FAIDA YA KUOMBA PAMOJA
* FAIDA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MAOMBI *
Mwlm .Peter Francis Masanja
The Voice of God Ministry
0679392829
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry
30 Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?
Kumbukumbu la Torati 32 :30
Ipo nguvu kubwa katika maombi ya pamoja .
Kupitia maombi ya pamoja mtu aliyekata tamaa hutiwa nguvu ya kuendelea kufanya maombi .
✍ Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.
Warumi 14:1
Maombi ya pamoja hufunika udhaifu wa mtu na kumtia nguvu.
Palipo na maombi ya pamoja upako au moto wa Roho Mtakatifu hushuka .
Palipo kusanyiko la watu waombao mtu inakuwa rahisi kunena kwa lugha .
✍ 1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
Matendo ya Mitume 2 :1
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Matendo ya Mitume 2 :2
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
Matendo ya Mitume 2 :3
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Matendo ya Mitume 2 :4
Zipo faida nyingi sana za kujumuika katika maombi lakini leo nilitaka tutafakari hizi mbili
1⃣ Kutiwa nguvu
2⃣ Kupokea upako wa Roho Mtakatifu ( nguvu ya kunena kwa lugha ) .
Kuna watu wakiomba wenyewe huomba mda mfupi sana na hawana bidii , lakini wakiwa kwenye kusanyiko la maombi ni mashujaa sana .
Katika tafakari yetu ya leo tunaona kuwa kuna wakati unatakiwa ushikiane na watu fulani ili Mungu akutendee mambo makuu .
Lazima uwe na rafiki yako wa imani wa kushirikishana naye katika mahitaji mbalimbali ya kuombea ili upige hatua .
Angalia huu mfano
1⃣Musa alikuwa na Haruni
2⃣ Yesu alishirikiana na Petro na Yohana .
3⃣ Pia tunawaona Shadrach, Meshach, na Abednego walitembea pamoja .
❓Je unarafiki mnayeshirikishana mambo mbalimbali ya kuombea ?
Kama huna chukua hatua kuanzia Leo .
Mungu akubariki sana .
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni