TAFSIRI YA NENO KIROHO
TAFSIRI YA NENO KIROHO
12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Waebrania 4 :12
NENO
👉 linaishi ( li hai )
👉 linanguvu
⇏ 👉 linakata
⇏ Linachoma
⇏linatambua makusudi ya moyo
⇏ Neno ni roho
⇏ Neno linakamata
⇏ Neno ni mtego
⇏ Neno linaumba
⇏Neno linajenga imani ndani ya mtu
⇏ Tuanze sasa kuona tabia za neno
⇏Kabla hatujaangalia sifa za neno unatakiwa ujue kuwa neno linaweza kumkamata au kumfunga mtu kwa kinywa chake mwenyewe kulingana na jinsi alivyojitamkia.
⇏Neno linaweza likatamkwa na mtu lakini likakukamata utakapokuwa umeamua kulisikia.
⇏ Kuna tofauti kati ya kusikiliza na kusikia.
⇏ Kusikiliza kunamfanya mtu afurahie tu sauti ya kitu fulani na asikumbuke tena .
⇒kusikia ni kushika kile ulichokisikiliza yaani neno
⇒Naomba niishie hapo turudi kwenye somo
⇒ Neno linaishi ,
⇒Neno lolote linaishi na linadumu
⇒ Neno la Mungu bado tunalihubiri kwa sababu linaishi
⇒Kama neno la Mungu linaishi na sisi tunaishi kulingana na neno hilo la Mungu kwasababu tulisikia linaokoa na tukaamini.
⇒Tunaishi kwa neno la Mungu kwa njia ya imani.
⇒ Neno linanguvu kwasababu
Nguvu za kiroho zimebebwa na neno.
⇒nguvu ya uponyaji imebebwa na neno.
⇒nguvu ya kumshinda shetani imebebwa na neno.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12 :11
Neno limebeba nguvu ya ushindi
Hata Yesu alipokuwa nyikani alipojaribiwa na shetani alimshinda kwa neno
Yesu alikuwa anajibizana na shetani kwa neno , akisema imeandikwa.
Je binti zetu leo wanawashambulia vijana kwa kuwaambia imeandikwa waasherati , waongo, wazinzi , wasengenyaji, na wasaliti hawatauingia ufalme wa Mungu ❓
Nataka nikwambie leo katika maombi yako jitahidi ujue unaombea nini na biblia inasemaje kuhusu hilo.
Neno linakata na linachoma
Watu wengi wanahama makanisa kwasababu kuna maneno wameyasikia yamechoma mioyo yao wakawa wamekata tamaa hata kusali.
Neno linachoma pia linauma kuliko fimbo
Ukichapwa fimbo unaweza kusahau lakini neno linachoma moyo na kumharibu mtu kiakili
Mchumba wako anakuandikia ujumbe wa ghafla.
mimi na wewe basi tena
Utajisikiaje moyoni mwako ukipokea neno hilo ❓
Lazima litakuchoma moyoni na wakati mwingine kama huna moyo mkuu unaweza ukafa hapohapo.
Neno baya linachoma na kuumiza moyo
Neno linatambua makusudi ya moyo.
Yesu aliweza kutambua makusudi ya Yuda Iskariote hata kabla ya kukamatwa akasulubiwe
Ndyo maana Yesu akamwambia Yuda ,
Rafiki fuata ulilolijia
47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Thenashara akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.Mathayo 26 :47
48 Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.Mathayo 26 :48
50 Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.
Mathayo 26 :50
Yesu aliyatambua makusudi ya Yuda hata kabla yake
Ione nguvu ya neno katika kutambua hila za adui
Neno ni roho
Kwahiyo neno kama ni roho inabidi uelewe kuwa linapatikana mahali popote na linasafiri
kama neno ni roho tambua kuwa sifa ya roho ni kukamata na kufunga maisha ya mtu
unaweza ukatamka neno kwa mtu au kwa watoto wako ambalo hilo neno ndani yake limebeba roho ya uharibifu
kuna baba mmoja baada ya kuona mkewake anamzalia watoto wa kike tu akamwambia mkewe anamzalia malaya .
😭 walipokuja kuvunja ungo hao watoto wote wakawa makahaba
roho ya ukahaba kupitia kinywa cha baba yao iliwakamata hao binti
Neno ni roho ikaayo ndani ya mtu
4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
Ayubu 26 :4
Huyo aliyetamka maneno ametamka roho gani ❓
Akitamka uharibifu ujue roho ya uharibifu itamfuatilia mlengwa wa hilo neno
Neno linatega na linakamata.
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Mithali 6 :2
Unaweza ukajitamkia kushindwa na maisha yako yakawa ya kushindwa tu
kila jambo unalojaribu kulifanya halifanikiwi kwasababu ulijifunga kwa maneno uliyojitamkia mwenyewe
Utasoma kitabu cha
HESABU 30
uone pia hatari iliyopo ukijitamkia maneno ya kushindwa
Hata kama ndoa yako inasumbuaje. , usitamke kuwa unajuta kuoa au kuolewa
Ukifanya hivyo utaendelea kujuta kila siku
Wadada wengi waliona wenzao wamesalitiwa wakajitamkia
Kwa hali hii sitaolewa , na leo hii wanajuta hawapati wenzi kwasababu walijifunga kwa maneno .
Neno ni nadhri / kiapo
Na sifa ya nadhiri lazima itolewe
Sasa binti ukijitamkia hutaolewa kwasababu ya kuona mazingira fulani ujue umeweka nadhiri ya kutokuolewa kabisa.
Neno linaumba
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.Mwanzo 1 :1
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.Mwanzo 1 :2
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.Mwanzo 1 :3
Tutaangalia
Roho na neno
Kuhusu uumbaji
roho ya uumbaji ilitulia juu ya uso wa maji
Neno la uumbaji lilipotamkwa yule roho akatimiza kazi yote
vivyo hivyo unapomwombea mgonjwa ukitamka uponyaji juu yake , roho ya uponyaji inafanya afya na uzima kwa huyo mgonjwa .
Haijalishi unatamka upo mbali kiasi gani , unatakiwa ujue ni nani unamtakia uzima hata kama yupo mikoa mingine atapona tu kwa sababu roho ya uponyaji itamfikia.
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.Yohana 1 :1
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.Yohana 1 :2
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.Yohana 1 :3
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.Yohana 1 :4
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
Yohana 1 :5
Neno unapolitamka linaumba
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
Mithali 18:21
Neno hujenga imani ndani ya mtu
Kuna vitu vingi hapa kwenye kujenga imani
MUNGU AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni