HASARA YA KUSHINDWA KUFANYIKA KIELELEZO MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU πŸ’»

πŸ’»HASARA YA KUSHINDWA KUFANYIKA KIELELEZO MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU πŸ’»





 πŸ’»πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?

1 Petro 4 :17


 πŸ‘‰ Mungu anapotaka kulihukumu kanisa huanza na viongozi kwanza


: πŸ‘‰Kama viongozi wanaowaongoza ni waovu kanisa linapata shida sana


 πŸ‘‰Kiongozi, awe mchungaji , mwalimu , nabii , mtume au mwinjilist  akiwa anafanya uovu kuna hatari sana katika kanisa la Mungu


 πŸ‘‰Inafikia hatua hata tunaowaongoza hawapendezwi na yale tuyatendayo


πŸ‘‰Tumekosa kuwa vielelezo ( mfano wa kuigwa )


πŸ‘‰ZIFUATAZO NI HATARI ZA KUSHINDWA KUFANYIKA KIELELEZO


*1⃣KUKOSESHA WATU WA MUNGU*_


πŸ’»πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 22 Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.
1 Samweli 2 :22

23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote.
1 Samweli 2 :23

24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana.
1 Samweli 2 :24

25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.

1 Samweli 2 :25



πŸ‘‰Moja hasara ya kushindwa kufanyika kielelezo ni kuwakosesha wengine kwa kufuata uovu wa kiongozi wao .



πŸ’»πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 16 Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.

Isaya 9 :16


πŸ‘‰Kama kiongozi anafurahia maisha ya dhambi na vijana pia watayafrahia tu kuishi hayo maisha



πŸ‘‰ Ukiwaonya watakwambia mbona mchungaji anafanya


*2⃣KUWAFANYA WATU WASITIMIZE MAAGIZO YA MUNGU*_


πŸ’»πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 2 Simoni Petro, na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja.
Yohana 21 :2

3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
Yohana 21 :3


πŸ‘‰Kiongozi anaposhindwa kutimiza maagizo na wengine pia wanatufuata_*


3⃣ JINA LA MUNGU LINATUKANWA*_


πŸ‘‰Jina la Mungu linatukanwa kwa sababu ya watumishi wa Mungu


πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’»πŸ’» 24 Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.
Warumi 2 :24

25 Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

Warumi 2 :25


πŸ‘‰Kwa maana hii hata mtu aliyeokoka akiwa mtenda maovu , kuokoka kwake hakumsaidii

πŸ‘‰ Maana hii ni kwamba huwezi kumwambia mtu aokoke kama wewe unaishi maisha ya kufumaniwa na wake za watu , au mwasherati, mwongo, mwizi, msengenyaji n.k


πŸ‘‰ Ukimwendea ambaye hajaokoka umwambie aokoke atakujibu siokoki kwa sababu unajifanya umeokoka .


πŸ‘‰Hii ndyo maana ya jina la BWANA kutukanwa pale mtu anaposhindwa kufanyika kielelezo .


*4⃣ KUWAFUNGIA WATU KUUONA UFALME WA MUNGU*_


πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’»πŸ’» 13 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.
Mathayo 23 :13


πŸ‘‰ Sisi viongozi tunaposhindwa kufanyika kielelezo tunawafungia watu kuuona ufalme wa Mungu
Ufalme ambao hata sisi hatutauona kama tukishindwa kufanyika vielelezo


 πŸ‘‰ Kiongozi akishindwa kuwa kielelezo hasara kubwa ni kutokuuingia ufalme wa mbinguni


 πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’»πŸ’» 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 7 :21

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Mathayo 7 :22

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Mathayo 7 :23


: πŸ‘‰ Kiongozi akishindwa kufanyika kielelezo akauelekea uovu hawezi kuuingia ufalme wa mbinguni

πŸ‘‰Kwa maana hii basi nataka ujifunze kuwa miujiza na karama ya uponyaji siyo tiketi ya kuuingia ufalme w



πŸ‘‰Ili tuingie kwenye ufalme wa mbinguni tunahitaji utakatifu


πŸ’»πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’» 31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
Mathayo 25 :31

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
Mathayo 25 :32

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
Mathayo 25 :33

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
Mathayo 25 :34

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
Mathayo 25 :35

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
Mathayo 25 :36

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
Mathayo 25 :37

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
Mathayo 25 :38

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
Mathayo 25 :39

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Mathayo 25 :40

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Mathayo 25 :41

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
Mathayo 25 :42

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
Mathayo 25 :43

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
Mathayo 25 :44

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Mathayo 25 :45

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Mathayo 25 :46

: Yesu atakaporudi atahukumu anataka akute watakatifu
viongozi na wale tuwaongozao tunapaswa kuwa vielelezo

 πŸ‘‰Ukiwa kielelezo uchumi wako utakua


πŸ‘‰ukiwa kilelezo ni rahisi sana kumwambia mtu aokoke na kukubali


πŸ‘‰unapofanyika kielelezo wewe kama kiongozi ni rahisi sana kukemea uovu kanisani kwako na watu wakaelewa

: πŸ‘‰Lakini kiongozi ukikosa kuwa kielelezo maana yake ndani ya kanisa una mahawara huwezi kuheshimika na huwezi waambia watu waache uzinzi kama humo kanisani una watu wako unafanya nao


*πŸ’» HITIMISHO πŸ’»*


πŸ‘‰Mbiguni hatuingii kwa kuwa tunafanya matendo ya miujiza au unabii

Mbinguni tunaingia kwa utakatifu .


: πŸ‘¨πŸ»‍πŸ’»πŸ’» 13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mithali 8 :13




πŸ› MUNGU AKUBARIKI SANA



Ni mimi

Mwlm.Peter Francis Masanja

Mtwara _ Tanzania



francispeter424@gmail.com




🎹🎹🎀🎀🎸🎸⛪⛪πŸ›πŸ›


Nakupenda sana 🀝🀝🀝

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*