UMUHIMU WA MAOMBI YA KILA SIKU
[1/26, 22:22] Mr Zawad Ngailo:
*UMUHIMU WA MAOMBI YA KILA SIKU*
Mpendwa msomaji
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikuletea mfululizo wa masomo kuhusu Maombi na Leo nakuletea ujumbe mfupi unaozungumzia umuhimu wa Maombi ya kila siku.
Maombi ni njia nzuri ya kuwasiliana na Mungu .
Ni gari ya kila siku inayobeba majibizano na mmoja aliyetuumba sisi .
Umuhimu wa Maombi ya kila siku hatuwezi kuuzidisha kwa kiwango cha ziada wala kukadiriwa .
Ni muhimu na Biblia ndio maana inatuonyesha zaidi ya 200 Umuhimu wa Maombi
✍Maombi ya kila siku yanatupa nafasi ya kushirikishana vitu vyote vinavyohusu MAISHA yetu na Mungu
✍Yanatupa nafasi ya kuelezea uzuri wa matendo aliyotutendea
✍Yanatupa nafasi ya kutubu dhambi zetu na kuomba msaada ili kuepukana na dhambi
✍Ni kitendo cha kumwabudu na kumtii Mungu
✍Ni kitendo cha kumshukuru Mungu kwa kuyaongoza MAISHA yetu
1⃣Kutupa nafasi ya kubadilishana vitu vinavyohusu maisha yetu
Msingi wa Maisha unabadiliki kila siku ,mambo yetu ,mipango yetu inaweza kubalika kutoka kwenye hali nzuri kwenda mbaya kwa muda mfupi sana
Lakini Mungu bado anatuwazia mema na kutufundisha
Yeremia 33:3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Mungu anataka tumuite ili aweze kujibu Maombi yetu
Na anata kushirikiana nasi baraka tusizoweza kuzifikia pasipo kumuita kwa Maombi
Anasema pia
Katika *Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.*
✍Tumkaribie Mungu ili atukaribie nasi ,Tujitakase mikono sisi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yetu .
Mungu anahitaji tusogee karibu yake muda wote.
2⃣Kutupa nafasi ya kuelezea uzuri wa Mungu
Sio siri kwamba sisi tunatakiwa kumpa Mungu Shukrani kwa vitu alivyotutupa na alivyofanya
Anafanya kwa niaba yetu
Uzuri wake na wema wake na ukarimu wake vitambulike kuwa msingi wetu .
: 1Nyakati 16:34 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3⃣Kwenye kutubu dhambi
*Zaburi 32:5 Nalikujulisha dhambi yangu,Wala sikuuficha upotovu wangu.Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Mwambie Mungu anachokijua na Fanya hivyo kila siku .
4⃣Kitendo cha kumwabudu na kumtii Mungu
1Thesalonike 5:16 Furahini siku zote;
17 ombeni bila kukoma;
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Muda wote kuwa na furaha pia mshukuru Mungu kwa kila jambo na mazingira yote ,Kwa kuwa yote ni mapenzi yake kwa ajili yako
5⃣Kutuongoza /Kuongoza MAISHA yetu
Mungu wetu ni huru,Hakina kisicho tokea pasipo yeye kujua .
Isaya 46:9 kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;
10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Maoni
Chapisha Maoni