Neno lakini tunaweza kujua tunaomba ndani ya Mapenzi ya Mungu tunapotumia Neno kama kiongozi chetu

Unapotumia neno au Andiko lolote kwenye maombi  

Unatakiwa kuwa makini maana si kila andiko litakufaa kwenye matumizi ya maombi na hali yako .
Kwa mfano

Mungu alimuahidi Solomon /Suleiman

Mali ,Utajiri  na Utukufu

2 Nyakati 1:11 Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
12 basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.

✍Hii ilikuwa ni ahadi ya Suleiman

Ahadi zetu pia kwetu kutoka kwa MUNGU zinatofautiana

Na zingine zinaendana ndio maana hatuwezi kulazimisha kutumia Ahadi ya Solomon /Suleiman
Au neno la hapo juu lazima tutafute mengine pia

Kuna wakati Mungu anaweza kukupa mstari mwenyewe binafsi .
Huo mstari ndio unaweza kukuongoza kusimamia maombi yako na kila unachokifanya. ..

Kama tutatumia kila   Neno kwenye kuomba kama linatufaa moja kwa moja hili litatupa shida sana

Mfano hili

*1 Sam 15:3 Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.*

Kwa hiyo kabla hujalitumia Neno angaliw kilichopo ndani yake kwanza kisha litumie

Ili lisikuletee matunda mabaya mbele zako .

Mungu awabariki nyote  nawatakia siku njema

Kwa Ushauri na maswali

Info @

What's up

No.
+255 762 450 772

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*