KUJITOA KWENYE VIFUNGO VYA MANENO MABAYA

🔥KUJITOA KWENYE VIFUNGO VYA MANENO MABAYA ULIYOTAMKIWA NA MTU AU KUJITAMKIA MWENYEWE 🔥

Mwlm. Peter Francis Masanja

Mtwara _Tanzania

0679392829

francispeter424@gmail.com

The Voice of God Ministry





👨🏻‍💻📖 4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?

Ayubu 26 :4

👉Neno lolote ulilotamkiwa ni roho

👉Kama neno hilo ni roho basi ujue kuwa unenewa linafanya kazi maishani mwako sawasawa na lilivyotamkwa.

👉kwa kuwa neno ni roho , neno lolote baya ulilotamkiwa ujue linakamata mfumo mzima wa maisha yako .

👉Tambua kuwa neno baya ukitamkiwa ile roho ya uharibifu inakuja kwako kukukamata.

👉Ukitamkiwa kutokufanikiwa huwezi kufanikiwa kweli kama hujalitubia hilo neno na kulikata lisikukamate .

📖👨🏻‍💻 2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,

Mithali 6 :2

👉 Maneno yanakamata na pia yanashika

👉Neno lolote la kushindwa ukitamkiwa kama anayekutamkia unamsikia mkanye hapo hapo mwambie maneno yake hayatasimama usipofanya hivo yatathibitika kwako

👉Kama ulitamkiwa na mtu hutakaa uoe au hutakaa uolewe tambua kuwa unanafasi ya kutubu juu ya maneno hayo na kuyafuta kabisa yasifuatilie maisha yako

👉Kuna wakati unaweza kuona kuwa mume uliyenaye au mke uliye naye siyo sahihi kwako kumbe kuna mtu alikutamkia kuwa hutakaa kwenye ndoa yako ukaifurahia .

👉 Ndoa nyingi zinaingia migogoro kwa sababu ya maneno mabaya yaliyotamkwa juu yake .

📖👨🏻‍💻 29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Yeremia 22 :29

30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.

Yeremia 22 :30

👉Itazame hiyo familia imetamkiwa kutokufanikiwa kabisa

👉 Utaona ardhi ( nchi) imetekeleza yale matamko na kuwafanya watu wakaao hapo kutokufanikiwa kabisa .

👉Lazima uyafute maneno yote mabaya uliyotamkiwa na watu kwa kusikia na kwa kutokusikia .

👉Ninakwambia ujifungue utoke kwenye vifungo vya maneno nikimaanisha kuwa neno lolote ukitamkiwa ujue linaumba .

📖👨🏻‍💻 1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Mwanzo 1 :1

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mwanzo 1 :2

3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Mwanzo 1 :3

👉Tambua kuwa Mungu aliumba vitu vyote kwa neno

👨🏻‍💻📖 1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1 :1

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Yohana 1 :2

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1 :3

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1 :4

5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.

Yohana 1 :5

👉 Kwa maana hii basi mtu akikutamkia neno litakuwa sehemu ya maisha yako usipolifuta kwa maombi( toba ).

📖👨🏻‍💻 9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama.
Zaburi 33 :9

10 Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.

Zaburi 33 :10

👉Neno lolote ukijitamkia au kutamkiwa linasimama juu yako
👉Ukijitamkia kushindwa utashindwa kweli kweli .

*🛐SOMA SALA HII 🛐*

🛐 Bwana Yesu , ninakuja mbele zako .
Ninakuomba unisamehe maana nimejitamkia maneno mabaya ya kushindwa.

🛐Nirehemu ee BWANA , maana sikukujua lakini sasa nimejua makosa yangu juu ya maneno mabaya niliyojitamkia.

🛐 Nakuomba uyafute maneno mabaya niliyojitamkia katika maisha yangu , katika jina la Yesu .

🛐Ninaomba uwasamehe hata wale walionitamkia maneno mabaya juu ya familia yangu , biashara zangu, ndoa yangu , elimu yangu n.k

Ee Mungu uyafute maneno yao mabaya , waliyonitamkia kwa kujua na kwa kutokujua. Kwa damu ya Yesu futa maneno yao kuanzia sasa , maana imeandikwa:

👨🏻‍💻📖 10 Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
Zaburi 33 :10

11 Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.

Zaburi 33 :11

Nami nakuomba maneno niliyotamkiwa uyafutilie mbali katika maisha yangu , familia yangu , ndoa yangu n.k bali neno lako likasimame daima maishani mwangu katika jina la Yesu .Amen

🔥Katika jina la Yesu , ninasema kama ilivyoandikwa;

📖👨🏻‍💻 7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.

Isaya 7 :7

Ninaamuru kila maneno mabaya kutokusimama katika maisha yangu na ndoa yangu , familia yangu , elimu yangu n.k

Maana imeandikwa:

📖👨🏻‍💻 10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

Isaya 8 :10

👉ninayaamuru maneno yote mabaya niliyotamkiwa na niliyotamkiwa kuwa batili , katika jina la Yesu.

🔥Ninaamuru kila maneno mabaya na roho ya uharibifu kuachia maisha yangu , katika jina la Yesu nina yavua mavazi ya maneno mabaya kwa damu ya Yesu .

📖👨🏻‍💻 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.

Waebrania 9 :22

Asante Bwana Yesu kwa kuwa unasikia kuomba kwangu nami najikabidhi mikononi mwako sasa na hata milele .Amen

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*