URAFIKI UCHUMBA NA NDOA
*👫URAFIKI , UCHUMBA NA NDOA* 💍
MWL. Peter Francis Masanja
francispeter424@gmail.com
👉🏼Hatua ya kwanza katika
mahusiano ni
1⃣ URAFIKI
📖Katika urafiki kila mtu atataka kumfahamu mwenzake
👉🏼Anapenda nini
👉🏼Anachukia nini
👉🏼Hali yake ya kiroho ikoje
🅰 Ameimarika
🅱Hajaimarika
👉🏼Anaishi wapi
👉🏼Ana wazazi
👉🏼Anamchumba
👉🏼 Umri wake
👉🏼 Elimu yake
👉🏼 Anajishughulisha na nini
HAYA NI MASWALI YA KUULIZANA KIPINDI CHA URAFIKI
📖Kipindi cha urafiki ndicho kipindi cha kumsoma mwenzako kabla ya kufanya maamuzi ya kumwambia ukweli unampenda na unatamani muingie hatua ya pili ya mahusiano
Ambayo ni
👉🏼UCHUMBA
📖Kijana ukiruka hatua ya kwanza ya mahusiano ukakimbilia ya pili utaacha wengi sana
📖Usiharakie kisa umeona sura tu ukaamua kuanzisha uchumba
Mfanye rafiki kwanza ili upate nafasi ya kumfahamu zaidi
Ukifanya hivyo utapata mke mwema kabisa.
📖 Ukishamfahamu tabia na mwenendo wake sasa unaweza kuingia hatua ya pili ya mahusiano , yaani UCHUMBA
📖 Naongezea katika kipindi cha urafiki
👉🏼 mjue anavaaje akiwa kanisani na mtaani
🅰Anavaa nguo zisizomstiri
Je unapenda kumuoa mtu wa namna hiyo ❓
🅱 Jitahidi ujue aina ya marafiki zake
Ukishajiridhisha ingia hatua ya pili
👇👇👇👇👇👇👇
2⃣UCHUMBA
Katika uchumba unatakiwa uzingatie yafuatayo :
📖📖📖📖📖📖📖🖍
HATUA YA PILI YA MAHUSIANO*
📖UCHUMBA
Uchumba ni nini ❓
📖Uchumba ni makubaliano ya hiari ya watu wawili wanaotarajia kuishi pamoja kama mke na mume .
📖 Ndani ya uchumba kuna neno hiari.Hiari maana yake bila kulazimishwa
📖 Uchumba siyo ndoa
📖Hivyo msifanye mambo ya wanandoa kabla ya ndoa
📖KANUNI ZA UCHUMBA
👉🏼Zingatieni utakatifu
🅰 Msizini
👉🏼zungatieni kuwa tendo la ndoa ni kwa wanandoa tu
📖🖍 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 22:3
Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 27:12
📖Nimekupa hayo maandiko ujue kuwa ukiona ubaya usilazimishe usije ukaendelea ukaumia
📖Kwa tamaa za mwili kila mwanaume anafaa kuwa mume
Lakini kwa kuangalia kanuni za Mungu siyo kila mwanaume anakufaa haijalishi ameokoka 📖📖📖📖📖📖
📖 Kama nilivyosema mwanzoni kuwa uchumba ni jambo la kujichunga sana ili msiende kinyume na mpango wa Mungu
📖HASARA ZA KULALA PAMOJA ( KUJUANA KIMWILI KABLA YA NDOA
1⃣ Binti lazima utachukiwa NA kuonwa mchafu
📖🖍 14 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.
2 Samweli 13 :14
15 Kisha Amnoni
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.
2 Samweli 13 :15
📖Mwone Tamari alipokubali kulala na Amnoni alichukiwa sana
📖🖍 8 Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.
Maombolezo 1 :8
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
9 Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, Bwana, teso langu; Maana huyo adui amejitukuza.
Maombolezo 1 :9
10 Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamaniko yake yote; Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
Maombolezo 1 :10
ASOMAYE NA AJIFUNZE
⛪⛪⛪⛪⛪⛪⛪⛪
Good, stay blessed
JibuFuta