KUIJENGA IMANI
.*πKUIJENGA IMANI π*
MWL.Peter Francis Masanja
ππ 2 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu;
1 Wathesalonike 3 :2
ππΌkuana wakati haitoshi kukaa peke yako na kuyatafakari maandiko
Hii inakulazimu ujifunze kwa walio juu zaidi yako ili imani yako izidi kukua zaidi
ππΌIpo faida kubwa kutaka kujifunza zaidi ili ukue zaidi kiimani
ZIFUATAZO NI FAIDA AMBAZO LEO NATAKA TUZIONE
πKUKUZA UWEZO WA KUMTAFAKARI MUNGU
πKUONGEZA KIWANGO CHA IMANI
π Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
Luka 17:5
ππΌ Kumbuka hili jambo , ili imani ijengeke ndani yako lazima uondoe mashaka ndani yako kwanza
π 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Marko 11 :23
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11 :24
ππΌIli imani ijengeke ndani yako epuka kusikia mafundisho yoyote yatakayokufanya uiache imani yako
π 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
Matendo ya Mitume 13 :8
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
Matendo ya Mitume 13 :9
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
Matendo ya Mitume 13 :10
11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.
Matendo ya Mitume 13 :11
12 Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Matendo ya Mitume 13 :12
ππΌepuka mafundisho yoyote yenye asili ya kuzimu yanayolenga kukuangusha kiroho
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni