NGUVU YA IMANI

*🤝NGUVU YA IMANI KATIKA MAOMBI 🛐*

Mwl. Peter Francis Masanja

0679392829

francispeter424@gmail.com

The Voice of God Ministry

📖💻Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Mathayo 8:8

💫Tunamwona huyu akida aliamini kuwa Yesu anaweza kuachilia uponyaji bila kufika nyumbani kwake .

💫Kwa hiyo hata upo mbali kiasi gani ukiamini kuwa Mungu anafanya atakutendea sawasawa na haja ya moyo wako.

📖💻 10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

Mathayo 8 :10

💫Yesu alistaajabu kumsikia yule akida akimwambia aseme neno moja tu na mtumwa wake atapona

💫Huyo akida aliamini kabisa kuwa uponyaji hauangalii umbali

💫Hiyo ilikuwa ni imani kubwa sana katika jina la Yesu .

Yule akida hakuwa na mashaka .

💫Leo tunashindwa kupokea tunacho kihitaji kwa sababu ya mashaka

📖💻 38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Waebrania 10 :38

💫Kinachotufanya tusifikie viwango vya maisha ambayo Mungu ametukusudia ni kukosa imani kwa yale tumwombayo Mungu.
.
💫 Imani yako inamfamya Mungu ajibu au asijibu maombi yako .

💫Mungu anaangalia imani iliyomo ndani ya moyo wako ili akujibu

💫Kumbuka kuwa kuomba huja kwa imani

Na kupokea huja kwa imani

📖💻 7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)

2 Wakorintho 5 :7

💫Nataka ujifunze kuwa uaminicho ndicho Mungu atakupa

💫Ukiamini kupokea kidogo utapewa kidogo

Ukiamini kuwa Mungu anakupa nguvu ya kupokea vitu vikubwa atakupatia.

💫Unapoona mtu anasema atakuja kumiliki gari ujue hiyo ni imani

💫Sasa ili aipate hiyo gari ataweka bidii ya kufanya kazi huku akimtanguliza Mungu .Hii tunaita imani na matendo.

📖💻 4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Waebrania 11 :4

5 Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.

Waebrania 11 :5

💫Wangapi huwa wanaiombea sadaka na kumwambia Mungu shida zao kupitia sadaka ❓

💫Kabla hujaenda kanisani sema shida zako zote kupitia sadaka hiyo unayoenda kumtolea Mungu

💫Amini kuwa sadaka inanguvu kwenye maombi yako ni vyema ukaishika mkononi ukamwambia Mungu kupitia sadaka hii naomba unifanyie yafuatayo .

💫Usiitoe sadaka kama desturi tu ya kanisa lako.

💫Weka imani katika sadaka yako kuwa Mungu anajibu maombi yako

💫Habili alimtolea Mungu sadaka kwa imani akabarikiwa sana .

💫Ili maombi yako yajibiwe omba kwa imani

💫Usiwe na mashaka amini kuwa Mungu anajibu.

📖💻 25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,
Marko 5 :25

26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya
Marko 5 :26

27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
Marko 5 :27

28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
Marko 5 :28

29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.
Marko 5 :29

34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Marko 5 :34

💫Yule mwanamke aliyetokwa damu miaka mingi aliweka imani kuwa akigusa pindo la vazi la Yesu atapona .

Hii ilikuwa ni imani katika uweza wa jina la Yesu.

: 💫Changamoto unazopitia zisikutisha amini Mungu atakupandisha viwango vya juu omba atakujibu

Mungu akubariki sana tukutane siku nyingine

https://peterfrancismasanja.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*