KARAMA NA TUNDA LA ROHO MTAKATIFU


KARAMA NA TUNDA LA ROHO MTAKATIFU
(Gifts and Fruits of the Spirit)










UTANGULIZI:

I.                   Who is the Holly sprit? (huyu Roho Mtakatifu ni nani?) (kulingana na majina ya asili ya Roho mtakatifu yeye anaitwa ni Roho wa Mungu (Hebr. 9:14; Zab 39:7 – 10; Luka 1:35; Kor 2:10 – 11 ). Yeye anaitwa kwa sababu ana sifa za Mungu. Math 18 na pia Roho Mtakatifu ni mtu au nafsi kwa sababu ana sifa za ubinadamu.
II.                Yeye anaufahamu au kukumbuka (Rum 8:26 – 27)
        Yeye ana will – Ana mapenzi (1 Kor 12:11)
        Yeye ana feeling – Anaona (Efe 4:30)
        Yeye ana intercedes – Anatuombea (Rum 8:16)
        Yeye ana speaks – Anaamuru (Mdo 16:6-7, Uf 2:7)
        Testifies – Anashuhudia (Yn 13:26)

III.             Roho Mtakatifu anaitwa Roho wa Kristo, kwa sababu alitumw akwa jina la Yesu, (Yn 14:25; 1:12-13, 4:10, 7:28; Math 3:11).
        Pia Roho Mtakatifu anaitwa Roho wa kweli (Yn 14:17).
        Roho wa ahadi, Roho Mtakatifu aliahidiwa tokea kipindi cha Agano la kale (Ezek 36:27; Yel 2:28; Luk 24:49; Gal 3:14).
        Ni Roho wa kweli, n apia anaitwa ni ROho wa Neema, (Heb 10:29) Roho Mtakatifu anampa mtu Neema ya kutubu mbele za Mungu na pia anaitwa Roho wa uzima, (Rum 8:2; Uf 11:11).

IV.            Mifano ya Roho Mtakatifu au malinganisho ya Roho Mtakatifu.
        Yeye anaitwa moto inamaanisha kazi yake ni kusafisha, (Yer 20:9; Isa 4:4; Math 3:11; Luk 3:16).
        Yeye analinganishwa n aupepo, (Ezek 37;7 – 10; Mdo 2:2; Yn 3:8)
        Yeye  analinganishwa na maji (Ezek.37:7-10;Mdo.2:2; Yn. 3:8)
        Maji kazi yake kusafisha
        Yeye analinganishwa na mafuta (1 Sam. 10:6-10, 16:13).
        Pia hulinganishwa na hua kwa sababu ni mnyenyekevu na mpole.

V.               Kazi za Roho mtakatifu
        Kufundisha yote (Yn . 14:16-26)
        Kutuombea(Rum, 8:26-27)
        Hushuhudia kweli, huchunguza mioyo ya watu,(Yn, 15:26)
        Kutuongoza na kututia kwenye  kweli yote (Yn 16:13-15)
        Kutufanya kuwa mashahidi (Mdo1:8)

VI.            Kusudi la ubatizo wa Roho Mtakatifu
(a)  Kumgeuza mwanadmau kuwa mwingine (1 Sam. 10:6-7)
(b) Kumtia mtu nguvu na ujasiri ili awe shahidi anayefaa, (Mdo 1:8,4:31).
(c)  Kusaidia katika maombi (Rum 8:26 – 27)
(d) Kumjenga n akumuimarisha mtu wa ndnai (Yuda 20; Efe 3:16)
(e)  Kuhudumu katika karama za Roho Mtakatifu (1 Kor 12:4 – 12).
(f)   Kukupa ushindi juu ya mwili (Rum 8:13)
(g)  Kuwafunulia watu wake mambo ya Mungu (1 Kor 2:9 – 12).
(h) Kusaidia katika sifa na kuabudu (Yn 4:240.

VII.         Sababu gani zinazowafanya watu wasipokee ujazo wa Roho Mtakatifu?
1.     Kutokumjua Mungu, ujinga. (Mdo 19:2).
2.     Hofu, kutokujua.
3.     Tofauti za kimafundisho.
4.     Dhambi, Mungu atawapa Roho Mtakatifu wale tu walioamini na kumtii. (Mdo 5:32; 2 Kor 6:17b). 

VIII.      Nani anayestahili kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu?
(a)  Wote waliookolewa (Mdo 2:38-39)
(b) Watoto wote wa kiroho watakaoomba, (Luk 11:11-13)

IX.            Je, unawezaje kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu?
(a)  Lazima uwe umezaliwa upya yaani umeokoka, (Yn 14:17)
(b) Kutubu dhambi zote, maana Mungu hatumii chombo kichafu, (Mdo 2:38). Kuishi kama Mungu anavyotaka.
(c)  Kuenenda katika utii kwa Bwana. (Ef. 5: 18).
(d) Lazima utake uombe, utafute Roho Mtakatifu. (Luk 11:9-13).
(e)  Ingia katika kusifu, kuabudu hii itaufanya moyo uwe tayari katika kupokea Roho Mtakatifu. (Yn 4:23).

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU.

A: Makusudi ya karama za Roho mtakatifu . 
        Sababu ya kwanza ya kuwepo karama za Roho Mtakatifu ni kudhihirisha mwili wa Kristo juu ya dunia. Roho mtakatifu anatupa karama kama kanisa na nguvu za asili.
        Karama zinamdhihirisha Yesu katika ulimwengu wote kwa maana ya usikivu wa asili wa Mungu. Mwana na Roho Mtakatifu na hizi nguvu za asili zinawezesha Kanisa kubeba jina la Kristo duniani kote.  
        Kusaidia katika shughuli za uenezaji injili duniani kote, ikiwa kama agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Hili agizo ni kwa wote waaminio, (Mar 16:15 – 18; Mdo 1:8).
        Kufundisha kanisa kwa njia ya karama za Roho Mtakatifu au karama za Unabii na lugha mpya hasa inapotafsiliwa kama inavyoonekana. ( 1 Kor 14:5).

HUDUMA YA ROHO MTAKATIFU KATIKA VIPAWA – KARAMA ZA ROHO.

Kando ya mto wa uzima, matunda ya Roho na vipawa au karama za Roho vinaota na kustawi. Mfano huu wa fungu la kwanza unatusaidia kuelewa na kuanalia daima umoja na uhusiano wa huduma za Roho za kuzaa matunda na karama zake. Mto wenyewe ni mfano wa kipawa cha Mungu, yaani Roho Mtakatifu amabye anaotesha mimea ya kiroho ya kila upande wa Mto.

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU:

I.                   Mambo muhimu yanayohusiana na karama katika kazi ya utendaji wa karama  hizo.

1.     Karama hazizunguki kiholela kwa watu mbali mbali, bali mtu maalumu binafsi hupewa karama. (1 Kor 12:8 – 11).
2.     Karama hazifanyi kazi kama mtu anavyotaka, bali kama Roho Mtakatifu anavyoongoza. Hivyo usiigize wala kulazimisha kwa uamuzi wako wa utendaji karama.   
3.     Karama zinaweza kutumika vibaya. (Hes 20:7 – 13; 1 Kor 20:33). Kwani mwanadamu anahusika katika utendaji kazi sahihi.
4.     Karama huwa zinafanya kazi kwa ushirikinao, mfano karama ya Neno la Maarifa inaweza ikataja ugonjwa na hatimaye karama ya uponyaji ikauponya.

II.               Mambo muhimu yanayo husu watu wenye karama  
1.     Karama siyo kipimo maalumu cha kukua kiroho au utakatifu kwa sababu hata mkristo mchanga anaweza kupokea karama. 1Kor 1:4-7, 3:1-4)
2.     Mtu mwenye karama anaweza kukuoseaHivyo anahitaji afundishwe na kuonywa (Gal 2:11-14)
3.     Mtu aliepewa karama anaweza kabisa akatawala utendaji wa karama aliyopewa (1kor. 14:32) L
4.     Mtu mwenye karama ni tishio kwa shetani.Hivyo huwindwa sana ili aangamizwe, inabidi ajitunze kwa uangalifu , madahra ya uzembe ni onyo kama Samsoni, (Waam.14:1-21)


III.           Jinsi ya kupokea karama za roho mtakatifu

1.     Kwa kutaka sana karama .(1 kor .12:31, 14:1) inabidi umuombe Mungu akupe (1 kor 11:13).
2.     Kwa kuwekewa mikono na watumishi wenye karama , (1 Tim 4:14, Tim. 1:6).
3.     Kwa kuwa na ushirika na watu wenye karama, (2 Fal.2:1-15).

Maana ya karama na matunda ya Roho matakatifu( The meaning of Gift and fruits of the Holly Spirit)(1 kor . 12:1-3)

MAANA YA KARAMA
Neno karama ni kipaji au kipawa amabacho maana yake ni uwezo wa utendaji katika fani fulani unaopita hali ya kawaida ya watu wote.Karama za roho mtakatifu ziko tisa (9) tu. Ingawa Roho mtakatifu anaweza kuwapa watu vipaji mbalimbali, mfano, uimbaji n.k.Karama ya roho mtakatifu imegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:-
1.     Karama za ufunuo: Neno la hekima (ni kitu kikubwa kuliko Hekima ya mambo ya kawaida (Yk. 1:5, 3:17) Hufumbua mafumbo makubwa magumu, huchambua mambo yaliyojificha, huongoza kwenye maswala ya utanashati.
2.      Neno la maarifa: Karama hii ufunua mambo yaliyojificha au dhambi.
 (I Sam 10:23; 2 Sam 12:1-10) Mdo 11:27-28) siri za adui (2Fal 6:8-12) Huongoza (Mdo 9:11) hutaja mambo ya wakati ujao.

3.     Kupambanua Roho: Hufunua roho inayotenda kazi kama ni ya Mungu, ya shetani au ni ya mwanadamu.
  
                 Litaendelea............

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*