KUNA WATANO LAZIMA UWAITE KABLA YA MAOMBI
KUNA WATANO LAZIMA UWAITE KABLA YA MAOMBI
Mwl. Peter Francis Masanja
The Voice of God ministry
19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 18 :19
Mathayo 18 :19
20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Mathayo 18 :20
Bwana Yesu asifiwe sana
Leo nitazungumzia hawa watano ambao unatakiwa uwaite kabla ya kuingia kwenye maombi ya kupambana .
1⃣Uwepo wa Mungu
Lakini Bwana yu pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Yeremia 20:11
Kabla ya maombi ita uwepo wa Mungu ili akufanye kuwa mshindi
45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
1 Samweli 17 :45
Tunamwona Daudi alimtanguliza Mungu kabla ya kupigana vita
Ndyo maana alishinda.
_2 ⃣ ITA JINA LA YESU_
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Wafilipi 2 :9
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
Wafilipi 2 :10
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Wafilipi 2 :11
Kuna ushindi mkuu ndani ya jina la Yesu kwahiyo yakupasa uliite kabla ya kuanza maombi mwite Yesu awe pamoja nawe .
_*3 ⃣ ITA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU*_
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8 :26
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8 :27
Roho Mtakatifu ni mwalimu wako.
Mwambie awe pamoja na wewe katika maombi akufundishe na kukuongoza katika kupigana vita dhidi ya adui
_*4⃣ JESHI LA MALAIKA WA VITA KUTOKA MBINGUNI*_
10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde;
Luka 4 :10
11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Luka 4 :11
Jeshi la malaika kutoka mbinguni unatakiwa uliite nifanye ulinzi juu yako ili adui asikuharibie maombi yako .
Katika anga, bahari na katika ardhi mwambie Mungu atume jeshi la malaika kutoka mbinguni wafanye ulinzi na kuhakikisha ufalme wa giza haufanyi vikao dhidi yako
Malaika wa Bwana wanafanya kazi ya kusambaratisha na kuangamiza majeshi ya pepo wabaya
Na nataka ujue kuwa kuna wapelelezi kutoka kuzimu ambao ni wanaweza kuiba siri za maombi yako na kupeleka kuzimu ili badae waje kama malaika wa nuru kwa dhumuni la kukuangamiza
Ndyo maana jeshi la malaika kutoka mbinguni unapaswa kuliita ili liwakomeshe hao wapelelezi wa maombi
Wapelelezi wa maombi huja kwa sura mbalimbali bila wewe kujua
wengine huja kwa sura ya ndege , paka, panya , nakadhalika
Hawa lazima uliambie jeshi la malaika kutoka mbinguni liwashughulikie .
Hawa lazima uliambie jeshi la malaika kutoka mbinguni liwashughulikie .
_5⃣ ITA AU JIFUNIKE NA DAMU YA YESU*_
Damu ya Yesu inazima mishale ya adui
Hakikisha unajifunika na damu ya Yesu kabla ya kuongia kwenye maombi
Funika eneo unalofanyia maombi , vitu na malizako zote , ndugu zako na familia yako mke wako au mume wako kabla ya maombi ili shetani asipate nafasi
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12:11
Ndani ya damu ya Yesu kuna ushindi
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni