MUNGU AKUONGOZE
*📖💻MUNGU AKUONGOZE 📖📖*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
📖 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Isaya 48:17
👉Siku zote bila Mungu huwezi kuwa na dira nzuri ya maisha .
👉Utakuwa unatembea bila kujua unaelekea wapi
👉 Utakuwa hupati faida yoyote ya uumbaji ambao Mungu alikupatia ili uishi hapa duniani .
💫 Nakuombea kwa Mungu ili maisha yako yamtegemee yeye katika kila jambo ulifanyalo.
👉Unataka upate faida katika jambo fulani ? Anza na Mungu kwanza ili aachilie kibali .
💫 Unataka utajiri ?
Mwangalie Mungu katika miradi yako yote ili akupe nguvu ya kuupata huo utajiri .
📖💻 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Kumbukumbu la Torati 8 :17
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8 :18
👉nguvu ya kupata utajiri ipo kwa Mungu peke yake
👉Utajiri unaopewa na Mungu ni wa kudumu .
👉Utajiri kutoka kwa shetani siyo wa kudumu .
📖💻 8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.
Hagai 2 :8
👉Mungu amekuandalia kila kitu lakini anahitaji umtumikie ili akupe .
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni