FAIDA YA KUOMBA TOBA

IJUE FAIDA YA TOBA KABLA YA MAOMBO






[1/24, 21:44] Mr Zawad Ngailo:


Yakobo  5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

1Yohana 5:14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.


Biblia inasema Ungameni dhambi zetu ninyi kwa ninyi na kuombeana ,Mpate kuponywa

Mpendwa katika Kristo tunaishi katika hali ya dhambi na tumetenda dhambi machoni pa Mungu na ndio maana anataka tuungame /Tutubu dhambi zetu sisi kwa sisi .

✍ Kundi hili linaitwa Darasa la Maombi

Darasa ni mahali pa kujifunzia ..

Nini tunachojifunza hapa ni kwa habari za Maombi

Kumbuka  Maombi siku zote ni lazima kwetu sote

Maombi si jambo la hiari Bali ni la lazima

Kila MTU ni lazima aombe

Na katika kuomba ili Mungu akujibu lazima ufuate kanuni na taratibu baadhi ili uweze kusikilizwa na Mungu
.

Si kila Maombi unayoyaomba yanaweza kusikika machoni pa Mungu ..

Kusukilizwa kwa Maombi yako itategemea msingi ulioujenga kabla ya kuingia kwenye Maombi yak

: ✍Kabla ya kuomba   hakikisha unatubu kwanza /unaungama dhambi zako kwanza kabla ya chochote

Unajitakasa

✍Kisha linafuata jambo lingine la Kuombeana

Huwezi kusima kuomba pasipo kujitakasa kwanza

Huwezi kumwombea MTU au kujiombea pasipo kujitakasa kwanza  ✍Baada ya kuombeana kuna kuponywa

Ukisha tubu na kuungama ,ukaingia kwenye kuombeana kinachofuata ni kuponywa

Mungu hawezi kukuponya au kumponya unayemuombea  ikiwa haatatubu kwa ajili yake ..

una wakati unaweza kusimama kuombea Mgonjwa apone lakini inashindikana kwa sababu hujatubu kwa ajili yake...

Uponyaji pia hawezekani kwa MTU asiye na haki

Bali unawezekana kwa mwenye haki .

Mwenye haki ni yule aliyejitakasa

Amejikamilisha kuzaa matunda mema /Amejikamalisha kutimiza mahitaji tarajiwa

Unaweza kusimama kuwaombea ndugu zako wafunguliwe lakini ikashindikana na inafikia hatua unakata tamaa kinachotakiwa beba Mzigo kwa ajili yao kisha ingia kutubu kwa ajili yao

Maombi ya waliojitakasa /tubu yanafaa sana mbele za Mungu ..

Kuomba kwa haki pia haitoshi pasipo kuomba kwa bidii

Ili ujibiwe usiombe kwa ulegevu au ili mradi umeomba *Omba kwa bidii*

: Huku ukimpelekea Mungu hoja zenye nguvu ..na kufanya mapatano naye .

Unapoomba kwa bidii usiwe na hofu kuwa na ujasiri ..

Kisha Omba sawa sawa na mapenzi ya   Mungu naye atakusikia

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*