KWANINI UYASIMULIE

*📖KWANINI UYASIMLIE ❓*

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

francispeter424@gmail.com

💻📖 4 Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za Bwana, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.

Zaburi 78 :4

5 Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao,

Zaburi 78 :5

6 Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao .

Zaburi 78 :6

7 Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake.

Zaburi 78 :7

💫Unakila sababu ya kuyasimulia yale makuu aliyokutendea Mungu ili kupitia wewe wengine waamini kuwa Mungu anaokoa na anao uweza mkuu sana.

💫 Unakila sababu ya kuyasimulia matendo makuu ya Mungu ili Mungu akupe kibali cha kuwa mshindi katika vita inayokukabili .

📖💻 6 akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.

2 Mambo ya Nyakati 20 :6

7 Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele?

2 Mambo ya Nyakati 20 :7

9 Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni, au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako, (maana jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, nawe utasikia na kuokoa.

2 Mambo ya Nyakati 20 :9

💫Jenga tabia ya kumshuhudia Mungu kwa makuu aliyoyatenda zamani yaani ishara na maajabu ili apate kukutendea mambo ya viwango vya juu katika maisha yako .

💫Ushuhuda ni njia inayomfanya Mungu asikie kilio chako ( maombi yako ).

💫Usichoke kuusimulia ukuu wa Mungu kwa watu wote .

Mungu akubariki sana

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*