KUMTAMBUA ALIYE NA VITA YA UKOO
*KUMTAMBUA MTU MWENYE VITA YA KIUKOO *
Mwlm.Peter Francis Masanja
Mtwara _Tanzania
francispeter424@gmail.com
Inawezekana kuna mpendwa ameokoka peke yake katika ukoo wake au familia yake
Mtu ambaye kaokoka kutoka kwenye familia za wasiookoka huwa na vita kali sana .
Mtu huyo hufuatiliwa sana na mashambulizi ya miungu ya ukoo na wakati mwingine kutafta kumuua kabsa
Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;
Zaburi 116:3
mtu aliyeokoka kwenye familia ambazo wanaabudu mizimu anahitaji asimame sana katika maombi ili anusurike na miungu ya ukoo
Lazima atambue kuwa kama alishawahi kuchanjwa chale na kula chakula cha matambiko ajue kuwa hizo ni kamba amefungiwa na inabidi azikate ( azifungue ) na kuzitupa
Kamba hizo lazima zifunguliwe kwa njia ya toba na maombi .
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
Isaya 10:27
Elewa pia kuwa mtu huyo amefungiwa nira na miungu ya ukoo hivyo basi inabidi iondolewe na njia pekee ya kuiondoa ni maombi .
_DALILI ZA MTU ALIYE KWENYE VITA YA UKOO
1⃣ Kuota ndoto unafanyishwa kazi nyumbani ulikozaliwa .
2⃣Kutokuelewana na ndugu zako
3⃣ Kudhihakiwa na ndugu zako
4⃣ Kuota unakimbizwa na nyoka au unatumbukia shimoni
5⃣ kuota ndugu zako wanatambika
6⃣Kuota unagombana na ndugu zako
Hizi ni baadhi ya viashiria vya kuwa mtu yupo kwenye vita na miungu ya ukoo .
Watu ambao nyumbani kwao au katika ukoo wao kuna mbuzi au ng'ombe wamepewa majina ya watu na kufungwa kengele huwa wanapata tabu sana kiroho .
Utakuta jina la ukoo unaloitwa kuna mbuzi au ng'ombe anaitwa jina hilo hilo na wamemfanya huyo mnyama kama njia ya kufikisha maombi yao kwa miungu ya ukoo .
SULUHISHO JUU YA VITA VYA UKOO
1⃣ MAOMBI YA TOBA.
Toba kwaajili yako mwenyewe
*SOMA SALA HII*
BWANA YESU asante kwa damu yako iliyomwagika msalabani kwaajili yangu .
Nimekuja mbele yako Mungu mwenye enzi yote na mamlaka yote , ninatubu dhambi zangu zote nilizozitenda kwa makusudi na pasipo makusudi .
Kwa damu ya Yesu naomba unioshe na kunisafisha na kila uovu nilioutenda katika maisha yangu eeh Mungu utakasaye ( Jehovah maccadeshem ).
Nakusihi ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu nakuliandika jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele.
Lifute jina langu kwenye kitabu cha laana na uliandike kwenye kitabu cha baraka kwa jina la Yesu.
Kuanzia leo ninatoa mwili wangu ,nafsi yangu na roho kwako ee Bwana Yesu.
Roho Mtakatifu karibu ndani yangu na uweza wako unipe nguvu za kushinda dhambi kwa jina la Yesu .AMEN
Toba kwa ajli ya waliokutangulia ( wazazi , babu na bibi )
Kumbuka toba hii ni pande mbili yaani ukoo wa baba na ukoo wa mama yako
29 Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.
1 Wafalme 21 :29
Mwangalie Ahabu alipotubu utajifunza kitu kizuri sana kuhusiana na toba
Unapotubu unapangua mabaya yasikupate
Unapotubu juu ya waliokutangulia unapangua mabaya ya kurithi yasikupate kabisa
Ikiwa ni magonjwa , mikosi na kila aina ya laana mfano kutokuolewa au kutokukaa kwenye ndoa ukafurahia
Haya yote ni mabaya yanahitaji toba .
Inawezekana ndoa yako inasumbua au uchumi wako unasumbua sana kumbe tatzo ni waliokutangulia na cha ajabu umeyarithi mabaya yao .
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.
Maombolezo 5 :7
Lazima ujitenge na uovu wa baba zako na mababu zako pia ili uweze kufanikiwa
[3/9, 11:53] Rev.Peter Francis: *SOMA SALA HII
BWANA YESU ninakuja mbele zako masihi .
Ninazileta mbele zako dhambi za baba yangu na mama yangu pamoja babu zangu wa upande wa baba na mama yangu.
Ninatubu na kuziungama dhambi zao , kwa maana walikutenda dhambi .
Naziungama dhambi zao zote za kuua binadamu wezao , kuabudu sanamu, kuuza na kununua wanadamu, kutoa kafara za watu kwa miungu ya sanamu, kula nyama za watu , uasherati, uzinzi na kila matendo ya giza waliyoyafanya .
Nakusihi uwarehemu na kuwahurumia juu ya uovu walioutenda .
Ninawasamehe makosa yote waliyonitendea kwa kujua na kutokujua katika jina la Yesu .
Ninaomba uzisahau dhambi yao yote katika kizazi changu .
Baba siyapendelei makosa na uovu wao wote , kwahiyo ninajitenga mwenyewe kutoka kwenye adhabu ya makosa hayo ee Bwana kama ilivyoandikwa :
✍ 20 Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
Zaburi 68 :20
Nakuomba Mungu unitoe kwenye mauti ya dhambi zao katika jina la Yesu.AMEN
Toba kwa ajili ya watoto wako na uzao wako
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;
✍✍✍✍✍✍✍✍
nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kutoka 20 :6
Tubu juu ya watoto wako na uzao wako ili uwe na kizazi kizuri
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni