NGUVU YA KUISHINDA DHAMBI
*🔥NGUVU YA KUISHINDA DHAMBI 🔥*
💫DAY ONE 🔥
Mwlm.Peter Francis Masanja
0679392829
The Voice of God Ministry
📖💻 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
Warumi 6:12
👉Mpendwa ili mtu aweze kuishinda dhambi lazima atambue kuwa amepewa mamlaka ya kuishinda dhambi
👉Na mamlaka ya kuishinda dhambi yamo ndani ya Yesu .
📖💻 5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
1 Yohana 3 :5
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
1 Yohana 3 :6
👉 Kanuni kuu ya kushinda dhambi ni kukaa ndani ya Yesu .
👉Yesu alikuja duniani kuzivunja hila zote za shetani maana shetani ndiye mwanzilishi wa dhambi na baba wa uovu wote duniani .
💻📖 8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3 :8
👉Kwahiyo inakupasa umkaribishe Yesu akae ndani yako ili usitende dhambi .
👉Ukikaa ndani ya Yesu kuna uzima na unafanyika kuwa mwana wa Mungu.
💻📖 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1 Yohana 3 :9
10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
1 Yohana 3 :10
👉Mpendwa dumu sana katika kusoma neno na kulifanyia kazi ili uweze kufanikiwa kumshinda shetani na kazi zake
Mungu akubariki sana
Nitaendelea siku nyingine .
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni