IJUE THAMANI YA ZAWADI

*ITUNZE NA KUIPENDA ZAWADI ULIYOPEWA*


Mwl.Peter Francis Masanja .
067392829
The Voice  of God Ministry
*Bwana Yesu asifiwe*
 Leo napenda tujifunze kuhusu thamani ya zawadi katika maisha yetu .
Zawadi ni kitu chochote ambacho utakipokea kutoka kwa mtu kama sehemu ya kujenga mahusiano maziri .
Zawadi ni zawadi tu hata iwe ndogo ni zawadi tu
Unapopewa zawadi maana yake ni kwamba huyo akupaye zawadi anakupenda , anakujali , na anakuthamini sana.

Zufuatazo ni zawadi ambazo Mungu alitupatia
1⃣ *UUMBAJI*
 24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Mwanzo 1 :24
25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 1 :25
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 :26
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1 :27
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 :28
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
Mwanzo 1 :29
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Mwanzo 1 :30
Mungu alituubia vitu vyote kama zawadi kwetu ili tuvitumie.
Hata kumwumba mwanadamu ilikuwa ni zawadi kwake Mungu .
Kwahyo uumbaji ni zawadi tosha kabisa , ulivyoumbwa na Mungu jithamini sana.
 13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Zaburi 139 :13
14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi 139 :14
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Zaburi 139 :15
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Zaburi 139 :16
2⃣  *MAISHA*
 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Mwanzo 2:7
Pumzi tuliyopewa ni zawadi tosha kabisa .
3⃣ *MAHUSIANO NA WATU WENGINE*
 3 Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Amosi 3 :3
Watu unaosaidiana nao ni zawadi toka kwa Mungu .
Mke uliyenaye au mime uliye naye ni zawadi ambayo Mungu kakupa mtunze , mpende , mjali na kumwona mzuri kila Siku.
4⃣ *YESU KRISTO NA KIFO CHAKE MSALABANI*
hii ni zawadi kubwa kuliko zote ambayo Mungu alitupatia maana kufa kwake msalabani tumepokea uzima wa milele
 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3 :16
Pia kufa kwake msalabani tumefanyika wana wa Mungu .
 32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
Warumi 8 :32
Kwahyo zawadi yoyote upewayo ni ya thamani sana .
Mungu akubariki sana .
https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*