MTEGEMEE MUNGU
📖📖📖📖📖📖📖📖
*📖UNAMTEGEMEA NANI KATIKA SHIDA ZAKO ❓*
Voice of God ministry ⛪
📖👨🏻💻 1 Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia.
Zaburi 120 :1
👉 mpendwa unapaswa kumwangalia Mungu katika kila shida unayoipata hapa duniani.
👉 Mungu ndye kila kitu maishani mwako
👉 mtegemee sana maana yeye ndyo msaada wako.
📖👨🏻💻 1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
Zaburi 121 :1
2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
Zaburi 121 :2
👉 Ni kweli hapa duniani tunasaidiwa na watu lakini siyo kila msaada ni halali
👉Kuna misaada mingine inatoka kuzimu haitokani na Mungu .
👉Mpendwa usiharakie kupokea msaada toka kwa mtu misaada mingine inamasharti magumu ambayo yanakuingiza kwenye dhambi .
🙆🏽♂ Kwa mfano binti unatafta kazi unatembea na bahasha za vyeti vyako kila siku hufanikiwi kupata kazi lakini akatokea bosi anakwambia ili upate kazi lazima uzini naye
Mkimbie huo sio msaada ni ushetani_ .
👉 Mtegemee Mungu naye atakuletea watu sahihi wa kukusaidia maishani mwako tena watakuja wenyewe na siyo kwa kuwatafta .
📖 Nakutangazia mwaka wa mafanikio maishani mwako katika elimu,biashara ,na afya yako iwe imara
Amen
MUNGU AKUBARIKI SANA
Ni mimi
Peter Francis Masanja
Mtwara_Tanzania
0679392829
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni