MAOMBI YA ULINZI
💒MAOMBI YA ULINZI
Mwlm Peter Francis Masanja
The voice of God Ministry
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
Isaya 62 :6
👉 Baba katika jina la Yesu , achilia nguvu yako , mamlaka yako,na uweza wako juu ya yule baba, mama, kaka na dada katika familia yake usiku huu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.Amen
👉Katika jina lipitalo majina yote la BWANA wetu YESU KRISTO wa Nazareth tunaagamiza kila silaha iliyotengenezwa toka kwenye ufalme wa giza kumdhuru yule baba mama , kaka na dada pamoja na familia yake , tunawasambaratisha wote waliokaa ili kumtumia mabaya na mateso ,tunawaangamiza hata majini na mapepo na wanyama , wadudu au ndege waliotumwa kuleta mabaya wakati wa kulala katika jina la Yesu .
15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
Isaya 54 :15
16 Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.
Isaya 54 :16
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
Isaya 54 :17
👉 Tunaondosha kila pigo na nguvu za mauti kwa yule baba, mama, kaka , dada pamoja na familia yake katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
👉Ee roho ya Mauti , mauti ya magonjwa kwenye macho , tumbo , kichwa , masikio , kifua, moyo , milango ya uzazi , miguu , mikono , uti wa mgongo , ngozi n.k .Tunakuamuru katika jina la,Yesu toka , achia mwili wa yule baba,mama, kaka,dada ,na familia yake na marafiki zake , roho ya mauti hutainuka tena tunakuseta kuzimu katika jina la Yesu .
👉Wasimamizi wa ndoto mbaya , majoka ,roho za wafu, matambiko , majeneza na makaburi imeandikwa hivi
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
14 Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
Hosea 13 :14
toka katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
👉Naamuru kila roho za mapepo na majini kuangamizwa kwa damu ya Yesu , ninaamuru kila nira ya magonjwa kutoweka kwenye mwili ,nafsi na roho ya yule baba mama na familia yake katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
27 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
Isaya 10 :27
👉 Tunamweka huru na kumfunika kwa damu ya Yesu Kristo wa Nazareth .Amen
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Isaya 61 :1
2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Isaya 61 :2
3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.
Isaya 61 :3
👉MUNGU AKUBARIKI
💒Rev.Peter Francis💒
0679392829
0744056901
francispeter424@gmail.com
AYUBU 22:21
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni