SEMA NA VIJANA
JUKUMU LA KIJANA
The Voice of God Ministry
francispeter424@gmail.com
😭😭😭nawalilia vijana waliobeba dhamana ya kutumika lakini hawataki
👉Ni dhambi kuacha kuhuniri injili 😭😭😭😭
📖💻
''
......Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu."
1 Yohana 2:13
👉Leo vijana badala ya kumshinda shetani wamekuwa watumwa wa dhambi
👉Vijana wamepoteza dira ya maisha shetani amewameza
📖💻 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
1 Petro 5:8
👉vijana wengi hawana kiasi na hawakeshi na shetani amewameza
😭😭😭tutapataje kupona kama vijana hawajibidiishi na kuomba 🙋🏻♂
💻📖 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
Waebrania 2:3
😭😭tutaponaje ikiwa vijana hawapendi kujishughulisha na mambo ya Mungu .
😭😭ndoa zetu zitapataje kupona ikiwa tunaamka na kumshukuru Mungu kwa kutupa afya na uzima huku tunasahau kuziombea ndoa😭😭😭😭
💻📖 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Marko 16:15
👉Kijana umeagizwa kuhubr injili
👉Kwanini unasema huwezi kumwimbia Mungu 😭😭😭😭
😭😭Huku nyimbo za dunia unaziimba sana lakini kanisani umekataa kwaya .
👉jua wito wako usipo zaa matunda mbele za Mungu utakuwa tawi lisilozaa matunda
👉Ukiwa mhudhuriaji tu kanisani huna karama au kipawa chochote unapoteza mda wako bure shetani amekunasa kijana
👉Kwenye kikundi cha maombi haupo
👉 kwenye kwaya haupo .
👉Kwenye kusifu na kuabudu haupo
👉 Hata uinjilist na ushauri haupo
.
Mpendwa ujue mbinguni huingii 😭😭😭😭
👉kijana lazima utumike usilete sababu za kuwa huwezi hakuna aliyezaliwa anaweza
👉 Inawezekana unaogopa kuhubiri kisa hutaki kutazamwa na watu unaona aibu
👉 ukiogopa kufanya kazi ya Mungu mbinguni hutaingia 😭😭😭
👉waoga hawatauona ufalme wa mbinguni
📖💻 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo wa Yohana 21:8
😭😭unaweza kuhubiri lakini unasema unaogopa , utapataje kupona ❓😭😭😭😭
👉kijana kutumika mbele za Mungu ni lazima siyo ombi
👉ukitumika unakuwa kijana safi sana mbele za Mungu
💻📖 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Zaburi 119:9
👉Ili njia ya kijana iwe safi lazma atii na kufuata sheria za Mungu.
👉Hakuna kijana aliyewahi kuwa salama bila kutumika mbele za Mungu
👉Hakuna mahusiano yaliyowahi kubaki salama bila kumtumikia Mungu
👉Usalama wa kijana ni kutumika mbele za Mungu
👉 usalama wa Daniel kwenye tundu la simba ulikuwa ni kwa sababu alitumika kwa Mungu .
👉Daniel alisali mara tatu kwa siku wewe unasali mara moja kwa wiki utaponaje ❓
📖💻 10 Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Danieli 6 :10
👉Danieli alitumika ndyo maana alipata kibali pia akawa waziri mkuu
👉Je utapataje kibali ofisini kwako kama umepungukiwa maombi ❓
👉Utaishia kuona aliyekukuta anapanda cheo lakini wewe hupandi
Kumbe hutumiki kwa Mungu
👉 Inafikia hatua hata kuongoza ibada nyumbani kwako huongozi unafikiri hapo kijana utapona 😭😭😭
👉Ni lini mlishikana mikono na mke wako mkaombeana ❓
Na kama hamfanyi hivyo mnafikiri hiyo ndoa inaupendo 😭😭😭
👉Ndoa za vijana hazidumu kwa sababu baada ya kuoana wanamsahau Mungu na kufuata tamaa zao 🙆🏽♂🙆🏽♂🙆🏽♂
ukiona ndoa ya vijana wachunguze inawezekana wamemwacha Mungu wanaendesha ndoa kwa akili zao tu .
👉ukiona mtu mgomvi na mtukanaji ujue amemsahau Mungu
Yaani hatumiki maana yake haishi kwa neno la Mungu
💻📖 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Wagalatia 5 :16
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
Wagalatia 5 :19
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
Wagalatia 5 :20
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wagalatia 5 :21
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
Wagalatia 5 :22
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Wagalatia 5 :23
24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Wagalatia 5 :24
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Wagalatia 5 :25
👉Wewe kijana kama ukikwazwa unatukana unafikiri upo sawasawa na Mungu 😭😭😭
👉Kijana lazima utumike mbele za Mungu ili uwe mti mwema uzaao matunda
👉 Itambue faida ya kutumika mbele za Mungu
1⃣ Ukitumika mbele za Mungu utapata kibali ( utakubalika )
2⃣ Utapata ulinzi
👉 katika kibali utamiliki na kutawala
👉Nabii Yeremia alipokubali kutumika kwa kazi ya Mungu alipata vibali vifuatavyo ✍🏻✍🏻✍🏻
YEREMIA 1:10
1⃣Kung'oa
2⃣kubomoa
3⃣ Kuharibu
4⃣Kuangamiza
5⃣Kujenga
6⃣Kupanda
👉alipewa vibali sita ( 6 )
👉Alikuwa kijana mdogo sana lakini angalia zawadi aliyopewa na Mungu
Vibali sita ni vyake tu 😊😊😊😊
👉ukikubali kutumika lazima Mungu akupe uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makuu 😊😊😊
👉Wale mitume walipotumika walipewa mamlaka ya kutoa pepo na kuponya magonjwa na udhaifu wa kila namna 😊😊😊
👉Na wewe kijana ukikubali kutumika utapewa uwezo mkubwa katika eneo ambalo unatumika
👉 kama wewe ni mwimbaji weka bidii katika kumwimbia Mungu naye atakupatia uwezo wa kufanya kazi yako kwa viwango vya ubora wa hali ya juu.
👉Na ukiwa mwanamaombi sana unauwezo wa kumwambia Mungu ahamishe bar kama ipo mtaani kwako itakufa.
👉kwahiyo tafta kutumika mbele za Mungu
👉Haiwezekani usiwe na eneo la kutumia mbele za Mungu lazima uwe nalo tu .
📖💻 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Wakolosai 3 :16
Mwl.Peter Francis Masanja
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni