MTEGEMEE MUNGU
*📖 MTEGEMEE MUNGU UPATE UZIMA 💻*
👉 Umepitia majaribu mbalimbali mwite Mungu .
👉Usimtegemee mwanadamu kama kinga yako
👉Mwanadamu hawezi kulinda roho yako bali Mungu akupaye pumzi ya uhai anaweza mtegemee yeye peke yake.
📖💻 5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Yeremia 17 :5
👉 Msaada wako utegemee kwa Mungu .
👉Siyo kila shida umwambie mwanadamu ataishia kukusema na hakusaidii anaanza kueneza shida zako .
📖💻 1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
Zaburi 121 :1
2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
Zaburi 121 :2
3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;
Zaburi 121 :3
MUNGU AKUBARIKI SANA
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
francispeter@gmail.com
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni