FAIDA YA KUFUFUKA KWA YESU
π FAIDA YA KUFA NA KUFUFUKA KWA YESU KATIKA MAISHA YAKO π
Mwlm.Peter Francis Masanja
The voice of God Ministry
0679392829
π«Bwana Yesu asifiwe
π» 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
Mathayo 27 :51
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
Mathayo 27 :52
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Mathayo 27 :53
βπ»Leo napenda nikushirikishe ili tuweze kuangalia faida za kifo cha Yesu pale msalabani pamoja na kufufuka kwake .
π» 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3 :16
π«Kwanza tutazame lengo kuu la Yesu kuletwa duniani ambalo kila mtu amwaminiye apate uzima wa milele .
π«Ilimpasa Yesu afe msalabani ili tuupate huo uzima wa milele .
π« Kupata kwake mateso ilikuwa si bure kabisa .
π«Damu ya Yesu iliyomwagika msalabani ilikuwa sadaka tosha kabisa kuweza kutukomboa sisi wanadamu na kutusafisha na uovu wetu .
π» 9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Ufunuo wa Yohana 5 :9
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Ufunuo wa Yohana 5 :10
π«Damu yake iliyomwagika msalabani ilitutoa kwenye nguvu za mauti na kutufanya kuwa warithi wa ufalme wa Mungu.
π«Kufa kwake na kufufuka kwake Yesu kulileta faida zifuatazo:
1β£ Alivunja kazi zote za shetani ( ibilisi )
π» 8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3 :8
π Tunajua kazi za ibilisi ni kumwangusha mtu asiweze kuuona ufalme wa mbinguni . Kwahiyo Yesu alikufa ili avunje kazi zote za shetani.
2β£ Aliharibu nguvu za mauti ambazo shetani anatumia kuwatesa watu wa Mungu .
π» 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Waebrania 2 :14
π«Kwahiyo kufufuka kwake leo amevunja nguvu za mauti za shetani kama vile mauti ya dhambi, mauti ya magonjwa n.k
3β£ Kwa kufufuka kwake tumepewa uwezo na mamlaka ya kufanya mambo makuu sana katika ulimwengu wa roho.
4β£ Kufufuka kwake kumetufanya tuwe pamoja naye katika mji mtakatifu tuungojeao .
π» 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
Mathayo 27 :51
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
Mathayo 27 :52
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Mathayo 27 :53
π«Kwahiyo nilipenda nikushirikishe katika somo hili la leo ili tupate kutafakari kwa pamoja kuhusu faida za ufufuo wa Yesu .
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Ubarikiwe
JibuFuta