MUNGU NDIYE MLINZI WAKO
📖 MUNGU NDIYE MLINZI WAKO
Mwlm.Peter Francis Masanja
Mtwara _ Tanzania
📖💻 7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
Zaburi 121 :7
8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
Zaburi 121 :8
👉Kuna watu tuna walinzi wetu tumewaweka lakini hawawezi kulinda roho zetu
👉 Mwanadamu hawezi kulinda roho yako ila Mungu analinda roho yako.
👉unatakiwa umtegemee sana Mungu akulinde kuliko kuwategemea wanadamu ambao hawawezi kukulinda na magonjwa wala hawawezi kukuepusha na ajali.
👉Ni jambo la aibu kumsahau Mungu na kutegemea ulinzi wa wanadamu tena ni laana .
📖💻 5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Yeremia 17 :5
👉Mtegemee Mungu katika kila jambo ili uwe salama.
👉 Utategemea mganga wa kienyeji ambaye anakufa mpaka lini ❓
Yupo Mungu aliye hai milele ndye mlinzi wako .
📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖
Mungu akubariki sana
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni